Serikali ya Tanzania sasa itoke hadharani kujibu Tuhuma za Serikali ya Kenya na viongozi wa Muungano wa JUBILEE kuwa Rais Magufuli anamdhamini kifedha Kiongozi wa Upinzani Raila Amolo Odinga kusababisha Maandamano, ghasia na hatimaye kuipindua serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.
Siku Chache Zilizopita Msemaji wa Serikali ya Kenya Erick Kiraithe alisema kuwa tayari kuna taarifa za kijasusi kuwa kuna wanasiasa nchini Kenya wanadhaminiwa na kusaidiwa na Nchi Mbili Jirani maadui wa Kenya kutaka kuvuruga amani na kuiangusha Serikali na kudai kuwa Baraza la Ushauri la Usalama (National Security Advisory Council) lilikutana siku ya Jumatatu kuangalia namna ya kuwashughulikia watu hao
Mbunge wa Jimbo la Starehe Mwenye ushawishi ndani ya Serikali ya JUBILEE akiambatana na wabunge wengine alifanya mkutano na waandishi wa Habari Nairobi Hoteli na Kuwataja marais John Magufuli wa Tanzania na Salva Kiir wa Sudan ya Kusini
Rais Magufuli akiwa mapumzikoni CHATO msimu wa Sikukuu ya Pasaka alikua Mwenyeji wa Raila Odinga anayejiandaa na Uchaguzi nchini Kenya mwaka 2017
Pia Mwezi Desemba nilialikwa na Mwenyekiti wa Vijana wa ODM wakati huo Rashid Mohammed n kwenye mkutano mkuu wa chama cha ODM kumteua Mgombea Urais 2012 nchini Kenya.Mhe.Magufuli pia alikuwepo. Nilimshuhudia Mhe.Magufuli akiwa waziri wakati huo akidai amehudhuria mkutano ule na kutangaza kuwa Raila Odinga ni Rafiki yake na amekuja kumuunga Mkono.Aliendelea kushtua watu Ukumbini akidai kwamba wagombea wengine wanaotarajia kuchuana na Raila Odinga hawawezi kusafiri hata nje ya nchi.Kipindi Hicho Uhuru Kenyatta na Willium Ruto walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mahakama ya kimataifa ya ICC.
Mhe.Magufuli akaendelea kusema hata Odinga angegombea jimbo la Chato yeye Magufuli asingethubutu kugombea maana asingeweza kumshinda
Urafiki binafsi wa Raila Odinga na Rais Magufuli sio tatizo jwani hata Mwalimu Nyerere alikua na urafiki na akina Thom Mboya,Jaramogi Oginga Odinga ila tatizo ni pale ambapo Mhe.Magufuli anaposhindwa kuwa senstive kisiasa na Kidiplomasia.Mbaya zaidi tuhuma zinatolewa na serikali ya nchi jirani tena mwanachama ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa Rais Magufuli anatumia Raslimali za nchi kumfadhili Mpinzani wa nchi jirani kwa lengo la kupindua serikali kwa sababu ya urafiki wao tu
Nikumbushie tu kitendo alichofanya Mhe.Magufuli kipindi kile nilisema na niliandika kuwa kitakuja kuleta matatizo ya kidiplomasia siku za usoni ikiwa ODM wangeshindwa kwani tayari kupitia Udhaifu alioonyesha waziri wa serikali ya Tanzania Mhe.Magufuli wakati Ule walishaaminisha Umma kuwa serikali ya Tanzania inawaunga Mkono.Kosa hili la Kidiplomasia ameendelea kulirudia.
