Serikali: Taarifa za Wahisani kujitoa kusaidia Bajeti ya 2016/2017 si za kweli

Mi nafikiri kama TRA ikijikita katika ukusanyaji kodi kisawasawa na kuwekeza katika viwanda na Kilimo Tanzania itaweza kujisimamia ;)
 
Kwa waliokuwa wanapondea Tanzania kunyimwa msaada na nchi wahisani mbona wajitokezi hata kwenye kanusho hili?

'Threads' zinazohusu MCC zilijaza page lakini kwenye kanusho watu wamenywea kweli hahahahaa....
 
Hivi kumbe misaada inapendwa hivyo? kwa hiyo zile kelele za kujitegemea zilikuwa ni mbwembwe tu!!
 
kama pamoja na misaada yote hiyo bado ndio tuko hapa,sasa hawa wanaopiga filimbi humu kwamba tujitegemee wanataka tujitegemee kufanya nini ladba kama ni kuwapa wake zetu mimba hilo tunaweza kujitegemea lakini zaidi ya hapo chaliiiii!
 
Hawa Wizara ya Fedha mbona wanatofautiana na viongozi wa serikali katika matamko yao.

Sasa wananchi tuelewe nini!!!!! ya kuwa tunataka kujitegemea au bado ni ombaomba??????

Saidia baba.jpg

Waziri aliibuka hadharani mara tu baada ya tamko la MCC kutolewa. Akasema kuwa Tanzania tunajiweza na tutaendesha bajeti yetu kwa mikono yetu; na hata katika mipango ya bajeti mwaka huu pesa ya MCC haikuwekwa, sasa huyu naye anasema kuwa bajeti inachangiwa na pesa za wahisani wakiwemo Umoja wa Ulaya (Je hawa ni akina nani kama siyo walewale USA na Britania????)

Tunaomba serikali wasilete siasa katika suala kubwa kama hili linalohusu mustakabali wa maisha ya Watanzania.

NI NANI SERIKALINI MWENYE KUWA NA MADARAKA YA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI??? MAANA HAWA WOTE WANAOIBUKA HATUWAELEWI KABISA. TUNATAKA TAMKO LA SERIKALI
 
Kwahiyo wewe unachotaka ni official tangazo siyo uhalisia ?

Tuwe wakweli tuache kudanganyadanganya wananchi.
Tumenyimwa misaada, sasa tutatokaje hapa tulipo.
Tufanyeje?
Duh. Taratibu mzee. Huwezi ku sustain kwa msaada. Fanya kazi ulipe kodi ndo uwe mkali kudai matumizi ya kodi zako. Sio kupiga tu domo kwa kitu usichokijua.
 
Duh. Taratibu mzee. Huwezi ku sustain kwa msaada. Fanya kazi ulipe kodi ndo uwe mkali kudai matumizi ya kodi zako. Sio kupiga tu domo kwa kitu usichokijua.
Sisi tulikuwa tumezoea misaada mbona MCC wamekata kelele zikaanza au tulikuwa tunajitegemea since b4 sasa tumekataa misaada?
Vp bwana wewe?

Kodi tunalipa kila kona usifikiri kodi inatoka kwenye huo mshahara wako tu.
Hata hii bundle unayotumia hapa kuandika hizi ngonjera hapa kuna kodi ndani yake.

Sasa fungua domo kwa vitu unavyovijua tukusikilize
 
Sikiliza Mkuu. Zambia hawana misaada hiyo mwaka wa tatu huu. Halafu wao hata kukopa hawakop. Walinyimwa et hawakopesheki. Sawa walikuwa na shida ya kutokusanya kodi na uchumi wao ni mdogo lakini hujasikia wakililia misaada. Walichofanya ni kuanza kukusanya kodi effective na kusonga mbele. Hakuna mwananchi aliekufa na njaa. Wako safi tu kiasi chake. Mataifa yote yenye uchumi wa kati yalifika apo baada ya kususiwa na Mataifa ya magharibi. Hakuna nchi iliyowahi kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kupata misaada mingi. Dunia nzima haipo.

Hata wazee wetu waliopigania uhuru wa nchi yetu hii na hata nchi zote za africa kama wangeogopa kuwa wazungu wakiondoka tutakufa njaa wasingepambana kudai uhuru wa mtu mweusi.

Ukiangalia tu wakat wa Nyerere viwanda vingi vilijengwa kipindi chake. Kila mkoa ulikuwa na viwanda zaidi ya vitatu. Lakini ni kipindi tulichowahi kuvunja uhusiano na uingereza na Mataifa kibao na ndo kipindi ambacho taifa liliheshimika duniani pote.
Mawazo ya kuabudu misaada na wazungu yalipotuingia tu tukauza viwanda vyote na ndo mwanzo wa nchi kurudi nyuma na umaskini kuongezeka kwa sabb tu tulianza kuwasikiliza Marekani na washirika wake kuhusu sera za uchumi.

Hii kitu iko wazi kabisa kuwa huwezi kutegemea maendeleo kwa hela ya msaada. Lazima ujifunze kuzalisha kilicho chako.

Halafu hakuna waziri alielilia msaada. Kila waziri alisema tulitegemea hivo na ndo maana tulijiandaa. Ukimsikiliza mkurugenzi wa tanesco atakwambia wazi kuwa miradi ya umeme iliyokuwa ifadhiliwe na MCC haitaathirika kwa sabb tayari walishaitafutia fedha.

