Serikali yakiri kuachana na madai ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia

Mtumishiwetu

Senior Member
Jul 13, 2022
187
334
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa ufafanuzi kuhusu wapi zipo shilingi trilioni 360 zilizopo kwenye mashauri ya madai 1,095.

Waziri Nchemba amesema, kuna jumla ya mashauri 400 katika mabaraza ya rufani za kodi (TRAT) yenye thamani ya shilingi trilioni 4.2 na dola za Marekani milioni 3.04 zinaendelea katika mabaraza hayo.

Hata hivyo Dkt. Nchemba amesema, serikali ilikubali kupokea shilingi bilioni 700 kutoka Barrick baada ya makubaliano baina ya timu ya serikali iliyoundwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli kufikia makubaliano ya pande zote na Barrick kuhusiana na madai ya shilingi trilioni 360.

Amesema baada ya makubaliano hayo ndipo ikaundwa kampuni ya Twiga ambayo inamiliki hisa asilimia 16 na Barrick inamiliki asilimia 84 ya kampuni hiyo.

Ufafanuzi huo wa waziri wa Fedha na Mipango unatokana na maswali ya Mbunge wa jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina aliyetaka kufahamu kwa nini serikali imekubali kulipwa shilingi bilioni 700 kutoka kampuni ya Barrick badala ya shilingi trilioni 360 za awali.

Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
 
Magufuli aendelee kuungua moto mkali huko aliko. Hizi takwimu za UWONGO alizopika na Prof Mruma ndizo alizotumia kumjeruhi Tundu Lisu. Magufuli aliwaaminisha watu kuwa tunawadai ACACIA USD 190 billion kutokana na ASSUMPTION kuwa container moja la 20ft la MAKINIKIA lina 7Kg za dhajabu wakati ukweli ni kwamba lina 0.7Kg. Akawapa matumaini hewa Watanzania na kwa jinsi WATANANIA wengi walivyo wajinga wakamuona ni shujaa au mkombozi au MZALENDO.

Hizo Tsh 360 Trillion au USD 190 Billion kwa exchange rate ya wakati ule hazipo popote. Ni UJUHA tu kuamini taarifa kama hizo. Magufuli alikuwa anadanganya mpaka Shetani anaogopa
 
Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
Inaulizwa serikali na siyo Mwigulu! Ye yote aliye ndani ya serikali mwenye dhamana ya fedha anatakiwa kutafuta majibu!
 
Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
Hivi ni nani alikuwa waziri wa fedha enzi zile?

Maji ya kuoshea maiti yanatumika kuhifadhi sangara.

Viongozi ovyo sana. Hivi nyie warundi kwa nini ???!!!!!
 
Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
Wale maprofesa walimwingiza mwendazake cha kike naye akajaa. Eti Trilion 370! Mwisho wa siku wakapewa 700m na kusema ahsante na kufumba mdomo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…