Serikali isiache kuhusishwa na Jaribio Dhidi ya Lissu; Ijisafishe!

Na. M. M. Mwanakijiji

Haijalishi nani amefanya, haijalishi nani amedhaniwa kufanya, na haijalishi nani anaweza kuwa amefanya. Kwamba, jambo hili limefanyika inatosha kabisa kuwafanya watu wote wenye kuheshimu utu wa mwanadamu kulaani kwa maneno yote yanayowezekana jaribio la kiwoga dhidi ya maisha ya Mbunge wa Singida Mashariki, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika na Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni Bw. Tundu Lissu.

Shambulio hilo la risasi zaidi ya ishirini kwa mtu ambaye hana silaha, na hana ulinzi wa kutosha ni wazi halikuwa la kumtishia tu bali lilikuwa na lengo la kuondoa uhai wake mchana kweupe na bila kujali matokeo yoyote kwa watakaofanya. Tukio hili limefanyika tayari kukiwa na hisia ya kuongezeka kwa vitendo vya mauaji yasiyoelezeka na matukio ambayo yanaashiria kuwepo kwa mfumo mwingine wa kiutawala nje ya ule uliowekwa kikatiba na kisheria.

Sote tunafahamu kuwa tukio hili kwanza si la peke yake na siyo la kwanza la aina yake nchini. Tayari yameshawahi kutokea matukio ya mauaji ya watu mashuhuri nchini ambapo wahusika wake hawajaweza kufahamika hadi hivi sasa na kubakia kuwa ni “watu wasiojulikana”. Wiki chache tu zilizopita mmoja wa wanaharakati wa vita dhidi ya ujangili ambaye ni raia wa Uingereza aliuawa Jijini Dar-es-Salaam na hadi sasa hakuna taarifa zinazoeleweka za uchunguzi ulipofikia.

Miaka saba nyuma Julai 2010 mwanasheria mwingine mashuhuri na msomi aliyebeboa Profesa Jusa Mwaikusa aliuawa jijini Dar-es-Salaam mchana kweupe vile vile. Wakati ule watu kadhaa walikamatwa wakitajwa kuhusika na tukio lile.

Miaka mitatu baadaye mwanasheria mwingine na wakili mashuhuri Dkt. Sengodo Mvungi naye alijeruhiwa katika jaribio la mauaji na baadaye kufariki huko Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa matibabu. Katika tukio lile watu wengine karibu kumi walimatwa na kufikishwa mahakamani.

Ni rahisi sana katika matukio ambapo wanasiasa au watu mashuhuri wanauawa au kujaribiwa kuuawa kuhisi moja kwa moja kuwa kwa namna fulani mkono wa serikali unahusika. Ni jambo la hatari na baya sana kwa serikali au vyombo vyake kudhaniwa kuwa vinaweza kutumia njia ya nje za kisheria (extra judicial) kushughulikia watu ambao inaona ni wana matatizo.

Binafsi, naamini – na tayari tumeona hili likitokea – serikali imekuwa ikitumia njia za kawaida za kisheria za kushughulika na changamoto na hoja za Tundu Lissu. Kwa baadhi yetu njia hizi tumeona si za lazima kwani kwa kiasi kikubwa hoja za Tundu Lissu zilikuwa zinaweza kujibiwa kisiasa na zimekuwa kujibiwa kisiasa. Na pale ambapo serikali imeona amevuka mpaka mara kadhaa wamekuwa wakimkamata na kumfungulia kesi. Inawezekana sasa hivi Lissu anashikilia rekodi ya kuwa Mtanzania mwenye kesi nyingi – za kushtakiwa na kusimamia kama wakili!

Ni kwa sababu hii wazo kuwa inawezekana kuna kuhusika kwa vyombo vya dola linatisha na linatulazimisha kutupa ukimya wa sekunde. Ni kwanini watu wanahisia hizo? Jibu kwa wengi ni kuwa tayari Lissu alishanyoshea mkono serikali na kudokeza kuwa anahisi anafuatiliwa na vyombo vya dola na alishatuhumu vyombo vya usalama kuwa kama kuna watu wametumwa kumfuatilia waache hivyo kwani tayari amewakaba. Vyombo vya dola havikusema maneno mengi ya kukanusha au hata kuonesha kuwa havihusiki; na inawezekana labda Lissu mwenyewe hakutoa taarifa polisi hasa kama inawezekana aliowadhania ni vyombo vya dola ni watu wengine wabaya.

