DOKEZO Serikali inasema Kipindupindu Simiyu ni ukosefu wa Vyoo lakini kuna sababu kubwa nyuma ya pazia

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
67
129
Wananchi wakichota maji katikati ya mito hiyo, wengine wakiwa wamejitwisha ndoo tayari kupeleka maji ya kutumia majumbani kwao.
Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu katika Mkoa wa Simiyu, umeendelea kushika kasi, eneo la Wilaya ya Meatu ndilo limeathirika na linaendelea kuathirika zaidi.

Jimbo la Kisesa katika Wilaya hiyo ndilo hatari zaidi kwa sasa, ukienda katika Kata za Mwandoya, Kisesa, Mbugayabanya, Sakasaka, pia Vijiji vyote vya jimbo hilo, mfano Mwakisandu, Mbalagane, Mwandu, maeneo yote hayo kwa sasa ni hatari.

Kuna idadi kubwa ya wagonjwa kutoka katika Vijiji hivyo wanaletwa kwenye kambi takribani mbili zilizotengwa na
Serikali kwa ajili ya Wagonjwa wa Kipindupindu.

Nilibahatika kukaa kwenye kambi mojawapo, kwa siku moja, nilishuhudia wagonjwa wapatao watano wakifikishwa kwenye kambi hiyo, wengi wakitoka kwenye vijiji hivyo.

Takribani mwezi mmoja sasa, nimefanya uchunguzi kutaka kujua nini chanzo cha ugonjwa huu kukita mizizi? Idadi ya wagonjwa kuongezeka? Kwa nini ugonjwa huu nyakati hizi za kiangazi? Na hiki ndicho nilibaini.

Wakati Serikali ya mkoa na Wilaya kupitia viongozi wake wakisema chanzo cha ugonjwa huu ni idadi kubwa ya wananchi wa Wilaya hiyo kutokuwa na vyoo, na wananchi kuwalazimu kujisaidia vichani.

Ni kweli hata uchunguzi wangu ulibaini kaya nyingi katika Wilaya hiyo hazina vyoo, ni Mkoa ya pili kutoka Mwisho
Tanzania wananchi wake hawana vyoo kwa mujibu wa takwimu za NBS.

Niliongea na wananchi wengi juu ya sababu hizo za serikali, wao wanasema sababu kubwa ni maeneo yao kukosa maji safi na salama.

Serikali na Wananchi kila mmoja analaumu mwenzake Nilianza kufanyia kazi sababu zote mbili, ambapo Serikali
inatupa mpira kwa Wananchi na wananchi wanaitupia lawama Serikali.

Changamoto ya maji safi na salama.
Wilaya ya Meatu ina changamoto kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama, maeneo mengi Wananchi wanatumia maji ambayo siyo safi wala salama.

Wilaya hiyo imezungukwa na idadi kubwa ya mito mikubwa na midogo, mito ambayo haitiririshi maji wakati wote, bali imekuwa ikihifadhi maji kwenye mchanga.

Uwepo wa mito hiyo na uwezo wake wa kuhifadhi maji, kimekuwa chanzo kikubwa cha Wananchi wa Wilaya hiyo
kujipatia maji ambayo utumia kwa ajili ya kupikia, kunywa, kufulia, shughuli za kilimo cha umwagiliaji pamoja na
kunyweshea mifugo.

Katikati ya hiyo mito Wananchi uchimba mashimo madogo, kisha uchota maji yake ambayo wanayatumia kwa shughuli zote hizo.

Wananchi wakichota maji katikati ya mto, ambapo wamechimba shimo kisha wanachota maji, ambapo wanatumia kupikia, na kunywa, ni katika Wilaya ya Meatu, Simiyu.

Jambo moja la kushangaza ni kwamba kwenye hiyo mito, wananchi wenyewe wamejiwekea sheria na utaratibu, mito hiyo wameitenga katika sehemu kuu tatu.

Sehemu ya kwanza imetengwa kwa ajili ya kuchimba mashimo ya kuchota maji ya kula, kunywa na kupikia, sehemu ya pili kwa ajili ya kufulia, na sehemu ya tatu ni kwa ajili ya mifugo kunywa maji.

Maeneo hayo licha ya kutengwa, yapo kwenye eneo moja la moja la mto, ambapo maji yanaweza kutiririka kutoka eneo moja kwenye eneo jingine hasa mvua ikinyesha.

Aidha, maeneo mengine wananchi wametumia mito hiyo kuchimba visima ambavyo vipo pembezoni mwa mito yenyewe, visima hivyo ni vifupi na vimewekewa pampu za kusukuma.

Visima hivyo vimechimbwa kwa nguvu za Wananchi wenyewe, na kuweka pampu hizo kwa nguvu zao wenyewe, na uchota maji hayo bure kwa ajili ya matumizi yote.

