Serikali kukosa mchango wa dawa toka USAID

Hii habari haijakamilika.Lakini katika kujipanga huko kwa serikali bado hiyo ni divertion ya Resources kutoka mahali maana sidhani kama walijua hawataongezewa muda.Gharama bado anabeba mwananchi wa kawaida wakati hatukua tumejipanga.Maamuzi mabovu yanayosukumwa na uroho wa madaraka Mwananchi analipia gharama

Watakosaje kujipanga wakati wanajua muda unaisha?
 
Mi naomba tatizo LA madawa kukosekana lisijitokeze.
Kuna watanzania hawaeleweki ni wanafiki kwa upande mwengine wanamponda kikwete kuhusu misaada baadae tena utasikia wanafurahia au kuhitaji misaada
Tuache unafiki tuseme na tushauri ukweli hakuna asiyependa kujitegemea tutafute namna na njia nzuri ya kujitegemea
 
Siku zote panapotokea migongano ya waliopo madarakani wanaoumia ni raia
Waliosoma hadithi ya Alan Quarteman wanaweza kuthibitisha hili. Sisi tutaambiwa kirahisirahisi tu kuwa wizara imejipanga na kuamini lakini ukweli athari zipo. Suala la Zanzibar lina negative impact kiuchumi na kisiasa na kijamii. Ubabe na maguvu havisadii
 
Mi naomba tatizo LA madawa kukosekana lisijitokeze.
Kuna watanzania hawaeleweki ni wanafiki kwa upande mwengine wanamponda kikwete kuhusu misaada baadae tena utasikia wanafurahia au kuhitaji misaada
Tuache unafiki tuseme na tushauri ukweli hakuna asiyependa kujitegemea tutafute namna na njia nzuri ya kujitegemea
Kutokana na matatizo ya kihistoria nchi za Africa ahziwezi kukwepa misaada toka ulaya
 
Hivi mradi KUFIKIA UKOMO maana yake ndiyo serikali KUWEKEWA VIKWAZO? au haya ndiyo mahaba niue
Sikia mladi wa afya marekan inasaidi nchi nying hapa kinachotokea n kutunyima kwa njia ya nyuma .... Tatizo ni zanzibar
 
Kutokana na matatizo ya kihistoria nchi za Africa ahziwezi kukwepa misaada toka ulaya
Ngoja wakusikie wanafiki waliokuwa wakimpamba na kumsifia kikwete kwa misaada sasa hivi wameamia upande wa pili wakiponda misaada
 
Kwani hamjui kwamba mwaka jana serikali ilianzisha mfuko wa Uchangiaji kwa ajili ya kununua dawa za UKIMWI? tayari serikali ilikuwa ilishajipanga toka Mwaka jana, kwa hiyo hakuna wasiwasi wowote kuhusu hilo.
Mkuu kwamakusanyo yanayo pungua hatuwezi kununua dawa za ukimwi kwa watu wetu jua marekani imeamua kutukimesha na tutegemee hali kuwa mbaya zaidi lazima tuisome namba
 
Hii habari haijakamilika.Lakini katika kujipanga huko kwa serikali bado hiyo ni divertion ya Resources kutoka mahali maana sidhani kama walijua hawataongezewa muda.Gharama bado anabeba mwananchi wa kawaida wakati hatukua tumejipanga.Maamuzi mabovu yanayosukumwa na uroho wa madaraka Mwananchi analipia gharama

Usikurupuke kuchangia jambo usilolijua: si kweli serikali ya Marekani imejiondoa kuchangia kwenye mradi huo ila kilichofanyika ni kubadili shirika lililokuwa linatoa huduma hii kwa niaba ya USAID: Mwanzo mradi huu ulikuwa unasimamiwa na JOHN SNOW INC kupitia kwenye mradi wa SCMS yaani SUPPLY CHAIN MANAGEMENT SYSTEMS. serikali ya marekani hutoa grant kila miaka 5, baada ya hapo hutangaza tender huko marekani mashirika mbalimbali kushindana, bahati mbaya shirika la JSI/SCMS halikubahatika kupata mradi huo, shirika lililo pata mradi huo na CHEMONICS ambalo ni jipya hapa Tanzania, ndiyo litakalochukua kazi za JSI/SCMS. Hivyo madawa yataendelea kutolewa japo serikali inakiwa kujipanga kwaani msaada hauwezi kuwa endelevu, pia swala hili halijawa ghafra limechukua miaka 3 kutafuta shirika jingine na kipindi cha mpito kukabidhi mradi ilifanyika.

