LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 15,803
- 23,064
JPM uliposema utaziba mianya ya wala rushwa na wapiga dili kura ulizipata za kutosha.Haya sasa wapiga dili ndiyo hao wameinuka!Ndugu Wananchi napenda kuwajulisha kuwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na DR Magufuli, Rais Mchapa kazi asiyependa figisufigisu, ipo imara zaidi kuliko unavyofikiria
Serikali Ya JPM haitishwi na wala haitakwamisha na kikundi kidogo cha watanzania ambao wanataka kuchafua hali ya hewa nchini kwa kuwatishia wananchi kwamba Serikali inatenda maovu kwa wananchi wake.
Serikali ya JPM haimuonei na wala haitamuonea mtu yeyote awe Mtanzania au sio Mtanzania hao wanaopiga kelele kuwa Serikali kupitia TISS inateka nakuwaonea wananchi wake hao ni wapiga dili na mawakala wa mafisadi ambao mianya yao ya RUshwa na ufisadi imezibwa na JPM.
Hao wabunge wanaotaka kuleta uchochezi bungeni ni mawakala wa mafisadi na wapiga dili ambao maswahiba wao dili zao za kukwepa kodi na kuuza madawa ya kulevya zimedhibitiwa ipasavyo.
CHini ya DR Magufuli nidhamu ya nchi lazima irejee na sasa naona nidhamu inarejea kuanzia kwa mawaziri hadi wabunge.
kama kuna Mbunge wa CCM haridhishwi na Uchapakazi na maamuzi ya Rais DR Magufuli aondoke haraka kwani kelele zake hazibadili msimamo wa Serikali wa kuifanya Tanzania Mpya yenye uchumi wa kati.
Wabunge wanapiga kelele, mitandao inapiga kelele lakini sisi tunaendelea kuwaletea maendeleo na kesho tunazindua ujenzi wa reli ya Kisasa na baada ya wiki moja tutawaambia Watanzania wake mkao wa kufaidi madini yao kwani kuna Matrilioni ya fedha yanaenda kupatikana kutokana na mchanga wa madini uliokuwa unatoroshwa.
Hata msiposhukuru maendeleo tutawaletea tu na mafisadi na wakwepa kodi awe waziri, mbunge au mwananchi wa kawaida atashughulikiwa tu.
Tanzania ya Viwanda kwanza Blablaaaaaa badae JPM piga kazi hata tubaki wawili tunaokushabikia kwasasa lakini ipo siku watakukumbuka.