Serikali yapiga marufuku usambazaji wa sukari ya KK na kuiondoa sokoni mara moja

Akiongea na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Viwanda na Biashara ndugu Kaijage,amepiga marufuku mara moja matumizi ya sukari aina ya Kijiko Kimoja (KK) bila ushauri wa daktari.

Sukari hiyo aina ya KK imeamuliwa kurudishwa Dsm toka katika mikoa ya Kigoma,Bukoba na Mwanza ambapo tayari ilishaanza kuuzwa.

Waziri Kaijage anasema sukari hiyo inapaswa kuuzwa kwenye maduka maalumu(Super markets) na Maduka ya dawa Maalumu(Pharmacy) kwa sababu matumizi yake yanahitaji ushauri wa daktari kwa mtumiaji.

Kaijage anasema madhara ya sukari hiyo ni pamoja na kuharibika kwa mimba changa kwa wanawake wajawazito na madhara mengine makubwa ya kiafya.

Sukari hiyo imeamuliwa kutolewa kwenye magodown yote eneo la kanda ya ziwa na mkoa wa Kigoma na kurudishwa Dsm.

Mamlaka husika kama TFDA,TRA,TBS,Wizara ya Afya na mamlaka za Wizara ya Viwanda na Biashara zimeamuliwa kuiondoa sokoni sukari hiyo haraka iwezekanavyo na msambazaji kuacha mara moja kusambaza sukari hiyo kwa wananchi kwani ina madhara makubwa.

Licha ya kuwa Taifa lina uhaba mkubwa wa sukari,lkn serikali haipo tayari kuangamiza afya za watu wake kwa kuruhusu sukari isiyo "rafiki" kwa afya na maisha ya watu.Sukari ya KK inasemwa kuwa na utamu usio wa kawaida,kijiko kimoja tu cha sukari kinaunga kikombe cha ujazo wa lita moja ambayo ni hatari kwa afya.

View attachment 358650 View attachment 358651
Who is Kaijaje? Swala la sukari kuwa bora ua si bora ni swala FDA iliyo chini ya Wizara ya Afya. Mamlaka ya chakula na dawa ndiyo yenye jukumu la kusimamia ambo ya chakula na dawa. TFDA ndiko waliko wataalam wa kujua sukari ipi inafaa kwa matumizi gani. Aidha Kaijage hajui kazi yake ni ipi anatapatapa
 
KK siyo sukari. It is simply an artificial sweetener.

ARTIFICIAL TABLETOP SWEETENERS
MeTL Group’s own brand artificial sweetener, Kijiko Kimoja (KK), is available in consumer and industrial packs.
MT ulipotelea wapi mkuu?
huku kwetu habari mpya ni ukosefu wa sukari na mafuta ya taa. vipi huko ulikokuwa?
 
Who is Kaijaje? Swala la sukari kuwa bora ua si bora ni swala FDA iliyo chini ya Wizara ya Afya. Mamlaka ya chakula na dawa ndiyo yenye jukumu la kusimamia ambo ya chakula na dawa. TFDA ndiko waliko wataalam wa kujua sukari ipi inafaa kwa matumizi gani. Aidha Kaijage hajui kazi yake ni ipi anatapatapa
hili ni tatizo la serikali nzima kila mtu anafanya kazi ya mwenzie wakati ya kwake haina wa kuifanya
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Viwanda na Biashara ndugu Kaijage,amepiga marufuku mara moja matumizi ya sukari aina ya Kijiko Kimoja (KK) bila ushauri wa daktari.

Sukari hiyo aina ya KK imeamuliwa kurudishwa Dsm toka katika mikoa ya Kigoma,Bukoba na Mwanza ambapo tayari ilishaanza kuuzwa.

Waziri Kaijage anasema sukari hiyo inapaswa kuuzwa kwenye maduka maalumu(Super markets) na Maduka ya dawa Maalumu(Pharmacy) kwa sababu matumizi yake yanahitaji ushauri wa daktari kwa mtumiaji.

Kaijage anasema madhara ya sukari hiyo ni pamoja na kuharibika kwa mimba changa kwa wanawake wajawazito na madhara mengine makubwa ya kiafya.