Rais Jakaya Kikwete alikuwa Rafiki wa Kalonzo Musyoka lakini Uhusiano wao haujawahi kuibua mgogoro wa kidiplomasia na au kutoaminiana baina ya serikali hizi mbili
Tuhuma hizi ni nzito na zinazochochea mgawanyiko ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kitendo cha Serikali ya Tanzania kukaa kimya hadi muda huu maana yake kinatoa Silent Consent kuwa nu kweli hasa msemaji wa Serikali anaposema kwa ujasiri kuwa serikali yao ina taarifa rasmi
Mwaka 2013 kulikua na mgogoro wa kidiplomasia uliotishia kuipasua Jumuiya ya Afrika Mashariki .Kenya,Uganda na Rwanda ziliunda Muungano wao wa hiyari (Coalition of The Willing-CoW).Jitihada kubwa za kidiplomasia zilifanyika
Sasa muda huu Rais Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Africa Mashariki na Tanzania kama Mwenyekiti hatupaswi kuwa chanzo cha migogoro ndani ya jumuiya kwani sisi ndio tunaopaswa kuonyesha uongozi katika Diplomasia kuhakikisha Malengo ya Mtangamano(Intergration) yanafikiwa.
Jitihada zozote za Serikali ya Tanzania na wapambe wake kutumia propaganda pengine kwa kuibua hoja ya Bomba la mafuta Kutoka Uganda na Kupita Tanzania badala ya Kenya na Suala la Reli ya Rwanda kwamba ndio limesababisha wivu itakua ni uamuzi mbaya kidiplomasia
Serikali ya Tanzania ijibu tuhuma hizi kama si kweli basi Serikali ya Kenya iombe Radhi
Kenya na Tanzania zinahitajiana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote kiuchumi
Katika tathmini iliyotolewa bungeni jana,biashara ya Kenya na Tanzania imechangia sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi hizi
Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao ni wanadiplomasia Maahiri Dr.Augustine Mahiga wa Tanzania na Amina Mohammed Jibril wa Kenya wasaidie kunusuru hali hii ambayo inahatarisha Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Nchi hizi Mbili
Na Pia Rais Magufuli asaidiwe ili apate uzoefu wa Kidiplomasia katika maneno na matendo yake.
Kwa mfano kitendo cha kuongea na Rais Kenyatta mwezi March walipokutana Arusha na kuahidi kusaidiana kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya nchi hizi mbili na kisha mwezi mmoja baadae kumwalika Raila Odinga akiwa Mapumzikoni(Inaweza kutafsiriwa alichukua likizo ili akutane na Odinga isionekane amekutana nae ikulu) hakikutoa gesture nzuri kidiplomasia
Wakati Rais Magufuli anahutubia mkutano wa mfuko wa Wafanyabiashara Mwezi Desemba 2015 aliitaja kampuni ya Broakside Dairy Limited kuwa ilikua ikifanya biashara kiadui na kinyume na misingi ya Biashara nchini.Kampuni hiyo ilimilikiwa na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.Kidiplomasia Rais hakupaswa kutamka na kuitaja kamapuni ile bali angeweza kukwepa na kutumia namna nyingine au mtu mwingine kama ilikua ni lazima itamkwe.Siitetei kampuni ile isipokua ni udhaifu mkubwa wa kidiplomasia aliouonyesha Rais ingawa anaweza kujitetea kuwa alikua anasimamia Sheria.Diplomasia ni namna ya kumwambia mtu kafie mbali na yeye akakuuliza mbali kiasi gani badala ya kukukasirikia.Rais anapaswa ajifunze hili
Sasa hizi tuhuma za serikali ya Kenya na viongozi waandamizi zijibiwe na kama si kweli serikali ya Kenya Iombe Radhi.
Kama ni kweli inawezenaje Wanachi wa Tanzania wakose Sukari halafu Rais afadhali shughuli kama hizo nchi jirani?Na iweje sasa Serikali yake izuie mikutano ya kisiasa nchini?
Aluta Continua,Victory Ascerta......
