Babu Kijiwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 4,830
- 4,727
Nimepitia kwa uangalifu mwongozo wa TCRA juu ya kuonekana kwa local cuannels bure.. TCRA wanasema kwamba makampuni ya Startimes, Ting, Continental na Digitek hayajajisajili kama Pay TV hivyo yanapaswa kuonesha local channels BILA MALIPO. Hata hivyo makampuni ya Zuku, Azam, Multchoice yamesajiliwa kama pay TV hivyo watumiaji wanapaswa kulipia channels zake zote ikiwa ni pamoja na local channels.
Katika hali ya kushangaza ni namna TCRA, Mawaziri wa mawasiliano na viongozi wengine wa serikali wanavyokuwa WANYONGE ikifika suala la kujibia hili. Matamko mbalimbali yametolewa Bungeni kuyaamuru makampuni yasiyo pay tv kuachia local channels lakini hakuna kinchofanyika, mpaka sasa Startimes, Ting, Continental hawaachii local channels bure.
Niliwauliza TCRA wakasema tatizo ni wamiliki wa hizo local channel kushindwa kulipa gharama za uendeshaji kwa makampuni ya Startimes, Ting, Continental na Digitek hivyo kukatiwa huduma.
Hayo ni majibu mepesi sana na yakitoto, kwani wanachotaka watanzania ni kupata habari kama zamani (kabla ya digital) haya mambo ya nani anakwamisha HAYATUHUSU sisi watumiaji na yanapaswa kumalizwa.. halafu nashangaa kama mliweza kukimbizana na bloggers na wakatii ndani ya muda mfupi, mnashindwa nini kuwaadhibu wanaokwamisha?

MODERATOR IKIWEZEKANA U PIN HUU UZI WAHUSIKA WAONE