Tetesi: Serikali kununua ndege mpya kwa ajili ya Rais na viongozi wakuu wa serikali

Acha ndege inunuliwe ,

Mbona, Tanzania mnalalamika Sana.
Mfano, kila siku kila mahala, (wengine wamehamia USA wanaitukana serikali na nchi iliyowalea hadi wakaelewa kuoga na kuvaa) watanzania wengi huwa mnapenda kujilinganisha na nchi Kama USA na zile za ulaya.

Hapo USA, Trump kaingia WH, kaomba Air Force One mbili zitengenezewe Kwa ajili ya ikulu /uongozi wake.

Sasa, mbona mnalalamika pale nchi yetu na viongozi wakiiga kutoka nje ya nchi, Kama hilo la kununua ndege ya Rais !?

Mbona mengine, mnatoa mifano na kuandika makablasha makubwa-makubwa na kuongea hadi mate yanawakauka kwa kutoa mifano toka huko USA na ulaya!

Acheni unaaaa aiseeeeh (In Mrema's voice )
Hujitambui wewe na siku ukijitambua utakuwa umeshachelewa
 
Hapana hii habari sio kweli..Rais wetu wa wanyonge hawezi hata siku moja kufanya hayo mambo. Anajua vijijini hawana maji wala madawa. Aliwaahidi atapeleka maji swafi na salama na zahanati pamoja na vituo vya afya. Aliwaahidi kuboresha maisha hao..hakuahidi kununua ndege wala ndege ya Rais. Huyu ni Rais wa wanyonge hawezi kufanya hayo mambo kabisaa. Hatanunua ndege akaacha watu wafe kwa afya mbovu..ukosefu wa vyakuka..mfumuko wa bei..madawa..maji safi nk..huyu sio Rais wa starehe ni wa kufanya kazi tu. Tafadhali hizo habari sio kweli na naomba zisiwe kweli...
 
Hiyo ndege ni moja ya ndege imara kabisa zinazotengenezwa na wafaransa zikiitwa "business jet".

Kwa maelezo ya ufanisi wake kwenye matumizi zina la nyongeza maana umemaliza kila kitu.

Ila nina suali moja tu, kama ni kweli kwanini serikali inanunua hii modeli ya F2000LX badala ya modeli mpya kabisa ya F2000LXS ambayo ni toleo la 2014?

Kwani kama ni tofauti ya BFL yaani "balanced field length" zinapishana kidogo sana yaani F2000LX ina 5750 na hii ya F2000LXS ina 4675.

Sasa tofauti ni bei au ubora wa kuruka ama vipi?
Duuh JFs kweli ni kisima cha elimu mbali mbali...haya mnayajulia wapi
 
Hiyo ndege ni moja ya ndege imara kabisa zinazotengenezwa na wafaransa zikiitwa "business jet".

Kwa maelezo ya ufanisi wake kwenye matumizi zina la nyongeza maana umemaliza kila kitu.

Ila nina suali moja tu, kama ni kweli kwanini serikali inanunua hii modeli ya F2000LX badala ya modeli mpya kabisa ya F2000LXS ambayo ni toleo la 2014?

Kwani kama ni tofauti ya BFL yaani "balanced field length" zinapishana kidogo sana yaani F2000LX ina 5750 na hii ya F2000LXS ina 4675.

Sasa tofauti ni bei au ubora wa kuruka ama vipi?
Yetu macho
 
Ahsante mkuu kwa taarifa.

nadhani serikalii iweke wazi taarifa zake.

pia lazima mfumo wa manunuzi makubwa uzingatiwe. kuna kuna zabuni zitangazwe na watu washindanishwe.

watu wakipata madaraka wanajisahau na kupindisha mifumo mbali mbali wanasahau ipo siku wataacha haya madaraka waliyonayo leo na kesho hata kaburini watu watafukua mifupa na kuuliza kipi kilikuwa kipaumbele chako,infrastructure au human capital.
Kama ni kweli basi tunasubiri zzk atiririke na kututoa tongotongo
 
wakati ule tuliambiwa tule nyasi ndege inunuliwe,safari tutaambiwa tule rambirambi lakini ndege inunuliwe!!!!
 
Kheeee kheeeeeee wakati huo huo bajeti ya nchi ya 29 trilioni imekuwa hewa na hivyo kutolewa a little more than third of the total amount i.e. 34% of the actual budget.
Wakati huo huo sisi kajamba nani tuishio mwandiga tunamaliza siku 7 njiani kutoka kigoma hadi dsm
 
Miaka miwili tu bado cha maana hajafanya tayari anajinunulia Li Dege
sasa hela za reli ya umeme hana, anaenda kukopa SA, wabunge wanapoteza muda kujadili deficity budget
no ajira
no madawa mahospitalini
inflation rate haikamatiki
hela za huuu ujinga wa ndege anatoa wapi na hana hela au walizotaka kupiga kwenye dreamliner wanaamishia uku baada ya kuumbuliwa walizotaka kutupiga
 
Hela za rambi rambi za bukoba na arusha ndiyo zinanunua ndege....

Wagonjwa wanakufa mahospitalini hawana dawa.... Kijijini bibi anafuata maji km 10...
 
Kila kitu kinachotarajiwa kununuliwa na Serikali sharti iwepo kwenye bajeti. Je ununuzi wa ndege hiyo iko kwenye bajeti ya Serikali?. Mbona bado kuna changamoto nyingi sana za Huduma za Jamii hapa nchini. Ununuzi wa ndege ni wa nini kwa hivi sasa?.
 
Back
Top Bottom