Ben Saanane
Unanikumbusha kisa kimoja husimuliwa mtaani. Kuwa kunakibaka mmoja alienda kuiba kwenye nyumba ya wahuni bahati mbaya kwake na nzuri kwa wahuni yule mwizi alikamatwa. Wahuni wakamalizana naye walivyoona inafaa na kumuachia.Serikali ya Tanzania sasa itoke hadharani kujibu Tuhuma za Serikali ya Kenya na viongozi wa Muungano wa JUBILEE kuwa Rais Magufuli anamdhamini kifedha Kiongozi wa Upinzani Raila Amolo Odinga kusababisha Maandamano, ghasia na hatimaye kuipindua serikali ya Rais Uhuru Kenyatta.

Chadema itafaidika aje na uhusiano mbaya kati ya Uhuru na JPM. Inaonekana kuna kitu nyuma pazia qmabacho mnategemea kufaidika Na nacho.Tuhuma za Serikali ya Kenya na Wabunge wa JUBILEE zijibiwe. Kama huelewi madhara ya tuhuma hizi bora unyamaze maana haya tunayojadili yapo juu ya uwezo wako wa kufikiri.
Saanane unasahau upesi.CHADEMA ndio wanatakiwa KUJIBU tuhuma
Soma hii habari ambayo iko kwenye blog ya CHADEMA kuhusiana na uchaguzi uliopita wa Kenya
Chadema yambeba Odinga
WAKATI wananchi wa Kenya leo wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeonekana kumbeba mgombea urais kupitia Chama cha ODM ambacho kimo ndani ya Muungano wa CORD, Raila Odinga, kwa kupeleka magari na timu ya wasanii kumsaidia wakati wote wa kampeni zake.
CHADEMA ambao wanadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Odinga, kilituma magari mawili aina ya Fuso kwa ajili ya kumpigia kampeni ambazo zimedumu kwa mwezi mmoja. Mbali ya kutuma magari hayo, CHADEMA walituma kikundi cha wasanii kikiongozwa na mwimbaji maarufu wa chama hicho, Fulgance Mapunda 'Mwanakotide’.
Mbali ya chama hicho, Watanzania wengi ambao wanadaiwa kumuunga mkono Odinga na wamekuwa wakitajwa mara kwa mara ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na Rostam Aziz. Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa CHADEMA, Boniphace Makene alikiri chama chake kupeleka magari hayo na wasanii kwa ajili ya kumsaidia Odinga na timu yake kuendesha kampeni zake kwa ufanisi.
“Ni kweli kwa kipindi cha miezi mitatu sasa, timu ya CHADEMA imekuwa ikizunguka katika miji mbalimbali nchini Kenya, kwa ajili ya kumsaidia mgombea wa Muungano wa CORD kupiga kampeni, kumekuwa na mafanikio makubwa mno.
“Tuliruhusu magari yetu mawili aina ya fuso, ambayo yalikuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya muziki na wasanii wawili, Mwanakotide na Pepe ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa, tunaamini mchango umeonekana,” alisema Makene.
Alisema magari hayo, yalitumiwa na Odinga katika mikutano yote ya kampeni, ambazo zilihitimishwa juzi katika Uwanja wa Nyayo mjini Nairobi.
“Kama ulifanikiwa kuangalia televisheni, juzi kwenye Uwanja wa Nyayo, magari yale yalikuwa kivutio kikubwa sana, yalikuwa yamepambwa picha nyingi za Odinga na Kalonzo Musyoka, ambaye ni mgombea mwenza wake,” alisema Makene.
Kwa upande wake, Mwanakotide alipoulizwa alisema wamekuwa Kenya kwa kipindi cha miezi mitatu kusaidia ODM, kutokana na kuwa na uhusiano mzuri na chama chao.
“Tumekuwa na mafanikio makubwa, kazi yetu ilikuwa kuhubiri amani na kuwataka Wakenya kuachana na mambo ya ukabila na chuki, tunaamini wametuelewa…unajua wale ni jamaa zetu, lazima tuwasaidie,” alisema Mwanakotide.