Kila siku asubuhi mito hiyo inajaa wananchi, baadhi wakichota maji ya matumizi, wengine wakifua na wengine wakinywesha mifugo yao.

Chanzo ni vyanzo vya maji kuchafuliwa
Eneo kubwa ambalo katika uchunguzi wangu nimebaini ni kuwa, mito hiyo kwa sasa imechafuka kwa kiwango kikubwa, na waliochafua ni wale ambao wanafua nguo na wanatumia mito hiyo kuoga na kujisaidia.

Nilishuhudia baadhi ya Wanawake wakifua nguo za watoto zenye vinyesi, pia baadhi wakioga katikati ya mito hiyo na kujisaidia, uwepo wa shughuli hizo ndizo chanzo kikubwa cha mito hiyo kuwa michafu.

Mwanamke akiwa amebeba mtoto, ameacha ndoo, na baadhi ya nguo ambazo alikuwa anafua, kisha kusogea hatua chache ndani ya mto kwa ajili ya kufua nguo za mtoto wake zenye kinyesi.
Mwananchi amemaliza kufua nguo hizo za mtoto na amerudi kwenye nguo na ndoo yake kwa ajili ya kuendelea kufua nguo nyingine. Shughuli zote hizo zinafanyika katika mto mmoja.
Mama mmoja nilimshuhudia alikuwa anafua nguo za mtoto wake, ambazo zilikuwa na kinyesi akizifulia katikati ya mto, lakini eneo jingine nikakuta wananchi wakitumia mto huohuo kuoga na kujisaidia.

Uchafu huo sasa umesambaa mito mzima baada ya mvua kunyesha, na kama ambavyo tunajua mito ya Wilaya hiyo ni mrefu kila kijiji ambacho unapita wanachi wake wanautumia kama chanzo chao kikuu cha maji.

Mvua ambazo zimenyesha mwaka huu, zimesababisha kusambaza uchafu huo kwenye maeneo yote ya mito hiyo, wakati wananchi wanaitumia kama chanzo chao kikuu cha maji, hivyo wanakula uchafu na ndiyo maana wanapata kipindupindu, kwa sababu hawana mbadala wa chanzo kingine cha maji.

Mwananchi mmoja anasema “Serikali inasema hatuna vyoo, tunajisaidia vichani, ni kweli wengi hatuna vyoo, lakini sababu kubwa ni matumizi ya maji ambayo siyo safi na salama, Wilaya, wengi tunatumia maji ya mito ambayo kwa sasa yamekuwa machafu, vinyesi vimesambaa sana,"

.....Watu wanafulia nguo za watoto zenye vinyesi, wanaoga humo na kujisaidia humo, sasa vinyesi hivyo vimesambaa mto mzima, na wakati huo wananchi wanategemea sana hiyo mito, hivyo ni lazima tutapa ugonjwa huu maana wengi hatuchemshi maji yake..........

Wanaokula kwenye shughuli ni majanga
Wananchi wengine wanasema kuwa ndugu zao wamepata maambukizi pindi walipokula chakula msibani au kunywa pombe za kienyeji, shughuli ambazo asilimia 90 zinatumia maji ya kwenye hiyo mito.

Visima vifupi ambavyo wananchi wamechimba pembezoni mwa hiyo mito, navyo ni hatari kwani maji yake yanatoka kwenye hiyohiyo mito.

Visima haviwekewi dawa, Takribani visima 10 ambavyo nilitembelea wananchi waliniambia haviwekewi dawa, ni visima vingine viwili tu ambavyo wananchi walisema dawa ziliwekwa kama miezi miwili imepita na mpaka sasa hazijawekwa nyingine.
4.jpg

Kwenye baadhi ya vijiji ambavyo vina miradi ya maji, ambayo ipo chini ya Wakala wa Maji na usafi wa mazingira mjini na vijijini (RUWASA) hata hivyo jambo la kushangaza wananchi wengi hawatumii hayo maji kutokana na uchumi wao kuwa duni, wanaona bora watumie ya kwenye mito au kisima maana ni bure.

Wengi ambao niliwauliza, wanasema hawana uwezo wa kununua ndoo moja Sh. 50, wanaona ni bora wakachote maji ya bure mtoni kuliko kununua, lakini sehemu nyingine huduma za maji safi na salama hazijafika na ndiko wanatumia zaidi maji ya mito na ndiko mlipuko umetokea kwa wingi

Mito yote ndani ya Wilaya hiyo imejaa vinyesi, imejaa vimelea vya kipindupindu, lakini bado kuna idadi kubwa ya wananchi wanaendelea kutumia maji ya kwenye hiyo mito na wengi hawachemshi hayo maji.