Sukari hiyo imeamuliwa kutolewa kwenye magodown yote eneo la kanda ya ziwa na mkoa wa Kigoma na kurudishwa Dsm.

Mamlaka husika kama TFDA,TRA,TBS,Wizara ya Afya na mamlaka za Wizara ya Viwanda na Biashara zimeamuliwa kuiondoa sokoni sukari hiyo haraka iwezekanavyo na msambazaji kuacha mara moja kusambaza sukari hiyo kwa wananchi kwani ina madhara makubwa.

Licha ya kuwa Taifa lina uhaba mkubwa wa sukari,lkn serikali haipo tayari kuangamiza afya za watu wake kwa kuruhusu sukari isiyo "rafiki" kwa afya na maisha ya watu.Sukari ya KK inasemwa kuwa na utamu usio wa kawaida,kijiko kimoja tu cha sukari kinaunga kikombe cha ujazo wa lita moja ambayo ni hatari kwa afya.

View attachment 358650 View attachment 358651
Ni nani anaagiza kk sugar ? Hii ni sukari iliyokuwa na kashfa kwa miaka lukuki , kwanini haikuondolewa ? Masikini wa Tanzania watateketea mpaka wakome .
 
Kuwa makini wakati wa kuandika jamani.
Kaijage - Mwijage.
Mkoa wa Bukoba - Mkoa wa Kagera.
Marekebisho hayo ni muhimu.
Asante mkuu Rweye kwa kunisahihisha....Haya majina ya Kaijage na Mwijage hunichanganya sana!!Sisi tuliokuta jina la Ziwa Magharibi huwa tunachanganya sana kati ya Bukoba na Kagera
Ubarikiwe mkuu
 
Who is Kaijaje? Swala la sukari kuwa bora ua si bora ni swala FDA iliyo chini ya Wizara ya Afya. Mamlaka ya chakula na dawa ndiyo yenye jukumu la kusimamia ambo ya chakula na dawa. TFDA ndiko waliko wataalam wa kujua sukari ipi inafaa kwa matumizi gani. Aidha Kaijage hajui kazi yake ni ipi anatapatapa
Ni Mwijage mkuu bantulile
 
Kama ni beki unazuia mpaka unachoka,duh sasa ndo una uchungu na wananchi afya zitaathirika basi tayari washakufa wengi!
 
Hivi nyie watu huwa mnasoma maelezo kweli?
Kwani umesikia hiyo sukari ni feki?
Sukari ya KK ni kwa ajili ya kutengenezea vinywaji na sio kwa matumisi ya mtu wa kawaida.
Ndio maana akasema inatakiwa iuzwe kwa watu wa kawaida ila kwa maelezo kamili toka kwa wataalam jinsi ya kutumia kwa matumizi ya kawaida...
Maana ya kijiko kimoja mnaielewa? We ukitumia sukari hii y pa kawaida unaweza ukaweka zaidi ya kijiko kimoja, ila hii ni kali zaidi jamani, si kwa ajili ya matumizi ya kawaida, bali hutengenezwa kwa madhumuni ya viwanda jamaniiiiiiiii....
Sasa mtu unakurupuka na kusema iliingiaje bila kuthibitisha ubora wake, kuna mwingine hapo juu kasema mbona ina nembo ya TBS... Kuwa na tbs sio tatzo tatzo ni matumizi ni ya wapi na kivip?

Acha kujitoa ufahamu kwa kutetea mambo yaliyo jinai!!! Hata kama maelezo yako yangekuwa sawa bado haiondelei mamlaka husika kupaswa kuwajibika kwa madhara yanayoweza kujitokeza! Ni wajibu waki kuhakiki kila bidhaa inayoingia sokoni ili kulinda afya na usalama wa mlaji! Wangepaswa watoe tahadhari tangu mwanzo kwamba sio kwa matumizi ya kawaida na pia kuhakikisha haisambazwi kiholela isipokuwa maduka maalum na kwa maelekezo maalum! Mtu wa kawaida atajuaje tofauti ya sukari ya kawaida na sukari ya viwandani? Hii ni kishfa, hamna lugha nyingine!!
 
KK siyo sukari. It is simply an artificial sweetener.