UCHAGUZI LEO
Homa ya uchaguzi imepanda kwa kila mwananchi wa Kenya, huku macho na masikio yakielekezwa zaidi kwa wagombea wawili wa urais, Raila Odinga wa Muungano wa CORD na Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee. Katika uchaguzi huo, kuna wagombea wengine na vyama vyao kwenye mabano ni Musalia Mudavadi (Amani), Martha Karua (NARC Kenya), Peter Keneth (KNC), Profesa Ole Kiapi, Paul Muite, Mohamed Abdalaah Dida.
Hata hivyo, Odinga na Kenyatta ndio wanaopewa nafasi kubwa kwa mmojawapo kuibuka na ushindi na hivyo kutegua kitendawili cha kampeni za aina yake, zilizodumu kwa mwezi mmoja. Katika viunga vya Jiji la Nairobi ambapo MTANZANIA limepiga kambi, kuna kila aina ya shamrashamra na majigambo ya hapa na pale kutoka kwa wapenzi wa wagombea hao wawili kila mmoja akitamba kuibuka na ushindi.
Jiji hilo, ambalo mara nyingi huwa ni safi, safari hii limechafuka kutokana na mabango ya wagombea ambayo yametanda kila kona.
Ufungaji kampeni
Raila Odinga na mgombea mwenza wake, Kalonzyo Musyoka walikuwa Uwanja wa Nyayo, wakati wenzao wa Muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta na William Rutto, walikuwa kwenye viwanja vya Uhuru Park, umbali wa kilometa 20 hivi. Katika mikutano yote miwili kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Hata hivyo, katika mkutano wa Kenyatta, kulikuwa na fujo za hapa na pale, zilizosababishwa na vijana walioonekana wamelewa pombe na kutishia kutaka kukaba watu, ambapo ililazimika polisi watumie nguvu za ziada kukabiliana nao.
Ujumbe wa wagombea wote, ulikuwa ni amani kutumia vyombo vya mahakama kama wakidhulumiwa. Kwa upande wake, Odinga alisema yuko tayari kupokea matokeo yoyote halali, lakini kama akidhulumiwa atatumia mahakama kudai haki yake. Aliwasihi mashabiki wake, kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani. Kwa upande wake, Kenyatta, aliutumia muda mwingi kujibu tuhuma ambazo amerushiwa na wapinzani wake kuwa amejimilikisha ardhi kubwa kupita kiasi. Alisema yuko tayari kuunda Serikali na kuwataka Wakenya wajitokeze kwa wingi, ili waweze kuwachagua.
Kalonzyo Musyoka, alitumia maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyewahi kusema kuwa ‘itaichukua miaka 1,000 dunia kumpata mtu kama Mahattma Gandhi (India) na itawachukua miaka 100 Wakenya kumpata kiongozi aina ya Odinga. Mgombea mwingine ambaye ana umuhimu wake katika uchaguzi huo, ni Musalia Mudavadi wa Chama cha UDF, ambao ni (Muungano wa Amani), yeye ndiye mwenye kura ya turufu kama uchaguzi utarudiwa.
Kampeni zake kubwa amezifanyia huko Magharibi mwa Kenya karibu na Uganda, ambako aliwasihi Wakenya wamchague yeye kuwa rais wao, hata hivyo aliwahi kuwa mshirika wa karibu wa Odinga wakati wa ODM.
Katika uchaguzi huu, awali alisaini mkataba wa ushirikiano na Kenyatta, kwamba yeye ndiye angekuwa mgombea urais kupitia Jubilee, lakini siku chache baadaye Uhuru alimgeuka na kusema kulikuwa na ushawishi wa kishetani.
Mudavadi kuona hivyo, aliamua kusimama mwenyewe. Hata hivyo, kiongozi huyo anaelezwa kuwa anaungwa na Rais Mstaafu wa nchi hiyo, Daniel arap Moi. Ikumbukwe kuwa mwaka 2002, Moi alimsimika Uhuru kuwa mgombea Urais kupitia KANU, wakati huo Mudavadi alikuwa Makamu wa Rais wa Moi ambaye alishindwa vibaya na Mwai Kibaki ambaye wakati huo alikuwa bega kwa bega na Odinga.
