Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,129
- 25,105
Kuna sheria yoyote iliyowekwa ili kufanya hili jambo kutojirudia tena? Maana naona kuweka jipo la madaktari tu haitoshi maana akiingia Rais mwingine asiyefuatilia sheria sana kama tulikotoka basi hata hayo majopo hayatazingatiwa sana au wataambiwa tu andikeni nikatibiwe nje.
Tatizo ni mamlaka moja kuingilia mamlaka nyingine na kuweza kupewa vitisho vya kufungwa nk,hivyo visipodhibitiwa kwa sheria ninaona hatari ya kujirudia kwa kasi miaka ijayo...kuwe na mipaka ya kuingilia mambo ya kitaalamu kwa hawa wanasiasa wetu,hilo tu basi kwa mani yangu.
Mambo hayabadiliki overnight tu mkuu, huu Ni mwanzo halafu sheria na kanuni zitafuata ili kusimika mizizi. Tukisubiri hadi sheria zitungwe zianze kufanya Kazi hapo tutasubiri miaka mingine kadhaa. Kwa mamlaka ya ofisi ya Rais anaweza fanya hili na sheria zikafuata ni mwanzo mzuri