Ile trilion moja ya MCC ni program ya miaka mitano. Yaani ni hela ambayo kwa mwaka inatoka kiasi cha bilion mia mbili tu then kwa miaka mitano. Sasa hiyo bilion mia mbili kwa nchi kama hii yenye makusanyo ya bilion elfu moja na mia tatu kwa mwezi itashindwaje ku cover hiyo bilion mia mbili kwa mwaka mzima.

Au ni kilema tu cha kudhani misaada ndo kila kitu kwa mtu mweusi. Au ni mind set yako tu ndo tatizo. Au ni aina tu ya elimu uliyonayo. Lakini hamkusoma hata historia iliyowafundisha jinsi akina chief mangungo walivouza nchi kwa msaada wa kipande cha nguo. Sijui kama una akili sawa sawa.

Hebu watanzania fungukeni akili muone kuwa misaada inawamaliza. Mnaibiwa. Mnadhalilika.
Waswahili wanasema heri lawama kuliko fedheha. Sasa sijui huo msemo umegeuzwa.

Use Ur brain man. Think think think!!!!!
 
Mzee hiyo ya Zambia kutokupokea misaada sijui vizuri ila nina a lot of ???? hapo.

2ndly sishabikii misaada, ninachosema ni kwamba serikali imekuwa ikiendesha nchi kwa misaada.
Ni lini tulipewa misaada tukakataa tukasema hapana sasa imetosha hatutaki tunajiendesha wenyewe.
Ilishawahi kutokea hiyo?
 
Uliza tu. Au google tu utaiona wala sio siri. Zambia ni majiran zetu. Fuatilia tu kuhusu uchumi wao. Na sio misaada tu. Hata kukopa hawakopi. Fuatilia siku hizi dunia ni kama kijiji
 
Fikra za wanaopenda Tanzania isiwe ya neema tuwaiteje! Kama wenye mtizamo huo ni wapinzani, wanasukumwa na siasa, wajitambue. Serikali ikishindwa kutimiza wajibu wake kwa kukosa uwezo, hasa fedha kukidhi mahitaji ya kujiendesha na naendeleo, wote tutaathirika. Fikra za kuombea mabaya ni utoto
 
Bado tunawahitaji sana wahisani. Fedha anazokusanya Magufuli kwa njia ya TRA ni fedha za madafu. Ukitaka kununua mafuta na mahitaji yetu mengine mengi inabidi kutumia fedha za kweli (hard currency).

Tunatumia fedha za kweli nyingi sana lakini tunazisalisha kidogo sana. Bila wahisani kujazia tungekuwa tena kwenye foleni za mgao wa sukari na mchele na hata mabaya zaidi ya hayo.

Mgonjwa hawezi kujivuna kwamba hahitaji dawa. Kuna siku tutajitegemea lakini itakuwa baada ya kuimarisha uchumi na kutokomeza ufisadi uliokidhiri.
 
Kwa hiyo katibu mkuu wa Wizara ya fedha anapingana na kauli za mawaziri wa fedha na mambo ya nje waliotoa matamko juu ya suala hilo, anataka kutuambia mawaziri waliudanganya umma

Kwa ushauri wangu huyo katibu mkuu angekaa kimya kwanza mpaka moto upoe, haya mambo ya kukubali baadae kukanusha yanaweza kututokea puani, tusitake kushindana na Marekani au kujaribu kutoa impression kwamba hata wasipo tupa msaada hatujali!

Kumbuka jamaa hawa wana mbinu nyingi za kutuwekea kibano hasa tukijionyesha vichwa ngumu, tusianza kukuza kuza mambo ambayo yanaweza kumuweka Dk.Magufuli katika hali ngumu.

Wachumi wote wanao jitia kumshauri Dk.Magufuli akomalie nchi za magharibi wakimpa hoja ambazo hazina mshiko wowote zaidi ya kunakili RAW siasa za ujamaa na kujitegemea ambazo hazikuwahi kutufikisha popote, hali yetu ibaendelea kubaki almost vile vile miaka nenda rudi.

Wachumi hao saa hizi wanajifanya kuikomalia MCC na wafadhili wengine, wakumbuke kwamba mwisho wa siku mambo yatakapo anza kukwama wao ndio watakuwa wa kwanza kuingia mitini na kumuhacha Raisi wa watu kwenye mataa.
 
Habari ya mchana great thinker!!

Itachukua muda kidogo hadi tuzoee hili neno "KWA HISANI YA CHINA" maana tulizoea kwa hisani ya Marekani. Nawaza tu kwa sauti.

Kweli Pombe amekuja na Mengi..
 
Hakika sasa Tanzania ni kama mwanamke wa Tanzania yenyewe bila kuwezeshwa hawezi chochote , kumbe yale mapovu yaliyomwagwa humu na vijana wachumia tumbo wa lumumba na kisiwandui wakiongozwa na huyu Kizabao kwamba Misaada ni utumwa ilikuwa uongo ?
 
Misaada ya nini si mmesema inakandamiza uhuru wetu mnataka tujitegemee!!

Hii ndio sura halisi ya Mtanzania leo anasema hiki kesho anasema kingine na mara nyingine hujikuta amepingana na kauli ya mwanzo.
 
Back
Top Bottom