Serikali iweke ofisi za Mkuu wa Wilaya pembeni ya Mji Mkongwe wa Mikindani, Mtwara

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,324
3,882
Wakuu,

Ni bandiko la pendekezo kwa serikali ya Tanzania kwamba kwa kuwa mji mkongwe wa Mikindani, Mtwara una historia ya kuvutia sana kwa vizazi vya sasa na vijavyo napendekeza makao makuu ya mkuu wa wilaya ya Mtwara yahamishiwe pembeni ya mji huo mkongwe ili kushamirisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi hivyo kuwezesha serikali kuwa na uhakika wa mapato yatokanayo na utalii, uvuvi, kiwanda cha Dangote lakini kupendezesha zaidi mandhari ukizingatia kuna uoto wa asili mzuri.
 
Ninaifahamu Mikindani, ni mji mkongwe kama Bagamoyo au Kilwa. Ila napingana na hoja yako.

Kama wananchi wa Mtwara/ Mikindani hawawezi kujiletea maendeleo hadi ofisi ya DC ijengwe Mikindani basi wananchi hao hawajitambui kwa nini wako hapo.

Nchi hii ina vitongoji vingi sina, je kila kitongoji kijengewe ofisi ya DC ndiyo kipate maendeleo? Jiheshimuni bana watu wa Mtwara
 
Nchi hii tuna ujinga huo,
Tunaamin maendeleo hata ya individual levels yanaletwa na serikali,
Watu wana mitaro michafu mtaani wanalalamika serikali, leo hii watu wanaomba ofisi za mkuu wa mkoa ili wapelekewe maendeleo, badala ya wao kupambana kukuza uchumi wao kwa style nyingine wao wanataka serikali
Ninaifahamu Mikindani, ni mji mkongwe kama Bagamoyo au Kilwa. Ila napingana na hoja yako.

Kama wananchi wa Mtwara/ Mikindani hawawezi kujiletea maendeleo hadi ofisi ya DC ijengwe Mikindani basi wananchi hao hawajaitambui kwa nini wako hapo.

Nchi hii ina vitongoji vingi sina, je kila kitongoji kijengewe ofisi ya DC ndiyo kipate maendeleo? Jiheshimuni bana watu wa Mtwara
 
Wakuu,

Ni bandiko la pendekezo kwa serikali ya Tanzania kwamba kwa kuwa mji mkongwe wa Mikindani, Mtwara una historia ya kuvutia sana kwa vizazi vya sasa na vijavyo napendekeza makao makuu ya mkuu wa wilaya ya Mtwara yahamishiwe pembeni ya mji huo mkongwe ili kushamirisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi hivyo kuwezesha serikali kuwa na uhakika wa mapato yatokanayo na utalii, uvuvi, kiwanda cha Dangote lakini kupendezesha zaidi mandhari ukizingatia kuna uoto wa asili mzuri.
Paendelee kubaki kwaajili ya utalii na sio utawala.
Dhana ya mji mkongwe ni pamoja na hizo nyumba za udongo zilizopo
 
Ninaifahamu Mikindani, ni mji mkongwe kama Bagamoyo au Kilwa. Ila napingana na hoja yako.

Kama wananchi wa Mtwara/ Mikindani hawawezi kujiletea maendeleo hadi ofisi ya DC ijengwe Mikindani basi wananchi hao hawajaitambui kwa nini wako hapo.

Nchi hii ina vitongoji vingi sina, je kila kitongoji kijengewe ofisi ya DC ndiyo kipate maendeleo? Jiheshimuni bana watu wa Mtwara
Kama umewahi kuishi au kukaa Mtwara kwa takribani wiki hadi miezi uneielewa hoja; wale jamaa zetu wana sifa moja mbaya sana kiburi, kujibagua na kijicho dhidi ya mtu anayefanya maendeleo eneo ambalo wako karibu. Ndio maana nikapendekeza ili kwenda nao mdogo mdogo hadi wajitambue ni sharti wageni kutoka mikoa mingine waende kuwekeza. Hali unayoiona Mtwara ndio utakumbana nayo Lindi. Ni afadhali Ruvuma wameanza kujitambua maana hata kijana akisoma akapata kazi hatimaye huenda kwenye asili yake kujenga tofauti na zamani.

Mikindani ni eneo liko chini ya serikali kwa hiyo kuna umuhimu wa kugatua mnyororo wa ushamirishaji miji.

Tazama soko jipya na la kisasa la Mtwara liitwalo CHUNO walilojengewa ili kuwezesha maendeleo yanasambazwa katika mji kwa kadri na mahitaji lakini mpaka leo ni wafanbiashara wachache mno wamehamia.

Kuna miji mingi mikongwe inayopaswa kushikwa mikono na serikali kwa makusudi mahususi
1. Mikindani Mtwara
2. Bagamoyo
3. Kilwa (masoko, Kivinje na kisiwani)
4. Mafia
5. Lindi
6. Kigoma Ujiji na Mwandiga
7. Magofu ya Tongoni Tanga
8. Mapango ya Amboni Tanga
9. Magofu ya Lushoto
10. Ngome Tabora
11. Kijiji cha Kayenze, Ilemela Mwanza
12. Eneo lote la Ngamiani Tanga
13. Kihesa na Kalenga, Iringa
14. Mapango ya wachagga, Kilimakyaro
15. Mapango ya Waluguru mlima Uluguru
16. Maziwa yanayohama usiku wa manane na kurejea sehemu zake alfajiri, Singida

Nk
 
Nchi hii tuna ujinga huo,
Tunaamin maendeleo hata ya individual levels yanaletwa na serikali,
Watu wana mitaro michafu mtaani wanalalamika serikali, leo hii watu wanaomba ofisi za mkuu wa mkoa ili wapelekewe maendeleo, badala ya wao kupambana kukuza uchumi wao kwa style nyingine wao wanataka serikali
Hawa Mtwara wakati wa msimu wa korosho ndiyo unakuta mtu amenunua chapati au bia halafu anampa mbuzi ili ale au anywe.
 
Back
Top Bottom