Serikali: Uwekezaji unaofanyika Kiwanda cha Chai cha Mponde utaongeza thamani kutoka Tsh. 790m hadi Tsh. Bilioni 4.8

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,807
13,575
WhatsApp Image 2024-08-10 at 14.21.17_7af264f2.jpg

Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya kumiliki kiwanda hicho iliyofanyika katika Ofisi ya PSSSF, Msajili wa Hazina iliyofanyika Agosti 9, 2024 Jijini Dodoma.
Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), wameingia ubia wa kumiliki Kiwanda Cha Chai cha Mponde kwaajili ya kuongeza tija katika uzalishaji, huku wadau mbalimbali wakitakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika zao la Chai.

Katika ubia huo Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa niaba Serikali inamiliki hisa ya asilimia 16, huku PSSSF na WCF wanamiliki asilimia 42 kila mmoja.

Pia soma: Katavi: Kiwanda cha Maziwa chafungwa baada ya uhaba wa mali ghafi ya maziwa

Akizungumza jijini Dodoma, Agosti 9, 2024 katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya kumiliki kiwanda hicho iliyofanyika katika Ofisi ya PSSSF, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu amesema kuwa uwekezaji huo unakwenda kuongezeka thamani ya kiwanda kutoka shilingi milioni 790 zilizopo na kufikia Bilioni 4.8.
WhatsApp Image 2024-08-10 at 14.23.51_66265c1c.jpg

WhatsApp Image 2024-08-10 at 14.23.52_ab39e90d.jpg

Mchechu amesema wanatarajia kuwekeza shilingi bilioni nne ambapo mpaka sasa tayari uwekezaji katika kiwanda hicho umefika bilioni 2.5.

“Kiwanda hiki kinakwenda kufufua uchumi kwa wakazi wa Korogwe na wakulima wa zao la chai watapata fursa ya kupata soko la uhakika wa kuuza mazao yao" amesema Mchechu.

Mchechu ameongeza kuwa kupitia uwekezaji huo, Serikali inakwenda kunufaika na ulipaji wa kodi, huku akisisitiza umuhimu wa Menejimenti kuongeza ufanisi katika utendaji ili waweze kuleta gawio kama ilivyo kwa taasisi nyengine.

“Nawashukuru sana PSSSF, WCF kwa kukubali wito wa kwenda kufanya uwekezaji katika sekta ya kilimo cha chai, ukiangalia tuna ardhi nzuri ambayo tunaweza kufanya uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali nchini,” amesema Mchechu.

Aidha, amesema kuwa Tanzania kuna ardhi kubwa na yenye rutuba ambayo inakubali kilimo cha chai hasa Mikoa ya Iringa na Mbeya, huku akieleza kuwa kulikosekana wawekezaji wa viwanda katika zao la chai ambalo linalimwa kwa muda mrefu na kuleta tija.

"PSSSF na WCF wanapoonekana katika uwekezaji sekta ya kilimo itawavutia wadau wengine na kufanya vizuri sekta hii, kwani kwa muda mrefu wakulima walishindwa kulima zao la chai kutokana na kukosa soko la uhakika," amesema Mchechu.
WhatsApp Image 2024-08-10 at 14.22.50_601c5d99.jpg

Meneja Mkuu wa Kiwanda Cha Chai cha Mponde, Muhoja Manane, akizungumza alipokuwa akitoa taarifa fupi ya uzalishaji wa Kiwanda hicho.
WhatsApp Image 2024-08-10 at 14.22.27_0f15ea59.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Abdul -Razaq Badru, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Agosti 9,2024 Jijini Dodoma.
Mchechu amebainisha kuwa Tanzania inazalisha kiwango kidogo cha chai na kufanya mauzo kuwa dola milioni 50 kwa mwaka, tofauti na nchi jirani ya Kenya ambao wanauza zaidi ya dola Bilioni moja.

“Tupo chini katika mauzo kwa sababu tuna mwamko mdogo wa kufanya uwekezaji katika zao la chai, lakini leo tunashukuru tunawapa nafasi kiwanda hiki, menejimenti, bodi kuanza kukimbia katika utekelezaji wa majukumu yao” amesema Mchechu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma amesema kuwa uwekezaji huo unakwenda kuibua uchumi wa wananchi katika mkoa husika, kwani wakulima wengi wa eneo wanakwenda kuuza zao la chai katika kiwanda hicho.
 
Back
Top Bottom