SoC04 Serikali iwe na jicho la tatu katika biashara ya uingizaji wa bidhaa toka nje ya Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kibubu4

Member
Jun 25, 2024
6
5
Nashukuru sana kupata nafasi ya kushiriki kwenye Stories of change.

Nimekuwa nikitoa maoni yangu kwenye mtandao wa X kwamba Serikali inaonaje kama ingeshusha ushuru wa kuagiza bidhaa toka nje ya Tanzania. Hapa namaanisha bidhaa kama magari, mashine na vifaa vyote vya kielectronic; bidhaa hizi kwa sasa zinahitajika sana kwenye masoko mbalimbali Afrika mashariki yote hata maeneo ya Zambia, Malawi na nchi nyingine zote za jirani.

Bidhaa hizi zikiingia nchini kwa unafaa mkubwa kwa waagizaji wa Tanzania itasaidia sana wafanya biashara wetu kupata wateja wengi kutoka nchi majirani, yaani tunaigeuza nchi yetu kuwa China ya Africa kwa maana kwamba majirani hawatawaza kuagiza bidhaa toka china watakuja kununulia hapahapa nchini kwetu; hii itaongeza thamani ya shilingi ya Kitanzania kwa kuwa nchi yetu itakuwa muuzaji mkubwa wa bidhaa.

1. Hivyo natamani serikali iangalie kushusha ushuru wa kuagiza bidhaa nje.

2. Serikali iwape wafanya biashara wetu mitaji mikubwa na nafuu ili waagize bidhaa nyingi zitakazouzwa kwa bei chee karibu na sawa na beinza kiwandani hapa Tanzania.

3. Tanzania ifungue mipaka kwa wanunuzi wa bidhaa kutoka nvhi zote jirani.

4. Serikali itoze kiasi cha ushuru kwa wanunuaji kutoka nje ya nchi yetu; hii itapandisha sana thamani ya shilingi yetu na uchumi wa Tanzania kwa ujumla.

Ninaamini kwamba muuzaji hupata fedha na mnunuaji hutoa pesa, sasa Tanzania ikijigeuza kama Sub market- kwa kuwa muuzaji kama wenye viwanda tutapata fedha nyingi toka kwa wakenya, Waganda, Rundi,Rwanda, Zambia malawi na ikiwa nafuu zaidi hata wakongo.

Tanzania tuna faida sana kuwa na bandari, tushindwe wenyewe. TRA isijikite kwenye kutegemea kupata mapato kupitia kupandisha kodi na tozo za kuingiza mizigo bandarini, inaweza ikashusha kodi na tozo kwa waagizaji wa Tanzania kwa asilimia hata tisini ili nchi ifaidike na fedha itakayopatikana kupitia mauzo na ushuru wa utakaotozwa baada ya mauzo.

Baadae nitakuja na stori kuhusu jambo lingine.
 
Back
Top Bottom