Kazi iliyokuwa kubwa ilikuwa na kujenga mifumo ya MSD ambayo imekamilika ikiwa ni pamoja na kujenga maghara ya madawa ya kisasa yenye mifumo ya ki eletronic. kutambua dawa zinakozalishwa ikiwamo humu nchini. cha msingi serikali ijipange kuvisaidia viwanda vya ndani kutengeneza hizo dawa badala ya kuendelea kuagiza kutoka nje ya nchi.
 
Serikali itakosa mchango wa dawa zenye jumla ya gharama ya dola za Marekani 375 milioni sawa na Sh787 bilioni, ambazo zimekuwa zikichangiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID).

USAID ilitoa mchango huo chini ya mradi wa kutunza na kugawanya dawa hasa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, kwa kipindi cha miaka 10 kote nchini.

Mradi huo ambao pia umeisaidia Serikali kujenga maghala ya kuhifadhia dawa umefikika mwisho, hivyo USAID akiwa kama mchangiaji mkuu wa dawa, inaiacha ikiwa na pengo.

Hata hivyo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya amesema licha ya mradi huo kufikia ukomo na kuwa na msaada, wizara imejipanga kuhakikisha kuna uhakika wa upatikanaji wa dawa nchini.

Chanzo: Mwananchi
Porojo, serikli haiwezi kumudu kununua dawa za Ukimwi at market price! Sema tusubiri kufa kupukutika
 
Waandishi wetu naona wanakosa weledi wa kazi zao. Mwandishi wa Mwananchi Media ndio kaandika hiyo Habari je yeye chanzo chake ni nini? Nani kasema hivyo? USAID, USA ama nani? Source ya taarifa ya kwamba marekani itakata hiyo misaada ni nini?

Kichwa cha habari kinapotosha...lakini kama ni gazeti la Mwananchi sishangai kwani gani hili lina ajenda zake dhidi ya Tanzania
 
M
Waandishi wetu naona wanakosa weledi wa kazi zao. Mwandishi wa Mwananchi Media ndio kaandika hiyo Habari je yeye chanzo chake ni nini? Nani kasema hivyo? USAID, USA ama nani? Source ya taarifa ya kwamba marekani itakata hiyo misaada ni nini?
Magazeti yetu ni hovyo kabisa afadhali ukakesha JF utapata taarifa za uhakika ambazo wanachama huzijadili na kuzichambua.
Vichwa vya habari vya magazeti yetu ni umbeya umbeya tu.
 
Umeisoma hiyo habari kwa undani kutoka kwenye hilo gazeti?
Nimeisoma. Kuisha kwa muda wa mradi haina maana kwamba wamesitisha misaada. Uandishi wa namna hiyo ni kujaza wananchi mawazo potofu juu ya serikali. Kwamaana kwamba kama tulikosa fedha za MCC na sasa tunakosa dawa. Wakati kiuhalisia mpango huo wa dawa ungefikia ukomo hata kama suala la zanzbar na MCC lisingekuwepo
 
Porojo, serikli haiwezi kumudu kununua dawa za Ukimwi at market price! Sema tusubiri kufa kupukutika
Labda serikali itarudi kwa Madabida ili kuwapa wananchi zile dawa za unga wa muhogo na kusema ni ARV. Ni kama mzazi masikini anayempa mwanae mchuzi wa mchemsho wa magazeti na kumwambia ni supu ya kuku kumridhisha kupoza njaa
 
Sikia mladi wa afya marekan inasaidi nchi nying hapa kinachotokea n kutunyima kwa njia ya nyuma .... Tatizo ni zanzibar
Wacha uwongo na kuonesha ujinga wa dhahiri kwa kuchangia kitu ambacho hukijui.. hilo gazeti la mwananchi ukiachia ya kuwa lina agenda ya siri na Tz bali na huo muandishi na muhariri wake ni vihiyo.etleast angetoka akeenda kuwauliza wadau wanaosimamia huo mradi..Watu wa ukimwi wanajua fika ya kuwa mkataba unaisha tangu mitatu nyuma na inajulikana dhahiri ya kuwa USAID haitokuwepo tena na serikali ilianza kujipanga siku nyingi sana na ndiyo maana ikaanzisha fund za dawa za ukimwi na kuhusu Project ya MSD imeshakamilika kwa hivyo haja ya kuongeza mkatana kwa project iliyokamilika.

waambie wahariri wenu atleast wafanye homework kabla ya kupost habari
 
Naanza kumuelewa Maalim Seif, mdogo mdogo Shein ataomba poo mwenyewe ahamie ughaibuni, sie kina yakhe tuombe Mungu magonjwa yapite mbali tumeshindwa sukari tutaweza dawa kweli?! Mungu tusimamie.
 
Back
Top Bottom