Swali la kujiuliza hapa ni je ikitokea kura zikarudiwa, Mudavadi atamuunga mkono nani kati ya Kenyatta na Odinga?
Habari zilizopatikana jijini Nairobi, zinasema Mzee Moi ameamua kumtosa Uhuru kwa sababu yeye amekitosa chama chake cha KANU, ambacho hakina nguvu kabisa katika uchaguzi huo. KANU imejiunga na Muungano wa Amani.
SUALA LA UKABILA
Kama ilivyo ada kwa Wakenya, suala la ukabila lipo juu kwenye kampeni za mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka 2007, wakati huo mchuano ulipokuwa kati ya Rais Mwai Kibaki na Raila Odinga, ukabila huo pia ulisababisha kutokea machafuko.
Gharama za uchaguzi
Gharama zote za kampeni kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inakadiriwa kuwa Sh bilioni 24, lakini inakadiriwa mgombea wa Jubilee (Kenyatta), ametumia Sh bilioni 30 hadi 50 (sawa na zaidi ya trilioni 6 za Tanzania).
Katika kampeni hizo, Kenyatta alitumia jumla ya helkopta 10 na Odinga anakadiriwa kutumia Sh bilioni 10 mpaka 20 za Kenya.
MAANDALIZI
Maandalizi ya aina yake yamefanyika ambapo, sehemu ya kujumlishia matokeo ya kura za kitaifa, (National tallying Centre), imeandaliwa vizuri, kuna sehemu maalum kwa ajili ya vyombo vyote vya habari. Vifaa vya kisasa vimesheheni katika eneo hilo ili kuwezesha upatikanaji wa matokea kwa uwazi na urais zaidi.
Vyombo vya usalama viko tayari, kila mahali kuna ulinzi wa kutosha ikiwa ni pamoja na sehemu zote zenye mjumuiko wa watu wengi.
Jaji Mkuu wa Kenya, Dk. Willy Mtunga, alisema mahakama itakuwa tayari wakati wowote itakapohitajika hata kama kesi itatokea usiku.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya, Isaack Hassan alisema, tume yake ipo tayari kuendesha uchaguzi huo hata kama kutatokea uchaguzi wa marudio kwa wagombea kutokufikisha asilimia 51 inayotajwa na Katiba. Watu waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 14.3, kuna majimbo 290, kata 1,450 na vituo vya kupigia kura 33,000 na Kaunti 47.
SOURCE:Chadema Blog: Chadema yambeba Odinga
Hivi nyie kumbukumbu mnapeleka wapi si nyie na chama chenu ndio mlienda kumpiga taff Odinga leo mnataka kutafuta watu wa kuangushia jumba bovu. Maandamano kenya ni katiba yao ndio imetoa idhini na wamepitisha kwa hiyari yao hata Uhuru anajua kabisa sasa JPM kwa siasa za Kenya mnataka kumng'arishia nyota yeke. Mlianza na MCC, LUGUMI, SUKARI, TULIA na Sasa mnampeleka kimataifa atawanyosha tu!
Uzoefu wa kidiplomasia JPM amepewa kazi ya kujenga nchi yake kwanza huko nje watakuja wenyewe. Jifunzeni kukaa kimya na muda huu someni budget sio mnamwachia kiongozi wenu aje kutoa matamko.
Maana anaweza akawaita vilazaMkuu, ili uhusiano wetu uwe salama, ni afadhali rais asijibu.
Ben Saanane umekuwaje siku hizi? mara msemaji wa ACT,Mara CHADEMA na sasa CCM, naKufananisha na mtu anayeoga bafuni mara anapita kichaa anakwapua nguo zake na kuanza kukimbia nazo,nawe bila kufikiri unatoka uchi na kuanza kumkimbiza kicha ili upate nguo zako,nani kichaa hapo?