Serikali imeendelea kujificha kwenye suala la vyoo lakini tatizo kubwa ni idadi kubwa ya wananchi kuendelea kutumia maji ya mito hiyo kutokana ukosefu wa huduma ya kutosha ya maji safi na salama.

Chanzo cha Kipindupindi katika Mkoa wa Simiyu hasa Wilaya ya Meatu kama eneo ambalo limeathirika zaidi, ni ukosefu wa huduma za maji safi na salama katika maeneo mengi ya vijiji vya Wilaya hiyo.
 
View attachment 3133799

Mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu katika Mkoa wa Simiyu, umeendelea kushika kasi, eneo la Wilaya ya Meatu ndilo limeathirika na linaendelea kuathirika zaidi.

Jimbo la Kisesa katika Wilaya hiyo ndilo hatari zaidi kwa sasa, ukienda katika Kata za Mwandoya, Kisesa, Mbugayabanya, Sakasaka, pia Vijiji vyote vya jimbo hilo, mfano Mwakisandu, Mbalagane, Mwandu, maeneo yote hayo kwa sasa ni hatari.

Kuna idadi kubwa ya wagonjwa kutoka katika Vijiji hivyo wanaletwa kwenye kambi takribani mbili zilizotengwa na
Serikali kwa ajili ya Wagonjwa wa Kipindupindu.

Nilibahatika kukaa kwenye kambi mojawapo, kwa siku moja, nilishuhudia wagonjwa wapatao watano wakifikishwa kwenye kambi hiyo, wengi wakitoka kwenye vijiji hivyo.

Takribani mwezi mmoja sasa, nimefanya uchunguzi kutaka kujua nini chanzo cha ugonjwa huu kukita mizizi? Idadi ya wagonjwa kuongezeka? Kwa nini ugonjwa huu nyakati hizi za kiangazi? Na hiki ndicho nilibaini.

Wakati Serikali ya mkoa na Wilaya kupitia viongozi wake wakisema chanzo cha ugonjwa huu ni idadi kubwa ya wananchi wa Wilaya hiyo kutokuwa na vyoo, na wananchi kuwalazimu kujisaidia vichani.

Ni kweli hata uchunguzi wangu ulibaini kaya nyingi katika Wilaya hiyo hazina vyoo, ni Mkoa ya pili kutoka Mwisho
Tanzania wananchi wake hawana vyoo kwa mujibu wa takwimu za NBS.

Niliongea na wananchi wengi juu ya sababu hizo za serikali, wao wanasema sababu kubwa ni maeneo yao kukosa maji safi na salama.

Serikali na Wananchi kila mmoja analaumu mwenzake Nilianza kufanyia kazi sababu zote mbili, ambapo Serikali
inatupa mpira kwa Wananchi na wananchi wanaitupia lawama Serikali.

Changamoto ya maji safi na salama.

Wilaya ya Meatu ina changamoto kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama, maeneo mengi Wananchi wanatumia maji ambayo siyo safi wala salama.

Wilaya hiyo imezungukwa na idadi kubwa ya mito mikubwa na midogo, mito ambayo haitiririshi maji wakati wote, bali imekuwa ikihifadhi maji kwenye mchanga.

Uwepo wa mito hiyo na uwezo wake wa kuhifadhi maji, kimekuwa chanzo kikubwa cha Wananchi wa Wilaya hiyo
kujipatia maji ambayo utumia kwa ajili ya kupikia, kunywa, kufulia, shughuli za kilimo cha umwagiliaji pamoja na
kunyweshea mifugo.

Katikati ya hiyo mito Wananchi uchimba mashimo madogo, kisha uchota maji yake ambayo wanayatumia kwa shughuli zote hizo.

View attachment 3133801

Jambo moja la kushangaza ni kwamba kwenye hiyo mito, wananchi wenyewe wamejiwekea sheria na utaratibu, mito hiyo wameitenga katika sehemu kuu tatu.

Sehemu ya kwanza imetengwa kwa ajili ya kuchimba mashimo ya kuchota maji ya kula, kunywa na kupikia, sehemu ya pili kwa ajili ya kufulia, na sehemu ya tatu ni kwa ajili ya mifugo kunywa maji.

Maeneo hayo licha ya kutengwa, yapo kwenye eneo moja la moja la mto, ambapo maji yanaweza kutiririka kutoka eneo moja kwenye eneo jingine hasa mvua ikinyesha.

Aidha, maeneo mengine wananchi wametumia mito hiyo kuchimba visima ambavyo vipo pembezoni mwa mito yenyewe, visima hivyo ni vifupi na vimewekewa pampu za kusukuma.

Visima hivyo vimechimbwa kwa nguvu za Wananchi wenyewe, na kuweka pampu hizo kwa nguvu zao wenyewe, na uchota maji hayo bure kwa ajili ya matumizi yote.

Kila siku asubuhi mito hiyo inajaa wananchi, baadhi wakichota maji ya matumizi, wengine wakifua na wengine wakinywesha mifugo yao.

