Serikali imerasimisha kisheria Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi kitaifa

Mnajua sana kutoa mifano;leo hamtaki kulipa kodi ya majengo,ardhi na ushuru mbalimbali halafu unataka manispaa ziwajibike kwa mapato yapi?...wakwepa kodi na wezi wakiadhibiwa mnawatetea.Bure kabisa.

Hakuna Yoyote ambaye hataki kulipa Kodi. Wewe huna uzoefu wa mambo ya Kodi inaonesha. Tatizo lipo kwa wakusanya kodi. Mfanya Biashara yupo anajulikana na anayo TIN Na VRN zote zimesajiliwa na zipo kwenye mitandao ya TRA ..wakiangali recodi zao wanajua nani amelipa na nani amechelewa au amekwepa muda mrefu. Tatizo lipo hapo hawa ndio wanao turudisha nyuma .
sasa hivi kila kata zimegawanywa kwa watoza ushuru wana wajibu wa kufata na kukumbusha ila wana matatizo ya kuchukua kitu kidogo.

hakuna pia anaepinga kukamatwa wezi , lakini njia zinazo tumika ndio watu wanatofautiana. na pia unapo mshuku mfanya biashara kukwepa kodi...ukiamua kumchukulia hatua basi unaanza TRA jee nani alikua anashughulika na account yake, kwa nini ameka miaka zaidi ya 3 hajalipa unafanya nini ? sasa unamuanza huyu halafu sheria za kodi zipo unamchukulia alokwepa. hapo tutafika.
sasa badala ya Manispaa kutufagilisha asubuhi ingetupa data ya fedha zifuatazo zinakwenda wapi :
  • kodi ya mabango....haya yapo zaidi ya Laki Dar tu peke yake..na hakuna Bango la tangazo linalotozwa chini ya 50,000 . yale Bill boards kwa mwezi ni ni shs 10,000,000 . watuambie wanakusanya kiasi gani kwenye matangazo haya kwa mwaka
  • kuna city levy ya 0.30% ya tuenover ya biashara zote kila quarter hulipwa Manispaa. Nakupa Mfano Turnover ua Insurance Companies ni 500 Billion kwa mwaka hivyo hapa Manaspaa wanapata 1.5 billion kwa mwaka. sasa wewe fikiria Banks ngapi zipo Dar ? fikiria Viwanda turnover zao ni ngapi? fikiria Vinywaji baridi , maji na pombe turnover yao ngapi na city lenvy ni ngapi?
  • Kuna kodi za Liv=cence kila mwaka. Dar kuna biashara ngapi ? jee manispaa wanaingiza kiasi gani ?
  • Kuna hili jipu la Parking fees za jji ...jee unfahamu mtaa mmoja tu wa Samora Unao anza Ocean Road Hospital Mpaka Clock Tower Una Magari mangapi yana Park ? wastani wa park moja ni shs 2,700 kwa siku, na parking za mjini hakuna inayokaa tupu kwa zaidi ya 15 minitues...kwa ufupi parking ni mabilioni ya pesa yanaingia mikononi kwa matapeli...kwa nini Makonda asifanye utafiti wa wiki moja tu kujua kuna Parking ngapi jijini Dar ? utagundua ni fedha nyingi
  • city inapata mapato kutoka vibali tofauti kama ujenzie, taxis, daladala, Harusi , vibali vya kugonga mihuri nk
  • Manispaa wamepewa jukumu la kukusanya ushuru wa majengo , ni kiasi gani wanakusanya ? kama wapo wasio lipa sanbabu gani ? jee wamefuatilia na sharia kufata mkumbo?
  • pia sio vibaya manispaa ikatuambia inaajiri watu wangapi kwa kila secta na wanatumia kiasi gani kama mishahara..na jee kuna umuhimu wa kuwa na hao wafanya kazi ? lengo la kodi zetu kwa manispaa sio kutoa ajira kiholela , fedha hizi ni kwa ajili ya kulihudumia Jiji.
Tukiweza kupata data hizo na kufatilia mianya basi hili Jiji litakua jiji safi zaidi Duniani . Vyanzo vyake vya mapato ni vingi na vinatosha pamoja na kuliwezesja jiji kuwa na mabustani na sehemu za kupumzikia. ..
Tukilafanyia audit ya sawa sawa wana jiji hawana haja ya kusafisha , wao kazi yao itakua ni kujenga Taifa . ...
Njoo na Mjaibu hayo au Muuize Makonda kama anaweza kutupatia data hizo...tuone kama Jiji halina uwezo wa kujiendesha...
USIKU MWEMA
 
Back
Top Bottom