Baada ufikirishe Ubungo unapanua miguu daahTeh Teh hebu twambie unataka wajibu nini? Wewe unaonaje? Halafu twambie hayo malalamiko yametolewa wapi na kwanjia gani?
Hakuna mwenye muda wa kujibu maswala ya vijiwe vya kahawa!
Endelea kuamisha magoli!
hembu kaa ufikirie mkuu huyo slava kiir nchini mwake ana matatizo hata bado hajayamaliza na anategemea msaada wa kuyamaliza kutoka kenya nchi iliyo karibu sana naye,leo hii aende kuifadhili ili kuingia kwenye machafuko ili iweje??Msemaji wa Serikali ya Kenya amesema anafadhiliwa na nchi mbili jirani ambazo ni maadui wakenya.Wabunge wa JUBILEE wakiongozwa na Maina Kamanda wakaitisha Press Conference Nairobi Hoteli wakamtaja Magufuli na Salva Kiir.
Fanya research kabla hujakimbilia kutoa comments
Safi sana. Bora umetuwekea hii habariSaanane unasahau upesi.CHADEMA ndio wanatakiwa KUJIBU tuhuma
Soma hii habari ambayo iko kwenye blog ya CHADEMA kuhusiana na uchaguzi uliopita wa Kenya
Chadema yambeba Odinga
WAKATI wananchi wa Kenya leo wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeonekana kumbeba mgombea urais kupitia Chama cha ODM ambacho kimo ndani ya Muungano wa CORD, Raila Odinga, kwa kupeleka magari na timu ya wasanii kumsaidia wakati wote wa kampeni zake.
CHADEMA ambao wanadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Odinga, kilituma magari mawili aina ya Fuso kwa ajili ya kumpigia kampeni ambazo zimedumu kwa mwezi mmoja. Mbali ya kutuma magari hayo, CHADEMA walituma kikundi cha wasanii kikiongozwa na mwimbaji maarufu wa chama hicho, Fulgance Mapunda 'Mwanakotide’.
Mbali ya chama hicho, Watanzania wengi ambao wanadaiwa kumuunga mkono Odinga na wamekuwa wakitajwa mara kwa mara ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na Rostam Aziz. Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa CHADEMA, Boniphace Makene alikiri chama chake kupeleka magari hayo na wasanii kwa ajili ya kumsaidia Odinga na timu yake kuendesha kampeni zake kwa ufanisi.
“Ni kweli kwa kipindi cha miezi mitatu sasa, timu ya CHADEMA imekuwa ikizunguka katika miji mbalimbali nchini Kenya, kwa ajili ya kumsaidia mgombea wa Muungano wa CORD kupiga kampeni, kumekuwa na mafanikio makubwa mno.
“Tuliruhusu magari yetu mawili aina ya fuso, ambayo yalikuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya muziki na wasanii wawili, Mwanakotide na Pepe ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa, tunaamini mchango umeonekana,” alisema Makene.
Alisema magari hayo, yalitumiwa na Odinga katika mikutano yote ya kampeni, ambazo zilihitimishwa juzi katika Uwanja wa Nyayo mjini Nairobi.
“Kama ulifanikiwa kuangalia televisheni, juzi kwenye Uwanja wa Nyayo, magari yale yalikuwa kivutio kikubwa sana, yalikuwa yamepambwa picha nyingi za Odinga na Kalonzo Musyoka, ambaye ni mgombea mwenza wake,” alisema Makene.
Kwa upande wake, Mwanakotide alipoulizwa alisema wamekuwa Kenya kwa kipindi cha miezi mitatu kusaidia ODM, kutokana na kuwa na uhusiano mzuri na chama chao.
