Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 667
- 1,371
Watu wameng'ang'ania kujadili uhalali wa kuagiza umeme nje ya nchi. Kuna shida ingine kubwa haimulikwi.
Tatizo haswa la Tanzania ni kwamba, baada ya ule mradi wa bwawa la umeme kupitishwa na kuanza rasmi, kuna kitu kingine kilipaswa kufanywa sambamba na mradi wa bwawa la Nyerere, nacho ni Power Grid Transmission infrastructures ambayo ingemudu kusafirisha hicho kiasi kinachozaliswa.
Kwenye uchumi kuna bidha ambazo zonaendana matumizi, ukipika chai, lazima uwena sukari na majani ya chai. Sasa huwezi tu kununua sukari halafu ukasahau majani ya chai.
Walichofanya serikali ya CCM ni kutumia Trillioni 9 (5% ya GDP) kujenga capacity kubwa kiasi hicho na kusahau kuwekeza kwenye Power Grid. Maana yake ni kwamba, kama huna efficiency kwenye transmission, lazima iwe ghali na ineffective kupeleka umeme kule ambapo grid ni changamoto.
Kwa mahesabu ya haraka haraka, ku invest kwenye grid ya 600km inaweza kugharimu kama $1.2 billion (kama trilioni 3 hivi). Na hii risk nadhani ingepaswa kuonekana kwenye andiko la mradi.
Ambacho wangepaswa kufanya serikali ya Samia ni kuomba radhi watanzania kwa kufanya mradi mkubwa wa matrilioni bila kujua ukiisha huo umeme utasafirishwa vip.
Kwahiyo watu wasijikite sana na masuala sijui ya ni halali au sio halali kuagiza umeme nje, au sijui eti hasara ya bilioni 30 kwa mwaka, kuna hoja kubwa ya upotevu wa trillioni 9 ambao kwasasa ni wazi capacity yake haitumiki kwa asilimia 100 kwasababu ya poor grid
Kwahiyo wote mnaotetea kununua nje umeme hamjisikilizi. Na kununua umeme nje sio sustainable, kwasababu hujui ni kwa haraka kiasi gani huo umeme wa nje utamudu demand growth ya Tanzania.
Maana yake hapa ningetegemea serikali ije na project ingine ya kujenga power grid ya 600km ambayo ni uwekezaji kama wa 3 trillion hivi. Huwezi kusema tu tutakuwa tunanunua umeme Ethiopia halafu ukaishis tu hapo bila way forward, ukizingatia una bwawa la 9 trillion pesa zimelala tu hapo.
Inasikitisha