ARTIFICIAL TABLETOP SWEETENERS
MeTL Group’s own brand artificial sweetener, Kijiko Kimoja (KK), is available in consumer and industrial packs.

Nikiona watu wanamsifia jamaa huyu huwa nawashangaa sana, Ulaya na Marekani zilipiga marufuku sukari hii kutokana na madhala yake kiafya including kusasabisha cancers!

Cha ajabu kampuni ya MeTL ilitumia kila mbinu kulazimisha kupatiwa vibari vya ku synthesize sukari hii hatarishi, mwanzo TBS ikishirikiana na mtaalamu wa sukari na asali nchini walimkatalia kutengeneza sukari hiyo wakampa na sababu za kisayansi kwa nini sukari hiyo haifai - lakini kwa kuwa ana misuli alipigana juu chini kuhakikisha sukari yake ya KK inapata vibari vya kulazimisha, baada kuhakikisha mtaalamu ambaye alikuwa anatumia uzalendo na taaluma yake kusimamia na kulinda afya za Watanzania wenzake anafanyiwa mizengwe na kuondolewa kazini kwa hila ili asiendelee kuwawekea kiwingu!!!

Hivi sasa ndio naona Serikali ya awamu ya tano ndiyo inashtukia madhala ya KK, kitu ambacho mtaalamu wa sukari na asali nchini alionya kwa muda mrefu akahishia kutimuliwa kazi unceremonousily, kuna umafia wa ajabu sana kwenye Taifa letu.

Siyo kwamba owner wa MeTL hajui madhala ya sukari ya KK , anajua sana lakini kwa kuwa yeye na familia yake hawaitumii hana sababu ya kujali - kwanza familia yake na ndugu zake hawanywi juice na chai ya mahotelini inayo tumia KK kwa wingi sana, pili watoto wao wa shule hawanywi majuice juice kwenye jivichupa vya plastic vilivyo jazwa na viwanda vya uwani/backyard - kutokana na utamu uliyo zidi watoto wa shule wanapenda sana kunywa juice hizo na kuhatarisha maisha yao, thereby wrecking lives of our future generation kwa kujali faida tu sio binadamu.
 
Swali ni kwamba, hiyo sukari iliingiaje sokoni kabla mamlaka husika hazijathibitisha ubora wake? Nani aliidhinisha hilo? Kwa maslahi ya nani? Waliokwisha kutumia wakiweza kuthibitisha madhara waliyopata serikali itawasaidia kulipwa fidia?
Tatizo sio ubora?
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Viwanda na Biashara ndugu Mwijage,amepiga marufuku mara moja matumizi ya sukari aina ya Kijiko Kimoja (KK) bila ushauri wa daktari.

Sukari hiyo aina ya KK imeamuliwa kurudishwa Dsm toka katika mikoa ya Kigoma,Bukoba na Mwanza ambapo tayari ilishaanza kuuzwa.

Waziri Mwijage anasema sukari hiyo inapaswa kuuzwa kwenye maduka maalumu(Super markets) na Maduka ya dawa Maalumu(Pharmacy) kwa sababu matumizi yake yanahitaji ushauri wa daktari kwa mtumiaji.
Mwijage anasema madhara ya sukari hiyo ni pamoja na kuharibika kwa mimba changa kwa wanawake wajawazito na madhara mengine makubwa ya kiafya.

Sukari hiyo imeamuliwa kutolewa kwenye magodown yote eneo la kanda ya ziwa na mkoa wa Kigoma na kurudishwa Dsm.

Mamlaka husika kama TFDA,TRA,TBS,Wizara ya Afya na mamlaka za Wizara ya Viwanda na Biashara zimeamuliwa kuiondoa sokoni sukari hiyo haraka iwezekanavyo na msambazaji kuacha mara moja kusambaza sukari hiyo kwa wananchi kwani ina madhara makubwa.

Licha ya kuwa Taifa lina uhaba mkubwa wa sukari,lkn serikali haipo tayari kuangamiza afya za watu wake kwa kuruhusu sukari isiyo "rafiki" kwa afya na maisha ya watu.Sukari ya KK inasemwa kuwa na utamu usio wa kawaida,kijiko kimoja tu cha sukari kinaunga kikombe cha ujazo wa lita moja ambayo ni hatari kwa afya.

