Serikali imenyoosha mikono dhidi ya watoa huduma za TV!

Ukweli ni kwamba TCRA ni wala rushwa wa hali ya juu, kwa sababu kama sheria wanayoitumia haifai basi wangefuata utaratibu wa kupendekeza mabadiliko ili itungwe sheria mpya inafaa. Ukiangalia sababu TCRA wanazotoa kwa kutoweza kuitekeleza sheria iliyopo hazina msingi wowote. Hii ni changamoto kwa waziri wa mawasialiano kupata ufumbuzi wa tatizo hili. Kinachofanyika hapo ni TCRA wamewekwa mfukoni wa wafanyabiashara. Tunamuomba Rais Magufuli atume vijana wake wamletee ripoti kwani majipu yako tayari kutumbuliwa.
 
Hizi asasi kama Tcra nk, tatizo lao liko kwenye namna maafisa wao wanavyopatikana au wanavyoteuliwa.

Chombo chenye mamlaka ya uteuzi kina mamlaka yaliyopitiliza kuweza kuteua tu watu bila sifa au vigezo vinavyoeleweka na kwa mantiki hiyo wateule huishia kuwa wapambe au washikaji wa anayeteua.

Hii hali ya kukosekana kwa "Vetting Procedure" ndio chanzo cha taasisi zote type hii kuishia kuwa dhaifu na kubaki kuwa tu chanzo cha ajira kwa "Presidential Favourites".
 
Nimepitia kwa uangalifu mwongozo wa TCRA juu ya kuonekana kwa local cuannels bure.. TCRA wanasema kwamba makampuni ya Startimes, Ting, Continental na Digitek hayajajisajili kama Pay TV hivyo yanapaswa kuonesha local channels BILA MALIPO. Hata hivyo makampuni ya Zuku, Azam, Multchoice yamesajiliwa kama pay TV hivyo watumiaji wanapaswa kulipia channels zake zote ikiwa ni pamoja na local channels.

Katika hali ya kushangaza ni namna TCRA, Mawaziri wa mawasiliano na viongozi wengine wa serikali wanavyokuwa WANYONGE ikifika suala la kujibia hili. Matamko mbalimbali yametolewa Bungeni kuyaamuru makampuni yasiyo pay tv kuachia local channels lakini hakuna kinchofanyika, mpaka sasa Startimes, Ting, Continental hawaachii local channels bure.

Niliwauliza TCRA wakasema tatizo ni wamiliki wa hizo local channel kushindwa kulipa gharama za uendeshaji kwa makampuni ya Startimes, Ting, Continental na Digitek hivyo kukatiwa huduma.

Hayo ni majibu mepesi sana na yakitoto, kwani wanachotaka watanzania ni kupata habari kama zamani (kabla ya digital) haya mambo ya nani anakwamisha HAYATUHUSU sisi watumiaji na yanapaswa kumalizwa.. halafu nashangaa kama mliweza kukimbizana na bloggers na wakatii ndani ya muda mfupi, mnashindwa nini kuwaadhibu wanaokwamisha?

MODERATOR IKIWEZEKANA U PIN HUU UZI WAHUSIKA WAONE
Sijuti HAYATUHUSU?! KWELI?!
 
Back
Top Bottom