Serikali imuunge mkono Askofu Dr. Gwajima katika mpango wa kununua Treni ya Mwendo kasi

Serikali imuunge Mkono Gwajima katika mpango wake wa kununua Treni

Heshima kwenu wakuu,

Baba Askofu Dr. Gwajima, ameanza mchakato wa kunua Treni ya mwendo kasi ambayo itakua inatoka Dar hadi Morogoro. Katika usajili bado anawekewa Zengwe, ila nia yake ni nzuri kabisa.

Katika Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kufanikiwa Tanzania ya viwanda kama hatuna Usafiri wa Uhakika wa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Tayari kashafanikisha Mpango wa kujenga chuo cha Urubani, anasubiri ruksa ya Rais Magufuli. Dr Gwajima alishampeleka Mkufunzi wa mambo ya ndege kusomea kufundisha mambo ya ndege. Kwa Tanzania watu wengi wanapenda Urubani lakini garama za masomo ni kubwa. Hivyo kampeleka Kaka John kusomea Ualimu wa ndege. Nadhani wote mnamjua John wa Ufufuo na uzima. Ni kijana mwenye akili sana.

Hadi sasa Dr Gwajima kushirikiana na Msukuma(Mbunge) wameshaanza mchakato wa kumuona Rais ili awape sehemu ya kujenga chuo cha Urubani.

Vilevile ameshaagiza Chopa tatu kwaajili ya wanafunzi.

Wito wangu
Naomba Serikali isilete siasa katika hili Swala kwani lina manufaa kwa Watanzania. Tutawanyanyasa wawekezaji lakini Kenya ikiwachukua tunaanza kulalamika.

Askofu Dr Gwajima kwa wasiomjua, ni Askofu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima ambayo ni Zaidi ya Makanisa mia nne(400) Dunia. Vilevile ana makampuni mengi kama makanisa mengine yalivyo na mabank mfano Mkombozi, Efatha Bank nk.

Dr Gwajima ni Mwalimu ambaye Hulipwa zaidi ya dola 1,000/= kwa saa. Anafundisha Mambo ya Kiroho Duniani na huwa anaalikwa kufundisha hata kwa miezi mitatu.

Kwa sasa anamiliki ndege ambayo humuwezesha kuhudumia Ibada katika Makanisa Matatu Tofauti mikoa tofauti kwa siku.

Watanzania tuache wivu na kijicho cha roho mbaya, bali tuwaunge mkono Watanzania wenzetu ambao Mungu Kawainua.

Daniel 3:16-30

16 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili.

17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.

18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.Tanuri Liwakalo

19 Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto.

20 Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.

21 Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.

22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego.....
tupe mwanga kidogo pesa Za kufanya hayo yote vyanzo vyake ni vipi unaweza weka kila chanzo Na kinaingiza shilingi ngapi?
 
Hadi sasa Dr Gwajima kushirikiana na Msukuma(Mbunge) wameshaanza mchakato wa kumuona Rais ili awape sehemu ya kujenga chuo cha Urubani._Nmeelewa sasa jamaa kutetea Bungeni
 
Hawa matapeli huwa wanawalisha nini?
Mtu amekaa kiujanja ujanja tu chini ya mwamvuli wa dini
 
Mleta mada ametoa pendekezo zuri. Wawekezaji wa ndani wapewe fursa ktk kuukamata uchumi wetu huu wa kibepari tunaoujenga. Ila anaponipa mashaka ni kwenye kutumia vyeo na sifa za kidini ktk swala la kiuchumi tena wa kibepari.... Hapo nimemshangaa sana.

Nadhani yuko kinyume na haya aliyoyahitaji. Unataka utuoneshe nini hapo sasa, kwamba ni tajiri aso mashaka au. Ilitosha tu kusema, bilionea mkubwa Gwajima apewe fursa ya uwekezaji na kivipi anaweza tosha. Hayo ya uaskofu kanisani kwenu. Kwa vipimo vya wengine hafai hata kuwa mfuasi wa mbali wa ukristu.
 
Baba Askofu Dr. Gwajima, ameanza mchakato wa kununua Treni ya mwendo kasi ambayo itakua inatoka Dar hadi Morogoro. Katika usajili bado anawekewa Zengwe, ila nia yake ni nzuri kabisa.

Katika Tanzania ya Viwanda, hatuwezi kufanikiwa Tanzania ya viwanda kama hatuna Usafiri wa Uhakika wa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Tayari kashafanikisha Mpango wa kujenga chuo cha Urubani, anasubiri ruksa ya Rais Magufuli. Dr Gwajima alishampeleka Mkufunzi wa mambo ya ndege kusomea kufundisha mambo ya ndege. Kwa Tanzania watu wengi wanapenda Urubani lakini garama za masomo ni kubwa. Hivyo kampeleka Kaka John kusomea Ualimu wa ndege. Nadhani wote mnamjua John wa Ufufuo na uzima. Ni kijana mwenye akili sana.

Hadi sasa Dr Gwajima kushirikiana na Msukuma(Mbunge) wameshaanza mchakato wa kumuona Rais ili awape sehemu ya kujenga chuo cha Urubani.

Vilevile ameshaagiza Chopa tatu kwaajili ya wanafunzi.

Wito wangu
Naomba Serikali isilete siasa katika hili Swala kwani lina manufaa kwa Watanzania. Tutawanyanyasa wawekezaji lakini Kenya ikiwachukua tunaanza kulalamika.

Askofu Dr Gwajima kwa wasiomjua, ni Askofu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima ambayo ni Zaidi ya Makanisa mia nne(400) Dunia. Vilevile ana makampuni mengi kama makanisa mengine yalivyo na mabank mfano Mkombozi, Efatha Bank nk.

Dr Gwajima ni Mwalimu ambaye Hulipwa zaidi ya dola 1,000/= kwa saa. Anafundisha Mambo ya Kiroho Duniani na huwa anaalikwa kufundisha hata kwa miezi mitatu.

Kwa sasa anamiliki ndege ambayo humuwezesha kuhudumia Ibada katika Makanisa Matatu Tofauti mikoa tofauti kwa siku.

Watanzania tuache wivu na kijicho cha roho mbaya, bali tuwaunge mkono Watanzania wenzetu ambao Mungu Kawainua.

6f0210139cce0b09e4255d3ed1a5eea8.jpg
 
Tuhuma za madawa ya kulevya na wale Wajapan bado zinafuatiliwa...

Halafu mbona mnatumia nguvu kubwa kumpamba ...Mnaficha kitu gani..?
 
Back
Top Bottom