Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,294
- 3,483
Getty ImagesCopyright: Getty Images
Serikali ya Afrika Kusini imetuma maombi rasmi kwa mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin iwapo atawasili nchini humo.
Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini, Democratic Alliance, kinasema kuwa haya ni makubaliano ya matakwa yake: chama hicho hapo awali kiliwasilisha ombi kwa mahakama kulazimisha serikali kutekeleza agizo la kukamatwa kwa Putin lililotolewa mwezi Machi na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko The Hague.
Afrika Kusini inawajibika rasmi kufuata matakwa ya ICC, na Putin alialikwa kwenye mkutano wa BRICS utakaofanyika Agosti mjini Johannesburg, lakini uongozi wa nchi hiyo haukuficha ukweli kwamba haikuwa na nia ya kumkamata rais wa Urusi.
Hata hivyo, serikali ya Afrika Kusini haikupata njia yoyote ya kisheria ya kutotekeleza kibali hicho. Viongozi wa Afrika Kusini wamesema kwa uwazi katika siku za hivi karibuni kwamba walimwomba Putin asiende, na siku ya Jumatano aliamua kutokwenda, ingawa si lazima kutokana na hofu ya kukamatwa.
BBC SWAHILI