Sijui kwa nini ninyi Watanzania manojadili suala la Bajeti ya Wizara ya PM mpenda kukejeri uamuzi wa wizara hiyo kuwapa na kuwataka wafanyakazi wake, kuanzia mwaka mpya wa fedha ujao, kutumia usafiri wa bajaji na boda boda. You guys you seem to be very cynical. Kama kuna watu wadhani mabadiliko ni maneno tu ya wansiasa, kwa kutumia msemo wa waswahili, imekula kwao.
Policy environment ya serikali ya JPM ni kuhakikisha maisha ya maofisa wa serikali yanawiana na maisha ya wananchi wa kawaida. Closing an artificial status gap. Kwamba kuwa ofisa waserikali hakumaanishi kutajirika. Hii ni mentality iliyokuwepo huko nyuma tuliko toka, hasa katika tawala za BWM na JK.
Kwamba kuwepo kwa uwiano wa maisha baina ya maofisa wa serikali na watu wa kawaida kutahamasisha wananchi wengi kulipa kodi, kutapunguza au kuondoa kabisa corruption mentality kuwa ukiwa ofisa wa serikali basi you are presumed tajiri/mkwasi, hivyo unastahili kunatumia magari yenye hadhi kama V8. Mentality hii imekuwa ikiwafanya wananchi kuwasujudia wezi wa mali ya umma na wala rushwa, kwa kuwaogopa na hivyo kushindwa ku-monitor mienendo yao.
Treatment ya serikali kwa maofisa wake imechangia kwa kiasi kikubwa kwa maofisa wala rushwa kujificha na kupewa heshima wasiostahili kwa presumption kuwa ni matajiri kumbe ni wezi na wala rushwa tu wasiostahili hata chembe ya heshima.
Ukisoma bajeti ya PM unaona genuinity; Tzs.236.7bn kati ya hizo, Tzs.71.5bn ni pesa za matumizi ya kawaida wakati Tzs. 165.2bn ni pesa za matumizi ya maendeleo. Tujiulize (kwa ushahidi) ni wakati gani katika historia ya bajeti ya Tanzania makadirio ya bajeti ya maendeleo yaliwahi kuzidi makadirio ya bajeti ya matumizi ya kawaida? Tena kwa Zaidi ya asilimia 100!
Tuache mazoea tuliyotoka nayo huko nyuma, these guys are serious. Tusiwakebehi, tuwaunge mkono.