Serikali imesitisha michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA kwa mwaka huu

Mimi nimeelewa kwa maana ya funds zinazotumika katika hiyo michezo zielekezwe katika utengenezaji wa madawati. Nchi ina uhaba mkubwa wa madawati, ni lazima adha ya madawati iwe historia, haiwezekani nchi ina kila kitu, miti na magogo vinasafirishwa kwenda China kila siku alafu watoto wanakaa chini.
 
Bado tunataka Taifa Stars ishiriki kombe la dunia labda kupitia Sumbawanga
 
Serekali haina hela halafu inajitapa inakusanya pesa nyingi mbona awamu ya nne iliokuwa inakusanya kidogo iliweza kufanya yote haya.
Haikuwa na majukumu mengi ya ....bure, .......bure,.......bure,.....bure.
 
Japo kwenye umiseta na umitashumta watu wanapiga pesa lkn pia serikali inakukurupuka hovyo hovyo
 
Atakuwa ni super genius, yaani maamuzi yaliyoshindikana miaka 55 anayafanya kwa miezi sita tu! ...ngoja tuone kitakachofuatia.

labda hatakuwa ni dikteta alietukuka...

ashukuru kauli zake watu wana zpuuza...

~ watakaoleta fyokofyoko!~

~vila&za watafute vyuo size yao!~

~sukari iliyofichwa itagaiwa bure!~

~ watakaoingia barabara ya brt magari yao yaibiwe matairi na trafki!~
 
Yaan amri ya Rais ya mara moja ni muhim kuliko taratibu zetu za kusheria za miaka yote? Only in tanzania!! Kweli hii serikali ya magufuli!! Tupeleke baba .
 
Hawa wa ccm wa kiongozwa na lusinde!!!!!!!!
Teh teh kazi ipo

mkuu umenichekeshaaaaa!!! duuu!!! ccm wako busy na waziri mpango maana kawabeep sasa wanajiandaa kumpigia!!! wakiongozwa na Kangi Lugola, ni shiiidaaaaaaa kuwa na wabunge kama hawa, ya UDOM wamenyamaza kimya huku watu wakiitwa vilaza utadhani wanafunzi wenyewe walijipelek kumbe serikali ya chama hichohicho cha wabunge walewale ndo iliwafanyia udahiri leo hii wamekuwa vilaza? eti ndo wabunge haohao waseme chochote kuhusu michezo!!!! "ndiyooooooooo michezo isitishweeeeeeee"
 
Mwaka huu kila kitu kwenye elimu kinaweza kusitishwa kisa agizo la mkuu. Na hivi sasa nataka kumpa Waziri wazo zuri sana. Akilitekeleza nitajua kweli serikali yetu imedhamiria kuwakomboa watanzania. Huo mpango unahusu kufuta mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne isifanyike kwa kipindi cha miaka mitano ili pesa zilizokuwa zitumike katika kuratibu hizo shughuli ziende kwenye kutengeneza madawati.
Hiili jambo linasikitisha sana, hivi walipokuwa wakipanga pesa za bajeti hawakujua kwamba kuna kununua madawati? Hivi hawa watawala wanaelewa umuhimu wa michezo? Hivi ilaani ya CCM inasema mwaka huu hakuna michezo? Na sio muda mrefu utasikia hiyo michezo mashuleni inapigwa marufuku, halafu utawasikia wakiwahimiza vijana washiriki michezo kimataifa! Mwee, buriani UMITASHUMTA na UMISETA.
 
"Kuna watu wamekatazwa kula mboga za majani mpaka pale suala la pungufu wa mihogo litakapomalizwa"
... irrelevant!!!!!!
 
Serikali imefanya vema;
kwa miaka hii ni shida sana kupata hata hao waalim wakuweza
kusimamia maadili ya hao vijana kwenye hizo kambi;
Ngoja wajipange upya;
 
...inasemekana serikali imezuia kwa muda mashindano ya umisseta na umitashmuta hadi itakapotangazwa baadaye!!!!

Maafisa elimu wa mikoa na wilaya walitaka kutengeneza vitegauchumi vyao
Sio kutengeneza vitega uchumi bwana! Kama ni hivyo si bora waweke mkakati wa kudhibiti mapato na matumizi?? Kuzuia michezo shuleni kunadumaza akili!
 
Niliwahi kucoment hapo awali kuwa kwa sasa ni AWAMU YA TATU@-WORK, kwani mengi yanayofanyika sasa hayana tofauti sana na yaliyokuwa yakifanyika awamu ya tatu.
Magu si ndo aliyekabidhiwa kitabu cha hotuba za mkapa?
 
Back
Top Bottom