“Tumekuwa na mafanikio makubwa, kazi yetu ilikuwa kuhubiri amani na kuwataka Wakenya kuachana na mambo ya ukabila na chuki, tunaamini wametuelewa…unajua wale ni jamaa zetu, lazima tuwasaidie,” alisema Mwanakotide.
UCHAGUZI LEO
Homa ya uchaguzi imepanda kwa kila mwananchi wa Kenya, huku macho na masikio yakielekezwa zaidi kwa wagombea wawili wa urais, Raila Odinga wa Muungano wa CORD na Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee. Katika uchaguzi huo, kuna wagombea wengine na vyama vyao kwenye mabano ni Musalia Mudavadi (Amani), Martha Karua (NARC Kenya), Peter Keneth (KNC), Profesa Ole Kiapi, Paul Muite, Mohamed Abdalaah Dida.
Hata hivyo, Odinga na Kenyatta ndio wanaopewa nafasi kubwa kwa mmojawapo kuibuka na ushindi na hivyo kutegua kitendawili cha kampeni za aina yake, zilizodumu kwa mwezi mmoja. Katika viunga vya Jiji la Nairobi ambapo MTANZANIA limepiga kambi, kuna kila aina ya shamrashamra na majigambo ya hapa na pale kutoka kwa wapenzi wa wagombea hao wawili kila mmoja akitamba kuibuka na ushindi.
Jiji hilo, ambalo mara nyingi huwa ni safi, safari hii limechafuka kutokana na mabango ya wagombea ambayo yametanda kila kona.
Ufungaji kampeni
Raila Odinga na mgombea mwenza wake, Kalonzyo Musyoka walikuwa Uwanja wa Nyayo, wakati wenzao wa Muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta na William Rutto, walikuwa kwenye viwanja vya Uhuru Park, umbali wa kilometa 20 hivi. Katika mikutano yote miwili kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Hata hivyo, katika mkutano wa Kenyatta, kulikuwa na fujo za hapa na pale, zilizosababishwa na vijana walioonekana wamelewa pombe na kutishia kutaka kukaba watu, ambapo ililazimika polisi watumie nguvu za ziada kukabiliana nao.
Ujumbe wa wagombea wote, ulikuwa ni amani kutumia vyombo vya mahakama kama wakidhulumiwa. Kwa upande wake, Odinga alisema yuko tayari kupokea matokeo yoyote halali, lakini kama akidhulumiwa atatumia mahakama kudai haki yake. Aliwasihi mashabiki wake, kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani. Kwa upande wake, Kenyatta, aliutumia muda mwingi kujibu tuhuma ambazo amerushiwa na wapinzani wake kuwa amejimilikisha ardhi kubwa kupita kiasi. Alisema yuko tayari kuunda Serikali na kuwataka Wakenya wajitokeze kwa wingi, ili waweze kuwachagua.
Kalonzyo Musyoka, alitumia maneno ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyewahi kusema kuwa ‘itaichukua miaka 1,000 dunia kumpata mtu kama Mahattma Gandhi (India) na itawachukua miaka 100 Wakenya kumpata kiongozi aina ya Odinga. Mgombea mwingine ambaye ana umuhimu wake katika uchaguzi huo, ni Musalia Mudavadi wa Chama cha UDF, ambao ni (Muungano wa Amani), yeye ndiye mwenye kura ya turufu kama uchaguzi utarudiwa.
Kampeni zake kubwa amezifanyia huko Magharibi mwa Kenya karibu na Uganda, ambako aliwasihi Wakenya wamchague yeye kuwa rais wao, hata hivyo aliwahi kuwa mshirika wa karibu wa Odinga wakati wa ODM.
Katika uchaguzi huu, awali alisaini mkataba wa ushirikiano na Kenyatta, kwamba yeye ndiye angekuwa mgombea urais kupitia Jubilee, lakini siku chache baadaye Uhuru alimgeuka na kusema kulikuwa na ushawishi wa kishetani.
