Wambandwa
JF-Expert Member
- Dec 3, 2006
- 2,249
- 832
Binafsi sikumpa kura yangu, na wengi hawakumpa pia na yeye anajua. hata wewe TataMadiba unajua hilo.
Sikia wewe, kabla ya maamuzi ya kukurupuka sukari Ilikuwa ikiuzwa 2000@kg,Ndiyo maana hao wananchi wanasema tatizo la sukari litaisha mwaka moya Wa fedha ukianza, wanajua kwa sasa lipo au haujasoma mada yote?
Eti raia aliyepigika anaongea hivyo! Ndoto zingine ni shida tu!!Haya matatizo ya ukosefu wa
sukari, tusubiri tu mwaka mpya wa
fedha unaonza tarehe moja Julai
ambapo kila wizara itapewa fungu
lake, litaisha tu. Magufuli ana jeuri
sana ana uhakika pesa
ameshakusanya ya kutosha na ndiyo
maana hata hawa Wazungu
wakimletea za kuleta anawapotezea.
Nimecheka sana kweli villaza mpo.
Kama kujitoa ufahamu ni kuwa kinyume na wewe, uko sahihi, la sivyo unazi wa vyama unakutafuna ila ukweli ndiyo huo.Sijui hata chekechea ulimaliza kwa unavyojitoa ufaham?
Kwa anayejua maana ya Research, hapana shaka haka sample ya watu wawili inatosha kuakisi ukweli wa unachokifanyia utafiti.Utafiti wako umeufanya katika mitaa mingapi?
shame on you.. hayo maoni ni ya watu au ya kwako? hv huna taarifa kuwa ndani ya chama chako mabosi zako hawamtaki achukue kijiti? usirudie tena kuandika uzi kama magazeti ya shigongo au kama G.mlingaBaada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika mwaka jana na Dr. John Pombe Magufuli kuchsguliwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanazuoni na mwanachama wa ACT-Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo alinukuliwa akisema na hapa nanukuu "WAPINZANI TUKITAFUTA UMAARUFU KWA KUTEGEMEA MAKOSA YANAYOFANYWA NA SERIKAI YA CCM, KIPINDI CHA JPM TUNAWEZA KUWA NA WAKATI MGUMU" mwisho wa kunukuu.
Hakika nimeanza kuona ukweli wa maneno haya ya Prof. Kitila Mkumbo. Leo nikiwa ndani ya magari yetu ya kusafiria maarufu kama DALADALA nikitokea Mbagala Kwenda Kariakoo, kwa muda wote abiria walikuwa wakitoa maoni yao juu ya Serikali ya Magufuli na siasa zinazofanywa na vyama vya upinzani na hasa CHADEMA kwa mgongo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA).
Ninukuu tu baadhi ya yale yaliyowagusa wananchi hao:
1. Wapo wanaosema hawanielewi, nami nasema watanielewa tu-wananchi hao wakinukuu maneno ya Mh. Rais akiwa kwenye mikusanyiko mbalimbali.
2. Siku hizi bwana hakuna cha mtu kukamatwa na akasema "Unajua mimi ni nani". Wananchi wanakiri kuwa hakuna aliye juu ya sheria na hasa jeshi la polisi linapotekeleza majukumu yake.
3. Wanachokifanya CHADEMA, kugomea vikao vya bunge, kulishtaki jeshi la polisi na kudai maandamano kwa nguvu ni kutaka tu nao waonekane bado wana nguvu na kutaka kupunguza nguvu ya Magufuli maana kero zote walizozipigia kelele ndizo anapambana nazo.
4. Haya matatizo ya ukosefu wa sukari, tusubiri tu mwaka mpya wa fedha unaonza tarehe moja Julai ambapo kila wizara itapewa fungu lake, litaisha tu. Magufuli ana jeuri sana ana uhakika pesa ameshakusanya ya kutosha na ndiyo maana hata hawa Wazungu wakimletea za kuleta anawapotezea.
5. Hivi sasa wanaofanya maendeleo ni wale wanaopata pesa kihalali, majipu yote hivi sasa hayana chao.
6. Siku hizi kesi zikikaa sana ni siku saba hukumu inatolewa. Si ulimsikia wakati alipokutana na wafanyakazi wa Mahakama alivyoongelea inakuaje watu wanakamatwa na vidhibiti lakini unaambiwa uchunguzi bado unafanyika, uchunguzi gani wakati mtu kakamatwa na madawa ya kulevya?
7. Hospitalini sasa hivi ukienda unapokelewa kama mfalme na lazima upate dawa. Nyie acheni jamani tuliteseka sana.
8. Wafanyakazi zamani walikuwa wanakwenda kazini muda wanaotaka na wakati mwingine walikuwa wakiona wamechelewa wanapiga simu na kuomba wasainiwe halafu hawaendi.
Hayo ni badhi tu ya yale yaliyokuwemo kwenye mazungumzo ya abiria ndani ya daladala. Kiukweli wananchi wana imani kubwa sana serikali ya JPM.
Jambo ambalo sikulijua kabisa ni hili la wananchi kupuuza na kudharau kile kinachofanywa na upinzani hasa yaani kususia vikao vya bunge, kubeza hatua zinazochukuliwa na mhe. Rais Magufuli n.k.
Mkuu, unafikiri ukiniambia shame on me utakuwa umesaidia kitu? Hayo ni maneno ya watu siyo yangu. Labda kusema kuna watu ndani ya CCM hawataki JPM apewe kijti ndiyo niseme shame on you, hizi zilikuwa propaganda za zenu UKAWA, julai siyo mbali JPM atakabidhiwa chama na wana CCM wako tayari Chama kisafishwe, hakuna kurudi nyuma, jifarijini na maneno yenu ya shame on you. Ndege imeshaondoka hivyo.shame on you.. hayo maoni ni ya watu au ya kwako? hv huna taarifa kuwa ndani ya chama chako mabosi zako hawamtaki achukue kijiti? usirudie tena kuandika uzi kama magazeti ya shigongo au kama G.mlinga
hahaaa, mlinisema kwenye ubunge wa kuteuliwa, U-RC, leo tena U-DC? siko humu kutafuta cheo. Magufuli atamaliza miaka 10 ataniacha humu napigania kile ninachokiamini. Hata CCM wenyewe wakiwa wababaishaji kama UKAWA, sisiti kuwachana live. Kukumbatia FISADI kuliniondoa kwenye reli kabisa. Nililipinga likiwa CCM na kamwe siwezi kuwa pamoja na chama chenye watu wa kujali maslahi binafsi.Kama hukuchaguiwa ukuu wa wilaya hata mimi nitampongeza rais kwa kukuacha, yeye mwenyewe anajua bado haeleweki ndio maana anaomba kuombewa na asicheleweshwe maana anaona siku zinaisha na bado hata haja nyanyua mguu kusonga mbele now anasema anacheleweshwa wewe unasema anakubalika, haa wanamkubali kwa kuchelewa kuanza?
Manyu utayaweza? Achana nayo yqjibarague. Hawsomi mada nzima wakajua nini kimeandikwa.Mitaa yote unaijua? Au unaiishi mitaa yote?
2020 tutajua nani mnafiki mimi au wewe. Wanaopiga ni wananchi siyo nyie.Njaa na shibe ni vyote ni shida.
Mimi nimesikia watu wakilalama na si kusifia. Hasa hasa lilipotajwa suala la 'MITUMBA'. Tata Madiba, Mungu anaona zaidi ya JF...unafiki una adhabu ya moto.