Vyovyote vile ile ilivyo ni wajibu wa serikali kujisafisha na kuonesha kuwa katika nchi yetu sasa hivi hakuna sera ya mbwa kala mbwa! Siyo maslahi ya Rais Magufuli kuonekana kama Rais ambaye ameanza kushindwa hoja za maneno na sasa serikali yake inataka kuingia kwenye hoja za damu. Siyo sahihi kwa serikali na vyombo vyake ambavyo mara nyingi imedai kuwa na “intelligensia” inayokataza mikutano ya vyama vya upinzani lakini inakosa inteligensia ya kufuatilia watu ambao wana uwezo wa kumwaga risasi ishirini mchana kweupe na wakatokomea bila kufahamika.

Ninaamini, ni muhimu kwa serikali na vyombo vyake vyote kuhakikisha kuwa waliohusika na tukio hili wanafahamika na kukamatwa na kuhakikisha kuwa matukio kama haya hayazoeleki kwani tayari kuna hisia kwa baadhi ya watu kuwa tunaweza kuanza kuonekana kwa matukio ya namna hii.

Lakini vile vile ni wajibu wa vyama vya upinzani na hasa chama kikuu cha upinzani kuhakikisha kuwa kinatoa ulinzi kwa viongozi wake wakuu na hasa watu kama Lissu ambao tayari wameonekana kutishiwa maisha. Na hili linawezekana kwa viongozi hao kuwasiliana na Jeshi la polisi ili kutoa taarifa za kuwepo kwa ulinzi kwa viongozi wao, ulinzi ambao wa watu wenye silaha. Inasikitisha katika nchi ambayo tayari tuna harakati za kila namna viongozi wa namna hii hawapewi ulinzi wa watu wenye silaha. Na hata kama hakuna watu wenye silaha CHADEMA inapaswa kutoa ulinzi wa karibu kwa viongozi wake kuanzia sasa mara moja ili kuhakikisha inakuwa vigumu kwa mtu kupanga na hata kujaribu kutekeleza tendo ovu kama liliojaribiwa kwa Lissu.

Kama nilivyosema, haijalishi nani amefanya, haijalishi nani anadhaniwa kufanya kinachojali ni kuwa jambo hili limefanyika na linapaswa kulaaniwa kwa lugha yote kali. Lakini, ni muhimu sana kujua nani amefanya tukio hili ili kuhakikisha kuwa wananchi bila kujali nafasi zao hawaanzi kuishi kwa hofu hasa kwa vile tukio hili siyo la kwanza la aina yake.

Ni muhimu pia kwa wananchi kuwa na utulivu na hekima ya kutafakari kwa kujiuliza swali la msingi hasa – ni nani angenufaika kama Lissu angeuawa? Huu ndio msingi wa uchunguzi. Japo wengi tayari wameshahitimisha kuwa “serikali inahusika” au kuwa ni “Magufuli”; kuna uwezekano mkubwa kuwa ambaye/ambao wangenufaika na Lissu kuuawa bila ya shaka siyo Magufuli. Ni maslahi ya Magufuli kuona kuwa Lissu hapatwi na janga kama kama hili. Wengine wanaweza kusema “vipi kama Magufuli hajali kama angenufaika au la?” Swali hili ni zito na jibu lake siyo rahisi lakini linaweza kufikirisha wengi.

Ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa wahusika wanakamatwa mara moja ili isije kuonekana tukio hili ama lina mkono, baraka au maelekezo kutoka ndani ya serikali. Lakini kama jambo hili lina uratibu wowote kutoka kwa mtu yeyote (ndani ya serikali au nje yake), basi mtu huyo awe pia na ujasiri wa kusimama hadharani na kusema kuwa aliagiza kufanyika kwa tukio hilo na hana majuto.

Tunamtakia na kumwombea uponyaji wa haraka Bw. Lissu ili arejee katika majukumu yake ya kulijenga taifa na kusimamia maslahi ya taifa.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Mkuu wala hilo halina mjadala,waliohusika ni selikari na hata walipokuwa wanapokea hayo mataarifa yao leo rais ,spika,waziri wa mambo ya ndani na timu yao ikiratibiwa na makonda wote walijua kuwa leo lisu anapotea,kwani ukifuatilia hotuba ya mtakatifu na tukio zima la lisu radhma wenye akili watajua muhusika ni nani kama anaweza sema ktk vita hii ikiwezekana hata sheria yaweza vunjwa nini maana yake ni kweli kuvunjwa kwake imeanzia kwa lisu,lkn pia niseme kitu kimoja wapinzani wanashida sana kama wanwzani wanaweza kupata huruma kupitia serikali hii ambayo haiwahitaji kuanzia mkuu wao ni kama wanapoteza muda kilichopo kama kweli wamejitoa kuwa wapinzani wawe na akili ya ziada,na wanatakiwa kuwa wakweli na wauseme huo ukweli Antpasi kwa shambulio hili serikali imehusika wala hakuna luga ingine kikubwa kama kweli nyie ni wapinzani jipangeni vinginevyo mtamung'unya maneno lkn mwisho wake nanyi mtaingia kwenye 18 zao ni hrli kusrma kupambana dunia nzima ijue,mwenyekt mboe jipange kama unazani ww uko salama kwa kutokusema ukweli umepotea ieleze serikali kuwa imehusika hakuna zaidi na kama unahofu basi wako wenye moyo huo ww jiondoe hapa bila kugangamala hakuna mtakachoweza zaidi ya kuteswa na kuuwawa serikali hii c njema kwenu lkn serikali hii ndo inaweza kuwafanya kuwa washindi ,acheni kulalamika bal8 pambaneni nyinyi ni watoto yatima hapapo pa kupeleka shida zenu ila kwenu wenyewe ,MUNGU amponye msema kweli pekee MH Tundu lisu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais kama taasisi ilimwagiza Mh. Spika awashughurikie Bungeni na wakija nje nae atawashughurikia..
Mwigulu nae akasema itakuaje nao wakianza kuwashughurikia maana KIBITI walikua wanaouwawa ni wanaccm na viongozi
SHAKA uvccm alisema Hivi...Lissu anajifanya muongeaji ngoja aje akutanishwe na mauti..
Mimi kama mtanzania na Mzalendo naomba ufafanuzi juu ya hizi kauli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hili hata iweje sidhani kama serikali inaweza kujisafisha na ikaaminika kwa wananchi.

Mbaya zaidi ni kwamba kiongozi mwenyewe wa serikali, yaani rais Magufuli, ndiye yuko mstari wa mbele kuwafanya watu wasiiamini serikali yake kwa sababu ya nyingi ya kauli zake.

Laiti angekuwa yupo makini na maneno atumiayo labda walau kungewepo na nafasi ya kuaminiwa.

Lakini kwa sasa sidhani. Labda ambacho wanaweza kufanya ni kupunguza makali ya tuhuma hizo za kuhisiwa.

Ushahidi wa kimazingira dhidi ya uhusika wa serikali ni mwingi wa kutosha.

NB: Ni Jusa Mwaikusa au ni Jwani Mwaikusa..???

KAMA nchi tutakuwa na wakati mgumu sn ktk utawala wa huyu mzee
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Haijalishi nani amefanya, haijalishi nani amedhaniwa kufanya, na haijalishi nani anaweza kuwa amefanya. Kwamba, jambo hili limefanyika inatosha kabisa kuwafanya watu wote wenye kuheshimu utu wa mwanadamu kulaani kwa maneno yote yanayowezekana jaribio la kiwoga dhidi ya maisha ya Mbunge wa Singida Mashariki, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika na Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni Bw. Tundu Lissu.

Shambulio hilo la risasi zaidi ya ishirini kwa mtu ambaye hana silaha, na hana ulinzi wa kutosha ni wazi halikuwa la kumtishia tu bali lilikuwa na lengo la kuondoa uhai wake mchana kweupe na bila kujali matokeo yoyote kwa watakaofanya. Tukio hili limefanyika tayari kukiwa na hisia ya kuongezeka kwa vitendo vya mauaji yasiyoelezeka na matukio ambayo yanaashiria kuwepo kwa mfumo mwingine wa kiutawala nje ya ule uliowekwa kikatiba na kisheria.

Sote tunafahamu kuwa tukio hili kwanza si la peke yake na siyo la kwanza la aina yake nchini. Tayari yameshawahi kutokea matukio ya mauaji ya watu mashuhuri nchini ambapo wahusika wake hawajaweza kufahamika hadi hivi sasa na kubakia kuwa ni “watu wasiojulikana”. Wiki chache tu zilizopita mmoja wa wanaharakati wa vita dhidi ya ujangili ambaye ni raia wa Uingereza aliuawa Jijini Dar-es-Salaam na hadi sasa hakuna taarifa zinazoeleweka za uchunguzi ulipofikia.

Miaka saba nyuma Julai 2010 mwanasheria mwingine mashuhuri na msomi aliyebeboa Profesa Jusa Mwaikusa aliuawa jijini Dar-es-Salaam mchana kweupe vile vile. Wakati ule watu kadhaa walikamatwa wakitajwa kuhusika na tukio lile.

Miaka mitatu baadaye mwanasheria mwingine na wakili mashuhuri Dkt. Sengodo Mvungi naye alijeruhiwa katika jaribio la mauaji na baadaye kufariki huko Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa matibabu. Katika tukio lile watu wengine karibu kumi walimatwa na kufikishwa mahakamani.

Ni rahisi sana katika matukio ambapo wanasiasa au watu mashuhuri wanauawa au kujaribiwa kuuawa kuhisi moja kwa moja kuwa kwa namna fulani mkono wa serikali unahusika. Ni jambo la hatari na baya sana kwa serikali au vyombo vyake kudhaniwa kuwa vinaweza kutumia njia ya nje za kisheria (extra judicial) kushughulikia watu ambao inaona ni wana matatizo.

Binafsi, naamini – na tayari tumeona hili likitokea – serikali imekuwa ikitumia njia za kawaida za kisheria za kushughulika na changamoto na hoja za Tundu Lissu. Kwa baadhi yetu njia hizi tumeona si za lazima kwani kwa kiasi kikubwa hoja za Tundu Lissu zilikuwa zinaweza kujibiwa kisiasa na zimekuwa kujibiwa kisiasa. Na pale ambapo serikali imeona amevuka mpaka mara kadhaa wamekuwa wakimkamata na kumfungulia kesi. Inawezekana sasa hivi Lissu anashikilia rekodi ya kuwa Mtanzania mwenye kesi nyingi – za kushtakiwa na kusimamia kama wakili!

Ni kwa sababu hii wazo kuwa inawezekana kuna kuhusika kwa vyombo vya dola linatisha na linatulazimisha kutupa ukimya wa sekunde. Ni kwanini watu wanahisia hizo? Jibu kwa wengi ni kuwa tayari Lissu alishanyoshea mkono serikali na kudokeza kuwa anahisi anafuatiliwa na vyombo vya dola na alishatuhumu vyombo vya usalama kuwa kama kuna watu wametumwa kumfuatilia waache hivyo kwani tayari amewakaba. Vyombo vya dola havikusema maneno mengi ya kukanusha au hata kuonesha kuwa havihusiki; na inawezekana labda Lissu mwenyewe hakutoa taarifa polisi hasa kama inawezekana aliowadhania ni vyombo vya dola ni watu wengine wabaya.

Vyovyote vile ile ilivyo ni wajibu wa serikali kujisafisha na kuonesha kuwa katika nchi yetu sasa hivi hakuna sera ya mbwa kala mbwa! Siyo maslahi ya Rais Magufuli kuonekana kama Rais ambaye ameanza kushindwa hoja za maneno na sasa serikali yake inataka kuingia kwenye hoja za damu. Siyo sahihi kwa serikali na vyombo vyake ambavyo mara nyingi imedai kuwa na “intelligensia” inayokataza mikutano ya vyama vya upinzani lakini inakosa inteligensia ya kufuatilia watu ambao wana uwezo wa kumwaga risasi ishirini mchana kweupe na wakatokomea bila kufahamika.

Ninaamini, ni muhimu kwa serikali na vyombo vyake vyote kuhakikisha kuwa waliohusika na tukio hili wanafahamika na kukamatwa na kuhakikisha kuwa matukio kama haya hayazoeleki kwani tayari kuna hisia kwa baadhi ya watu kuwa tunaweza kuanza kuonekana kwa matukio ya namna hii.

Lakini vile vile ni wajibu wa vyama vya upinzani na hasa chama kikuu cha upinzani kuhakikisha kuwa kinatoa ulinzi kwa viongozi wake wakuu na hasa watu kama Lissu ambao tayari wameonekana kutishiwa maisha. Na hili linawezekana kwa viongozi hao kuwasiliana na Jeshi la polisi ili kutoa taarifa za kuwepo kwa ulinzi kwa viongozi wao, ulinzi ambao wa watu wenye silaha. Inasikitisha katika nchi ambayo tayari tuna harakati za kila namna viongozi wa namna hii hawapewi ulinzi wa watu wenye silaha. Na hata kama hakuna watu wenye silaha CHADEMA inapaswa kutoa ulinzi wa karibu kwa viongozi wake kuanzia sasa mara moja ili kuhakikisha inakuwa vigumu kwa mtu kupanga na hata kujaribu kutekeleza tendo ovu kama liliojaribiwa kwa Lissu.

Kama nilivyosema, haijalishi nani amefanya, haijalishi nani anadhaniwa kufanya kinachojali ni kuwa jambo hili limefanyika na linapaswa kulaaniwa kwa lugha yote kali. Lakini, ni muhimu sana kujua nani amefanya tukio hili ili kuhakikisha kuwa wananchi bila kujali nafasi zao hawaanzi kuishi kwa hofu hasa kwa vile tukio hili siyo la kwanza la aina yake.

Ni muhimu pia kwa wananchi kuwa na utulivu na hekima ya kutafakari kwa kujiuliza swali la msingi hasa – ni nani angenufaika kama Lissu angeuawa? Huu ndio msingi wa uchunguzi. Japo wengi tayari wameshahitimisha kuwa “serikali inahusika” au kuwa ni “Magufuli”; kuna uwezekano mkubwa kuwa ambaye/ambao wangenufaika na Lissu kuuawa bila ya shaka siyo Magufuli. Ni maslahi ya Magufuli kuona kuwa Lissu hapatwi na janga kama kama hili. Wengine wanaweza kusema “vipi kama Magufuli hajali kama angenufaika au la?” Swali hili ni zito na jibu lake siyo rahisi lakini linaweza kufikirisha wengi.

Ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa wahusika wanakamatwa mara moja ili isije kuonekana tukio hili ama lina mkono, baraka au maelekezo kutoka ndani ya serikali. Lakini kama jambo hili lina uratibu wowote kutoka kwa mtu yeyote (ndani ya serikali au nje yake), basi mtu huyo awe pia na ujasiri wa kusimama hadharani na kusema kuwa aliagiza kufanyika kwa tukio hilo na hana majuto.

Tunamtakia na kumwombea uponyaji wa haraka Bw. Lissu ili arejee katika majukumu yake ya kulijenga taifa na kusimamia maslahi ya taifa.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Muuaji anajulikana kwa watu wenye akili huru, anatoka katika mhimili uliojichimbia chini zaidi mingine. Jiulize yuko wapli Ben sanane, umetoka wapi mtindo wa kuua na kufunga maiti kwenye viroba zinazoopolewa kila siku nk.
 
Kupotea kwa Ben Saanane,kutishiwa kwa bastola @Nape Nauye, Kuokotwa kwa maiti kwenye viroba pwani ya dar es salaam. Haya yote ni matokea ya kauli za sizonje
 
Vyombo vya ulinzi. Saa nyingine ni bora kuvunja sheria kwa maslahi ya nchi,
 
Tusiume maneno. Sizyonjwe anahusika moja kwa moja kwenye mauaji haya! Ni jana tu akipokea ripoti za madini alisema ni bora kuvunja sheria ili kuokoa maslahi ya watanzania. Na amenukuliwa mara kadhaa skisema Tundu Lissu ni adui wa maslahi ya nchi. Anyway, Mungu yupo na yeyote aliye husika na uovu huu ukamrudie yeye kwa jina la Yesu
 
Kwenye hili hata iweje sidhani kama serikali inaweza kujisafisha na ikaaminika kwa wananchi.

Mbaya zaidi ni kwamba kiongozi mwenyewe wa serikali, yaani rais Magufuli, ndiye yuko mstari wa mbele kuwafanya watu wasiiamini serikali yake kwa sababu ya nyingi ya kauli zake.

Laiti angekuwa yupo makini na maneno atumiayo labda walau kungewepo na nafasi ya kuaminiwa.

Lakini kwa sasa sidhani. Labda ambacho wanaweza kufanya ni kupunguza makali ya tuhuma hizo za kuhisiwa.

Ushahidi wa kimazingira dhidi ya uhusika wa serikali ni mwingi wa kutosha.

NB: Ni Jusa Mwaikusa au ni Jwani Mwaikusa..???
Ngabu busara zimekosekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Style ya serikali ya awamu ya tano.

1. Kuwakamata wapinzani na kuwapeleka mahabusu na baadae kuwapeleka mahakamani

Kutuma wauaji sio style ya serikali hii.
Kwenye ukweli tuongee ukweli na tujitenge mbali na hisia hasi.
 
Kwenye hili hata iweje sidhani kama serikali inaweza kujisafisha na ikaaminika kwa wananchi.

Mbaya zaidi ni kwamba kiongozi mwenyewe wa serikali, yaani rais Magufuli, ndiye yuko mstari wa mbele kuwafanya watu wasiiamini serikali yake kwa sababu ya nyingi ya kauli zake.

Laiti angekuwa yupo makini na maneno atumiayo labda walau kungewepo na nafasi ya kuaminiwa.

Lakini kwa sasa sidhani. Labda ambacho wanaweza kufanya ni kupunguza makali ya tuhuma hizo za kuhisiwa.

Ushahidi wa kimazingira dhidi ya uhusika wa serikali ni mwingi wa kutosha.

NB: Ni Jusa Mwaikusa au ni Jwani Mwaikusa..???
Duh! Watu mnafikirisha sana
 
NN tuamaini kwamba kauli za raisi zinawaza mzima watu kutenda unataka huku wakija wazi kwamba kauli hizo zitatumika kama chanzo na hivyo kuwa poteza ushahidi?
Kwenye hili hata iweje sidhani kama serikali inaweza kujisafisha na ikaaminika kwa wananchi.

Mbaya zaidi ni kwamba kiongozi mwenyewe wa serikali, yaani rais Magufuli, ndiye yuko mstari wa mbele kuwafanya watu wasiiamini serikali yake kwa sababu ya nyingi ya kauli zake.

Laiti angekuwa yupo makini na maneno atumiayo labda walau kungewepo na nafasi ya kuaminiwa.

Lakini kwa sasa sidhani. Labda ambacho wanaweza kufanya ni kupunguza makali ya tuhuma hizo za kuhisiwa.

Ushahidi wa kimazingira dhidi ya uhusika wa serikali ni mwingi wa kutosha.

NB: Ni Jusa Mwaikusa au ni Jwani Mwaikusa..???
NN je wataka kutuambia kuwa kauli za mheshimiwa rais kuna watu zinawapa mzuka kiasi kwamba wanajificha chini yake huku wakijua kwamba ni ngumu wao kujulikana manake suspect wa kwanza sio wao?
 
Back
Top Bottom