Serikali ya DRC, kuomba michango ya kusaidia jeshi lake.

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Jan 31, 2025
376
639
1740065740894.png

Tangazo hili, lilitolewa na kusainiwa na waziri wa fedha nchini DRC, akiwataka wananchi kuchangia fedha kwenye account zilizowekwa katika tangazo hilo, llengo likiwa ni kukusanya uwezo wa kulisaidia jeshi la serikali huko mwashariki mwa nchi, kutokana na alichokiita vita vya kukabiliana na uvamizi.
 
Daah M23 chukueni tu iyo nchii asee
hata m23 wakifanikiwa kuchukua hawatabadili lolote maana wao wanafadhiriwa na mtu , wakiteka nchi mfadhiri atawadhibit wawe na serikali dhaifu ili waendelee kuiba mali ndan ya DRC , wakitaka amka tu mfadhiri anaunda kundi au mapinduzi ili kuwatoa wanaotaka amka , swala la DRC halitakuja tatuliwa na wakongo bali majirab tukiungana na kuacha akili za uomba omba bas DRC itakuwa huru
 
Ni tofauti kabisa na Baba yake hayati Etienne Tshisekedi angalia alivyowasababishia Askari wa South Africa wawe mateka.

View: https://youtu.be/puHTYTofgqg?si=FycV3jsqgw_zFd50
Sikiliza hii Video uone Tshisekedi alivyowaingiza watu Vyoo vya Kike.

Mr. tall aliwaonya wakae mbali, wakajiona wanaweza, akachimba kashimo kidogo tu, wakadumbukia. Sasa hivi,kawanyamazia, lakini kawaponda panapouma. Waliambiwa njia pekee ya kuachiwa huru, ni kupitia Rwanda,wakiwa wamevalia sale zao,bila silaha wala gari. South Africa, ikadai inahitaji wapite kama diplomats. Vuta nikuvute ndo hapo ilipobaki sasa.
 
View attachment 3243025

Tangazo hili, lilitolewa na kusainiwa na waziri wa fedha nchini DRC, akiwataka wananchi kuchangia fedha kwenye account zilizowekwa katika tangazo hilo, llengo likiwa ni kukusanya uwezo wa kulisaidia jeshi la serikali huko mwashariki mwa nchi, kutokana na alichokiita vita vya kukabiliana na uvamizi.
Si ajabu na hizo fedha zikapigwa watu wakanunua Property huko France wanapopapenda.
 
Mr. tall aliwaonya wakae mbali, wakajiona wanaweza, akachimba kashimo kidogo tu, wakadumbukia. Sasa hivi,kawanyamazia, lakini kawaponda panapouma. Waliambiwa njia pekee ya kuachiwa huru, ni kupitia Rwanda,wakiwa wamevalia sale zao,bila silaha wala gari. South Africa, ikadai inahitaji wapite kama diplomats. Vuta nikuvute ndo hapo ilipobaki sasa.
Mkuu mbona matangazo ya baadhi ya nchi za ulaya ikiwemo Belgium na jirani yetu 🇰🇪 kuwataka watu wao waondoke yameshamiri usalama upo?
 
Back
Top Bottom