Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 14,083
- 28,690
Ubunifu ndo bidhaa adimu zaidi kwa sasa duniani ambayo endapo utaitumia vizuri unaweza kujihakikishia una survive vizuri katika dunia hii ya ushindani mkubwa.
Kwa miaka mingi, Tanzania imekuwa ikisemwa kuwa na vivutio vingi ikiwemo rasilimali, mbuga, wanyama ila kwa bahati mbaya haijaweza kuvitumia ipasavyo na kupata faida ya kweli.
Nimeshawahi kusema mara nyingi humu kuwa shida kubwa tuliyonayo watanzania ni matumizi sahihi ya rasilimali akili ambayo endapo tungeitumia vizuri tungeweza kufika mbali sana na wananchi wetu wakawa na maisha mazuri sana.
Kwa sasa duniani, Utalii ndo bidhaa ya kukupa hela nyingi zaidi kwa urahisi zaidi. Hivyo tukiutumia huu utalii vizuri inawezekana sana tukawa nchi yenye uchumi mkubwa sana.
Kama nilivyosema kwenye uzi wangu wa jana. Ubunifu uliofanywa kuhusu Land Rover Festival ni jambo kubwa sana ambalo pamoja na kutakiwa kupongezwa, ni jambo linalotakiwa kuwekewa mkakati maalum kuanzia sasa na kufanywa kama tukio kubwa zaidi la kuleta watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali Duniani.
Tukio hili tayari limeshawafikia watu wengi katika media za kimataifa hivyo ni vyema kwa Serikali sasa kuliwekea mkakati rasmi ili liwe na muendelezo mzuri na ikiwezekana liwe tukio kubwa zaidi la kiutalii kwa Afrika.
Nategemea sasa Serikali wataweka miguu yote kwenye tukio hili na kilibrand zaidi ambapo kwa mwaka kesho washiriki watapata kuona vitu vingi zaidi vinavyohusiana na Tanzania ikiwemo utamaduni, mziki, vivutio, madini na mambo mbalimbali.
Kazi kwenu Serikali. Tunatarajia sasa tufunguke zaidi na tusiitwe tena a Sleeping giant of East Africa.