Chanzo ni vyanzo vya maji kuchafuliwa

Eneo kubwa ambalo katika uchunguzi wangu nimebaini ni kuwa, mito hiyo kwa sasa imechafuka kwa kiwango kikubwa, na waliochafua ni wale ambao wanafua nguo na wanatumia mito hiyo kuoga na kujisaidia.

Nilishuhudia baadhi ya Wanawake wakifua nguo za watoto zenye vinyesi, pia baadhi wakioga katikati ya mito hiyo na kujisaidia, uwepo wa shughuli hizo ndizo chanzo kikubwa cha mito hiyo kuwa michafu.

View attachment 3133802View attachment 3133803

Mama mmoja nilimshuhudia alikuwa anafua nguo za mtoto wake, ambazo zilikuwa na kinyesi akizifulia katikati ya mto, lakini eneo jingine nikakuta wananchi wakitumia mto huohuo kuoga na kujisaidia.

Uchafu huo sasa umesambaa mito mzima baada ya mvua kunyesha, na kama ambavyo tunajua mito ya Wilaya hiyo ni mrefu kila kijiji ambacho unapita wanachi wake wanautumia kama chanzo chao kikuu cha maji.

Mvua ambazo zimenyesha mwaka huu, zimesababisha kusambaza uchafu huo kwenye maeneo yote ya mito hiyo, wakati wananchi wanaitumia kama chanzo chao kikuu cha maji, hivyo wanakula uchafu na ndiyo maana wanapata kipindupindu, kwa sababu hawana mbadala wa chanzo kingine cha maji.

Mwananchi mmoja anasema “Serikali inasema hatuna vyoo, tunajisaidia vichani, ni kweli wengi hatuna vyoo, lakini sababu kubwa ni matumizi ya maji ambayo siyo safi na salama, Wilaya, wengi tunatumia maji ya mito ambayo kwa sasa yamekuwa machafu, vinyesi vimesambaa sana,"

.....Watu wanafulia nguo za watoto zenye vinyesi, wanaoga humo na kujisaidia humo, sasa vinyesi hivyo vimesambaa mto mzima, na wakati huo wananchi wanategemea sana hiyo mito, hivyo ni lazima tutapa ugonjwa huu maana wengi hatuchemshi maji yake..........

Wanaokula kwenye shughuli ni majanga

Wananchi wengine wanasema kuwa ndugu zao wamepata maambukizi pindi walipokula chakula msibani au kunywa pombe za kienyeji, shughuli ambazo asilimia 90 zinatumia maji ya kwenye hiyo mito.

Visima vifupi ambavyo wananchi wamechimba pembezoni mwa hiyo mito, navyo ni hatari kwani maji yake yanatoka kwenye hiyohiyo mito.

Visima haviwekewi dawa, Takribani visima 10 ambavyo nilitembelea wananchi waliniambia haviwekewi dawa, ni visima vingine viwili tu ambavyo wananchi walisema dawa ziliwekwa kama miezi miwili imepita na mpaka sasa hazijawekwa nyingine.

View attachment 3133804

Kwenye baadhi ya vijiji ambavyo vina miradi ya maji, ambayo ipo chini ya Wakala wa Maji na usafi wa mazingira mjini na vijijini (RUWASA) hata hivyo jambo la kushangaza wananchi wengi hawatumii hayo maji kutokana na uchumi wao kuwa duni, wanaona bora watumie ya kwenye mito au kisima maana ni bure.

Wengi ambao niliwauliza, wanasema hawana uwezo wa kununua ndoo moja Sh. 50, wanaona ni bora wakachote maji ya bure mtoni kuliko kununua, lakini sehemu nyingine huduma za maji safi na salama hazijafika na ndiko wanatumia zaidi maji ya mito na ndiko mlipuko umetokea kwa wingi

Mito yote ndani ya Wilaya hiyo imejaa vinyesi, imejaa vimelea vya kipindupindu, lakini bado kuna idadi kubwa ya wananchi wanaendelea kutumia maji ya kwenye hiyo mito na wengi hawachemshi hayo maji.

Serikali imeendelea kujificha kwenye suala la vyoo lakini tatizo kubwa ni idadi kubwa ya wananchi kuendelea kutumia maji ya mito hiyo kutokana ukosefu wa huduma ya kutosha ya maji safi na salama.

Chanzo cha Kipindupindi katika Mkoa wa Simiyu hasa Wilaya ya Meatu kama eneo ambalo limeathirika zaidi, ni ukosefu wa huduma za maji safi na salama katika maeneo mengi ya vijiji vya Wilaya hiyo.
Usishangae ukaambiwa kuwa hizo ni picha za wakati wa awamu ya pili!!!!
 
Back
Top Bottom