Serikali imekamilisha ujenzi wa shule ya sekondari, Wanafunzi wamezeshwa script iliyowasaliti kumsifia Rais Samia

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,013
1,634
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya kata ya Hinju, halmashauri ya mji Nanyamba mkoani Mtwara, wameishukuru Serikali kwa kuwajengea shule ya kisasa ya kata, iliyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 560.

Kwa kipindi kirefu wanafunzi wa kata hiyo, wamepitia mateso ya kutembea umbali umrefu kwenda kata jirani kwa ajili ya kufuata shule, kutokana na kata yao kutokuwa na sekondari.

Zawia Khatibu na Muslim Juma, ni miongoni mwa wanafunzi wa kidato cha Pili, ambao wametoa shukrani zao kwa serikali huku wakimpongeza zaidi Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuona umuhimu wa kushusha fedha hizo kwa ajili ya kuwasogezea karibu fursa ya kupata elimu.

Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota, amefika shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi ikiwa ni sehemu ya ziara yake jimboni, akikagua miradi ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom