Serikali inaweza kuanisha hasara kwa magari ya Bagamoyo kuingia Tegeta? Huu mgomo mpaka lini?

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
2,209
4,769
Serikali na ama mamlaka husika, inapokosa mwelekeo thabiti na kutoa maelekezo kwa muda sahihi na mwafaka! Inasababisha tafrani na hasira kwa wananchi

Kutokea Juzi 17 September mpaka hii leo, hakuna mwafaka juu ya mgomo wa daladala za Bagamoyo to Dar!

Maana yake nini?

Je, Serikali imebaini hasara gani mabasi ya bagamoyo kuwa yanashushia Tegeta na badala yake wanasema yaishie Bunju?

Mbunge wa bagamoyo, hasemi chochote, wala kiongozi yeyote hajitokezi kusema juu ya hili

Matokeo yake limekuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa Bagamoyo

Walianza kutimliwa Kule Makumbusho na sasa tegeta, au mpango ni magari ya mkoa wa Pwani yaishie Pwani pekee na ya Dar yawe Dar?

Hovyo sana kuwa na wabunge ambao ni mabubu na hawasaidii kutatua migogoro kama hii kwa wananchi

Hizi nafasi za kupeana shida zake ndo hizi, kiongozi hana uchungu na wananchi wake anaowaongoza,
 
Hovyo sana kuwa na wabunge ambao ni mabubu na hawasaidii kutatua migogoro kama hii kwa wananchi

Hizi nafasi za kupeana shida zake ndo hizi, kiongozi hana uchungu na wananchi wake anaowaongoza,
Dah huyo mbunge ni majanga sana, hana tofauti na kawambwa. Ni watu ambao wanaongoza majimbo kwasababu ya ujinga wa raia tu huko.

Alafu unawahamishaje watu kwenye stendi mbovu kama ile ya bunju sokoni. Stendi kama uwanja wa fisi.
 
Tatizo liko kwa Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima siyo mbunge wa Bagamoyo

Stendi inatakiwa ihame kutoka Tegeta Nyuki iende Bunju sokoni ambako miundombinu siyo rafiki

Tegeta Nyuki kujengwa Soko la kimataifa na DP World 😂
 
Back
Top Bottom