Serikali ya Rais Magufuli imefikaje hapa?

MTU aliyesema hakuwahi kutamani urais wala hakujipanga kuwa Rais na aliyekiri wazi wazi kuwa Urais ni kazi ngumu sana kwake na anajuta kwanini aligombea unategemea nini la ziada?

Unategemea nini kwa daktari aliyekata tamaa kwa mgonjwa?

Mmechoka kumpa muda?
Naona unaweweseka kweli
 
Mnarudi kule wewe na nani?

Usiweke mwanvuli wa fikra zako kwa wananchi wote.

Jenga hoja kwa maslahi ya fikra zako na siyo kuchukua kazi za fikra za wananchi wengine bila ridhaa yao.

Umetumia scientific research ipi kufahamu kama mwanzo ulikuwa mzuri na sasa ni mbaya?
Kutumbua majipu mbele, kubana demokarasia nyuma. Umeelewa?
 
Mnaompinga magufuli wengi wenu mnatokana na jamii ile iliyokuwa ya watu wachache ambao mlikuwa mnanufaika kutokana na mfumo mbovu wa serikal ya awamu ya nne,mpaka dkk magufuli amajitahidi sana na tayari ameshatupa matumaini ya Tanzania mpya.
Hata kidogo ina maana waliokuwa wananufaika ni wengi zaidi kuliko wanaonufaika sasa. Au anataka walimie meno?
 
Mwanzoni mwa Serikali ya Awamu ya tano,chini ya Rais Magufuli,kulikuwa na matumaini makubwa. Matumaini ya kuona na kusikia mambo tofauti. Matumaini ya kuachana na mazoea yasiyopendeza.

Matumaini ya kupunguza walalamikaji na kuongeza wawajibikaji. Kuanzia kwa wafanyakazi,viongozi hadi wanafunzi,matumaini ya mabadiliko ya kweli yalijaa. Matumaini ya kuondolewa kero na karo na kusonga kama Taifa.

Sasa,mambo yanarudi nyuma. Yanarudi yale. Tunarudi kale. Kule. Wafanyakazi wa NIDA wanasaka haki zao za kuachishwa kazi. Wabunge wa upinzani wanaadhibiwa kwa hoja ya kitaifa. Wananyamazishwa. Wanafunzi wa vyuo wanagoma na wengine wanarejeshwa makwao bila makosa yao.

Hakika,tunarudi enzi zile zile. Kwa mwanzo mzuri na wa kuvutia ule,Serikali ya Rais Magufuli imefikaje hapa?

Mzee Tupatupa wa 'Ulevini' Lumumba,Dar es Salaam

"Enzi zile" zipi?
 
Najuta kupoteza kura yangu 2015 aisee! Raisi gani anayeamini kila umbea anaopelekewa!mfano tamko lake la leo khs eti firm iv kusoma university
 
Atalipwa 2.3bn huko nida
 
Mnafiki mkubwa hujawai kuwa na matumaini na Magufuli wewe matumaini yako na akili zako ulimkabidhi Lowasa na hata mwenye kiti wako alimkabidhi kila kitu mpaka chama!
 
Mnaompinga magufuli wengi wenu mnatokana na jamii ile iliyokuwa ya watu wachache ambao mlikuwa mnanufaika kutokana na mfumo mbovu wa serikal ya awamu ya nne,mpaka dkk magufuli amajitahidi sana na tayari ameshatupa matumaini ya Tanzania mpya.
Hivi Tanzania mpya itakuwaje?
 
Mnafiki mkubwa hujawai kuwa na matumaini na Magufuli wewe matumaini yako na akili zako ulimkabidhi Lowasa na hata mwenye kiti wako alimkabidhi kila kitu mpaka chama!
Kwani kunatofauti gani na wewe? Wewe matumaini yako na akili si umezikabidhi kwa Magufuli? Hata JK, Kinana na wanaccm wote si mmekabidhi kwa Magu? Au nakosea?
 
Mnaompinga magufuli wengi wenu mnatokana na jamii ile iliyokuwa ya watu wachache ambao mlikuwa mnanufaika kutokana na mfumo mbovu wa serikal ya awamu ya nne,mpaka dkk magufuli amajitahidi sana na tayari ameshatupa matumaini ya Tanzania mpya.
Hapa unalazimisha.

Unawajua wote wanaompinga Magufuli na point zao?
 
Najuta kupoteza kura yangu 2015 aisee! Raisi gani anayeamini kila umbea anaopelekewa!mfano tamko lake la leo khs eti firm iv kusoma university

Cha kusikitisha ni kwamba kwa hii comment yako unaweza fungwa au faini sio chini ya 3million ati makosa ya mtandaoni, kila opinion imegeuka kua kosa kisheria, na sijui anayechagua kua maneno flani ni kosa na mengine sio kosa ni nani.

Uchaguzi ujao nagombea ubunge, siwezi kaa naona watu kama Agnes Marwa wamekaa bungeni wanamwaga pumba na mambo ya ovyo yanayoendelea alafu nikakaa kimya tu.
 
Serikali imechuja haraka sana,inaonekana hawakujipanga sana,kama umekaa serikalini miaka ishirini halafu hujui jinsi gani ya kuishughulikia sekta ya sukari!! Ina maana wakati serikali zilizopita zinaafanya maamuzi kuhusu sukari alikuwa haingii kwenye Baraza la mawaziri?
Tatizo anataka sifa kuonekana anabana.

Wakati anabana kabla hata hajapanga akibana kukitokea na upungufu atafidiaje.

Matokeo yake serikalibinaagiza sukari kutoka nje baada ya kupiga marufuku sukari ya nje.

Hopeless country bumpkin.
 
Kama hakuataka mbona alichukua form, siku zote kama unataka kufanya jambo fulani.. Ukilifanya kwa vitendo ndio utaonekana kweli ulikusudia.. Kuliko angekua anasema anataka alafu katika vitendo asichukue form
Magufuli hana breki ya mdomo.

Mambo mengine rais hatakiwi kusema.

Yeye anabwatuka tu.
 
Back
Top Bottom