Mudavadi kuona hivyo, aliamua kusimama mwenyewe. Hata hivyo, kiongozi huyo anaelezwa kuwa anaungwa na Rais Mstaafu wa nchi hiyo, Daniel arap Moi. Ikumbukwe kuwa mwaka 2002, Moi alimsimika Uhuru kuwa mgombea Urais kupitia KANU, wakati huo Mudavadi alikuwa Makamu wa Rais wa Moi ambaye alishindwa vibaya na Mwai Kibaki ambaye wakati huo alikuwa bega kwa bega na Odinga.
Swali la kujiuliza hapa ni je ikitokea kura zikarudiwa, Mudavadi atamuunga mkono nani kati ya Kenyatta na Odinga?
Habari zilizopatikana jijini Nairobi, zinasema Mzee Moi ameamua kumtosa Uhuru kwa sababu yeye amekitosa chama chake cha KANU, ambacho hakina nguvu kabisa katika uchaguzi huo. KANU imejiunga na Muungano wa Amani.
SUALA LA UKABILA
Kama ilivyo ada kwa Wakenya, suala la ukabila lipo juu kwenye kampeni za mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka 2007, wakati huo mchuano ulipokuwa kati ya Rais Mwai Kibaki na Raila Odinga, ukabila huo pia ulisababisha kutokea machafuko.
Gharama za uchaguzi
Gharama zote za kampeni kupitia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, inakadiriwa kuwa Sh bilioni 24, lakini inakadiriwa mgombea wa Jubilee (Kenyatta), ametumia Sh bilioni 30 hadi 50 (sawa na zaidi ya trilioni 6 za Tanzania).
Katika kampeni hizo, Kenyatta alitumia jumla ya helkopta 10 na Odinga anakadiriwa kutumia Sh bilioni 10 mpaka 20 za Kenya.
MAANDALIZI
Maandalizi ya aina yake yamefanyika ambapo, sehemu ya kujumlishia matokeo ya kura za kitaifa, (National tallying Centre), imeandaliwa vizuri, kuna sehemu maalum kwa ajili ya vyombo vyote vya habari. Vifaa vya kisasa vimesheheni katika eneo hilo ili kuwezesha upatikanaji wa matokea kwa uwazi na urais zaidi.
Vyombo vya usalama viko tayari, kila mahali kuna ulinzi wa kutosha ikiwa ni pamoja na sehemu zote zenye mjumuiko wa watu wengi.
Jaji Mkuu wa Kenya, Dk. Willy Mtunga, alisema mahakama itakuwa tayari wakati wowote itakapohitajika hata kama kesi itatokea usiku.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya, Isaack Hassan alisema, tume yake ipo tayari kuendesha uchaguzi huo hata kama kutatokea uchaguzi wa marudio kwa wagombea kutokufikisha asilimia 51 inayotajwa na Katiba. Watu waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 14.3, kuna majimbo 290, kata 1,450 na vituo vya kupigia kura 33,000 na Kaunti 47.
SOURCE:Chadema Blog: Chadema yambeba Odinga
mkuu ben msemaji wa serikali anaitwa bwn.kiraithe sasa naomba unijibu huyo msemaji wa serikali aliyesema hivyo anaitwa nani??ana cheo cha msemaji wa serikali,aliteuliwa na nani??Msemaji wa Serikali ya Kenya amesema anafadhiliwa na nchi mbili jirani ambazo ni maadui wakenya.Wabunge wa JUBILEE wakiongozwa na Maina Kamanda wakaitisha Press Conference Nairobi Hoteli wakamtaja Magufuli na Salva Kiir.
Fanya research kabla hujakimbilia kutoa comments
Tuhuma za Serikali ya Kenya na Wabunge wa JUBILEE zijibiwe. Kama huelewi madhara ya tuhuma hizi bora unyamaze maana haya tunayojadili yapo juu ya uwezo wako wa kufikiri.