Serikali yaanza maboresho ya Vyoo vya Kituo cha Afya cha Sokoine, Manispaa ya Singida

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,732
13,485
WhatsApp Image 2024-12-06 at 19.50.26_d25aaae9.jpg
Serikali imeamua kufanya maboresho ya vyoo vilivyopo katika Kituo cha Afya cha Sokoine ambacho wenyeji wamezoea kukiita Hospitali ya Sokoine baada ya kuripotiwa kuwa havipo katika mazingira mazuri.

Uamuzi huo unakuja siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kulalamikia kuhusu ubora wa choo hicho. Kuona hoja ya Mdau, soma hapa ~ Hali ya vyoo Hospitali ya Sokoine, Manispaa ya Singida inatisha, viboreshwe

JamiiForums imewasiliana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorian Ludovick kuhusiana na vyoo hivyo, amesema “Mkurugenzi ametoa fedha na shughuli ya ujenzi wa vyoo vipya umeanza leo (Desemba 6, 2024) rasmi. Kwa taarifa zaidi fika kwa Mkurugenzi au Kituo cha Afya Sokoine upate maelezo ya kina."



WhatsApp Image 2024-12-06 at 19.50.26_a6190fba.jpg

WhatsApp Image 2024-12-06 at 19.50.25_73e0d0ea.jpg

WhatsApp Image 2024-12-06 at 19.50.25_1d1dce19.jpg
 
Hivi hichi kituo cha afya ni hospitali ya wilaya au ni kituo tu hakijapandishwa hadhi?
 
Wapitie na haya
 
Hivi hichi kituo cha afya ni hospitali ya wilaya au ni kituo tu hakijapandishwa hadhi?
Ilikuwa hospitali ya wilaya zamani....baada ya kujengwa kwa hospitali ya Rufaa Mandewa, iliyokuwq hospitali ya Mkoa wa Singida ndo ikawa hospitali ya Manispaa na hii ya Sokoine ikawa Kituo cha afya. Ila zamani ilikuwa hospitali kubwa ikitoa huduma zote.
 
Wajenge na vyoo vya walemavu na waandike kabisa choo cha walemavu me na ke kama nilivyoona kuna shule zimepata msaada wa kujengewa vyoo vya namna hiyo
 
Back
Top Bottom