View attachment 358650 View attachment 358651
mmeshatuumiza big time sasa imebaki story tu
 
Nadhani hii sukari imekuwepo sokoni kwa zaidi ya miaka 15!, Taarifa nyepesi kama hii haitoshi kwa wadadisi wa mambo.
 
...hiyo KK inatumiwa sababu ya upungufu wa sukari uliopo nchini,na hiyo KK imeingiaje sokoni bila kuthibitishwa na TBS?!,halafu hii bei ya sukari kuna siku itarudi kama zamani ya kilo tsh1800/?
mbona hii serikali inazidi kufeli kwa kila jambo?
 
Wakati msako wa sukari ulipokuwa umechachamaa walikagua bohari ya MeLTD ambako sukari ilikuwa nyingi sana. Makonda akahoji kwanini anaficha asiisambaze? MeLTD akadai ni kwaajili ya kiwanda cha soda na viwanda vingine. Watu wakapiga kelele sana kuwa serikali iamuru isambazwe watu watumie. Ikaamriwa. Sasa imesambaa wanakuja na matamko kama wameshtuka usingizini
Una uhakika na unachosema au basi tu maka ilivyo "MeLTD" badala ya METL?!

Ninavyojua METL walipeleka ushahidi kama walivyoamriwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Hiyo sukari ilisambaza lini na wapi?
 
Dah..umepita mwezi sasa tangu iingie sokoni.. Nakumbuka wakati inashushwa pale libert mwanza ilikuwa inagombaniwa na nahisi iliuzwa yote..na kiasi kikubwa kitakuwa kimetumika...

Shikamooo serikali ya mwendokasi. Endeleeni kukurupuka ila msiguse afya zetu.
 
Akiongea na Waandishi wa Habari leo mjini Dodoma,Waziri wa Viwanda na Biashara ndugu Mwijage,amepiga marufuku mara moja matumizi ya sukari aina ya Kijiko Kimoja (KK) bila ushauri wa daktari.

Sukari hiyo aina ya KK imeamuliwa kurudishwa Dsm toka katika mikoa ya Kigoma,Bukoba na Mwanza ambapo tayari ilishaanza kuuzwa.

Waziri Mwijage anasema sukari hiyo inapaswa kuuzwa kwenye maduka maalumu(Super markets) na Maduka ya dawa Maalumu(Pharmacy) kwa sababu matumizi yake yanahitaji ushauri wa daktari kwa mtumiaji.
Mwijage anasema madhara ya sukari hiyo ni pamoja na kuharibika kwa mimba changa kwa wanawake wajawazito na madhara mengine makubwa ya kiafya.

Sukari hiyo imeamuliwa kutolewa kwenye magodown yote eneo la kanda ya ziwa na mkoa wa Kigoma na kurudishwa Dsm.

Mamlaka husika kama TFDA,TRA,TBS,Wizara ya Afya na mamlaka za Wizara ya Viwanda na Biashara zimeamuliwa kuiondoa sokoni sukari hiyo haraka iwezekanavyo na msambazaji kuacha mara moja kusambaza sukari hiyo kwa wananchi kwani ina madhara makubwa.

Licha ya kuwa Taifa lina uhaba mkubwa wa sukari,lkn serikali haipo tayari kuangamiza afya za watu wake kwa kuruhusu sukari isiyo "rafiki" kwa afya na maisha ya watu.Sukari ya KK inasemwa kuwa na utamu usio wa kawaida,kijiko kimoja tu cha sukari kinaunga kikombe cha ujazo wa lita moja ambayo ni hatari kwa afya.

View attachment 358650 View attachment 358651
Jamani,sukar hii kumbe ina madhara, mbona inauzwa kwa muda mrefu sana na tena inauzwa kiholela?sasa huko supermarket kuna daktar au mfamasia gani wa kutushauri?Aisee na TFDA wapo tu kumbe sukar inaharibu Mimba imeachwa imesambaa sokoni ni ngumu sana kutoa biadhaa sokoni,ni rahisi kuzuia bidhaa isiingie sokoni
 
Back
Top Bottom