JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 925
- 1,546
Tanzania tuitakayo baada ya miaka mitatu
SERIKALI IWAUNGANISHIE WANANCHI UMEME BURE, WAKATWE KWENYE LUKU, KAYA MASIKINI TASAF IWEKE UTARATIBU WA KUWALIPIA
Gharama za kuunganishiwa Umeme ni Kubwa sana kwa mujibu wa Tovuti rasmi ya Tanesco imeweka gharama za kuunganishiwa umeme ni kama ifuatavyo Uunganisho wa Umeme Vijijini na mijini kwa umbali usiozidi Mita 30 na miundombinu ya karibu iliyopo ni TZS 27,000.
Uunganisho wa umeme mijini kwa umbali usiozidi Mita 30 na miundombinu ya karibu iliyopo ni TZS 320,960.00.
Wateja wa Vijijini wanaohitaji umeme ambapo Miundombinu iliyopo ya TANESCO ipo ndani ya mita 60 ni TZS 337,740.00
Wateja wa Mijini wanaohitaji umeme ambapo Miundombinu iliyopo TANESCO ipo ndani ya mita 60 ni TZS 515,618.00
Wateja wa Vijijini wanaohitaji umeme ambapo Miundombinu iliyopo ya TANESCO ipo ndani ya mita 90 ni TZS 454,654.00
Wateja wa Mjini wanaohitaji Umeme ambapo Miundombinu iliyopo TANESCO ipo ndani ya mita 90 ni TZS 696,670.00
Wananchi wengi wa Tanzania hawana uwezo wa Kumudu Gharama za Kujiunganishia umeme, Hususani ameneo ya Vijijini ambao hawajapitiwa na Mradi wa Umeme vijijini kupitia kwa WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)
Janury 17 2024 Kaimu Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Thomas Mmbaga alisema kuanzia vijiji Vijiji 758 kati ya Vijiji 12,315 vilivyopo nchi nzima;havijafikiwa na Mradi huo.
kwa mujibu wa Matokeo ya Utafiti wa Athari yaUpatikanaji wa Nishati Endelevu (IASES) 2021/22, yanaonesha kuwa takriban asilimia 46 yaka ya zimeunganishwa na umeme kwa Tanzania Bara.
Asilimia ya kaya zilizounganishwa na umeme ni kubwa zaidi katika maeneo ya mijinii kilinganishwa na maeneo ya vijijini.
Karibu kaya tisa kati ya kumi kwa mkoa wa Dares Salaam (87 asilimia) na kaya saba kati ya kumi katika maeneo mengine ya mijini (70asilimia) zimeunganishwa na umeme. Kwa upande mwingine, takriban kaya nne katiya kumi (36 asilimia) zimeunganishwa na umeme katika
Kwa mujibu wa Takwmu hizi zaidi ya kaya 54% hazijaunganishwa na huduma Hii muhimu ya Umeme.
Wananchi wengi wana hitaji umeme, kwa ajili ya matumizi ya nyumbani yale ya kibiashara lakini wanashindwa Kumudu gharama za kuunganishiwa Umeme.
Serikali inaweza Kuweka utaratibu mzuri unaofaa na usioumiza kwa kuwaunganishia wateja wote wanaohitaji Umeme kisha iweke utaratibu mzuri wa wateja wao kulipia gharama hizo kila Mwisho wa mwezi kwa kukata Moja moja Pindi anaponunua LUKU.
Kwa mapendekezo ninayopendekeza Kwa mjini wakatwe Angalau elfu kumi kila mwezi Kwa muda wa Miaka mitatu na Kijini elfu tano kila mwezi kwa muda wa Miaka mitatu au Pia kwa jinsi ambavyo Serikali itaona inafaa.
FAIDA ZA ZAKE NI
Hii itasaidia TANESCO kuwa na wateja wengi wanaotumia Umeme na hivyo Moja moja itaongeza mapato ya shirika hilo kwa sababu wateja watakuwa wakinunua umeme kwa wingi
Wananchi Kuongeza kipato kwa Kutumia fursa zinazotokana na Upatikanaji wa umeme.
Kufungua Fursa nyingi za kiuchumi Katika maeneo ya Vijijini
Faida nyingine ni Kwamba tunatambua Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya changamoto kuu zinazoisumbua dunia kwa sasa.
Ili kukabiliana na athari mabadiliko hayo ikiwemo ukame, mafuriko na ongezeko la joto, watalaam wa mazingira wanapendekeza matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia na mwanga hivyo upatikanaji wa umeme utapunguza matumizi ya Kuni na mkaa ,Bila kusahau pia itapunguza kwa kiwango kikubwa uharibifu wa mazingira kwa kukata miti hovyo.
Lakini pia itawafanya wananchi wanufaike moja kwa moja na uwekezaji unaofanywa na serikali katika utekelezaji wa miradi Mikubwa ya kimkakati iikiwemo wa Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) Unaotarajia kuzalisha zaidi ya Megawati 2115 za Umeme.
KWA WALE WANANCHI AMBAO HAWANA UWEZO KABISA AMBAO NI WANUFAIKA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI, AMBAO UNATOA RUZUKU KWA KAYA MASKIN;
Serikali inaweza hawa badala ya kuwapa fedha taslimu ikaweka utaratibu mzuri pia utakaowawezesha Kulipia gharama hizo kupitia uwezeshaji wa kifedha wanaotoa kila mwezi katika kaya Hizo ili kuboresha maisha yao.
Mpango huu uende sambamba na Kutoa Elimu kwa wananchi Juu ya Utunzanji wa Mazingira na ujenzi wa nyumba za kisasa za Kuishi pamoja na matumizi ya nishati safi kwa ajili ya kupata mwanga na Kupika.
Pia serikali inaweza kuangalia namna ya kushirikisha wadau wengine wa maendeleo Katika kutekeleza Hili suala ambalo litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi
Kwa kuanzia serikali kupitia wizara ya nishati inaweza kulichukua na kujadili namna utekelezaji wake unavyoweza kufanyika na mwaka Ujao wa fedha 2024/2025 serikali ikaja na mkakakati madhubuti
Mwisho wazo hili likuchukuliwa kwa uzito na kufanyiwa kazi kwa kipindi cha Miaka Mitano ijayo kuanzia 2025-2030 wananchi wote watakuwa wameunganishiwa huduma ya Umeme na KUongeza pia idaidi ya wananchi wanaotumia nishati safi Kupikia, lakini pia itaboresha makazi hasa maeneo ya vijijini.
MWANDISHI NI YOHANE GERVAS MASSAWE
EMAIL GERVASYOHANE@GMAIL.COM
TABATA DAR ES SALAAM