Serikali yapiga marufuku mifuko laini ya plastiki na pombe maarufu ya viroba

Leo akiongea na waandishi wa habari Mh January Makamba amepiga marufuku matumizi ya mifuko laini ya plastic na pombe za kwenye mifuko ya plastic maarufu kama viroba.

Utekelezaji utaanza rasmi January 2017.

Source: Mimi mwenyewe
-------------—

May 26 2016 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba imepiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.

Waziri Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa kwa mzazingira.

Waziri Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’

Tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘

Waziri Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.

pombe Viroba zinachangia sana kwenye uhalifu na kuporomoka maadili ya vijana. Vikifichwa mifukoni ni vigumu kumtambua aliyenavyo. Bora chupa ni ngumu inatambulika kirahisi. Vijana mijini na vijini wameathirika na viroba, mpaka ndoa za watunazo zimeathirika. Wengine wanatengeneza pombe za bandia za viroba kirahisi kuliko za chupa. Mfano ni Moshi na Dodoma
 
Leo akiongea na waandishi wa habari Mh January Makamba amepiga marufuku matumizi ya mifuko laini ya plastic na pombe za kwenye mifuko ya plastic maarufu kama viroba.

Utekelezaji utaanza rasmi January 2017.

Source: Mimi mwenyewe
-------------—

May 26 2016 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba imepiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka 2017 hii pia inahusu matumizi ya mifuko ya plastiki inayofungia pombe maarufu kwa jina la viroba.

Waziri Makamba ameeleza kuwa mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na inasambaa na kuziba mifereji hivyo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa kwa mzazingira.

Waziri Makamba ameongeza kuwa ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya Serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungio mbadala’

Tumetuma wataalamu wa Serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza‘

Waziri Makamba ametoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko ya plastiki waanze kujiandaa sasa kwa zuio hilo.

Jambo zuri lililochelewa
 
Sijui ni kina nani hasa wanatumia hivyo viroba.
cadf2afdbac0dbb1185ea1b2acc0a07c.jpg
 
Kwanini serikali ya CCM huwa inakurupukaga kuvuta mashuka na blanket wakati jogoo ameshawika!
 
Sijaelewa wamepiga marufuku matumizi ya mifuko laini au unywaji wa virobo?
Hizi no zinaitwa egg-chick theory!!!
 
Athari za mtu aliyesoma/ishi nchi zilizostaarabika. Ingekuwa hawa hawa wa humu humu angetoa siku saba tu tena bila ya kutafuta njia mbadala. Unawavunjia watu nyumba hata bila ya kufikiria watoto wataishi wapi; jambo ambalo lingefanywa kistaarabu kabisa kwa kuwapa miezi miwili wahamie kwenye ardhi uliyowatengea. Ingedhuru nini hiyo? Saa nyingine naamini kuwa Waafrika tumepewa akili ndogo sana!
 
Ingekuwa vyema hiyo pombe ingezuiwa kabisa kwa maana wanasiasa wanatumalizia vijana kwa kuwahonga viroba nyakati za uchaguzi.
 
Kumbe Serikali yetu haina dira wala maono ya mbali. Hakika Inaendeshwa kwa kukurupuka. Nimeanza kumuelewa mleta mada mmoja aliyesema hayo maneno katika thread yake leo jii.

Kinacho nisikitisha zaidi ni kuona hawa viongozi wetu wasomi, tena kama huyu February Makatani ambaye ni kijana mdogo kabisa, badala ya kutumia elimu na taaluma yake kufanya mambo ya msingi katika wizara yake, badala yake waingiza siasa katika inshu sentive kama hii ya janga la uchafuzi wa mazingira yatokanayo na matumizi ya mifuko ya plastiki.

Leo amesema hivyo, kesho kutwa sijui atakuja na lipi kuhusu mifuko hiyo ya plastiki ili kupata "Kick" katika media.

BTW, kwa nini serikali inaendelea kulea maradhi haya kwa kujitoa ufahamu tena kwa makusudi kabisa kwa kipindi cha muda mrefu sana tangia awamu ya 3 ya Benjamin ilipotangaza vita dhidi ya matumizi ya mifuko ya plastiki hadi leo hii????.
Ni kwamba swala hili serikali imelishindwa, ila haitaki kusema ukweli??, au kuna conflict of interest hapo???
 
nanyi wachangiaji wa Viroba mnashidwa kujisogeza kwani hata maji zamani yalikua yanauzwa kwenyeBoroba je baada ya kupigwa marufuku maji ya Viroba wakatengeneza Grass na Chupa ndogo kazi inaenda tu na maji yanauzwa tatizo sio Nidhaa ya ndani tatizo kifungashio bidha Runxa...
 
kwahiyo mbadala wake utakuwa ni nini?

Mkuu, mbadala in kuwa na kikapu permanent kwa ajili ya kununulia mahitaji sokoni. Mbona zamani nakumbuka mama yangu alikuwa na kikapu special kwa ajili ya kununulia bidhaa tu! Au ikishindikana tutumie mifuko ya karatasi ambayo unaweza kuichoma moto bila kuharibu mazingira.
 
Nijuavyo kwa Unguja wamefanikiwa kwa sababu wazanzibar tamaduni yao ni kubeba vikapu hata wanaume hubeba waendapo sokoni ila kwa uku bara itakuwa ngumu kwa sababu hadi sasa serikali haijapata mbadala wa hiyo mifuko. Serikali inatakiwa iwe na mbadala kabla ya kupiga marufuku la sivyo yatakuwa yale yale ya sukari

Ahsante kwa mchango wako mkuu, huenda ikawa ni sababu mojawapo. Lakini nawapongeza kwa kuisimamia hiyo sheria, madukani haukuti mifuko ya plastic, ukinunua bidhaa utapatiwa mfuko wa karatasi au ile yenye asili kama kitambaa inayooza upesi. Hata mwananchi hakubali na anaogopa kutumia mfuko wa plastic. Mfano ukiwa unapanda boat kutoka Dar, unanunua mfuko mwingine kwa hadhari ya kuingia nao Unguja.

Nna imani hata bara wakisimamia vizuri, utekelezaji unawezekana.
 
Hakuna sababu za kitumia fedha za walipa kodi kwa kitu kilichowazi. Wakakifunze tu Zenj kama kweli dhamira ya kupiga marufuku ipo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom