Rais2020
JF-Expert Member
- Jul 14, 2016
- 3,248
- 5,537
Jaribu kutafuta kazi sehemu nyingine tofauti na hiyo.Mimi ni miongoni mwa vijana 3000 waliositishiwa ajira zetu mwezi June 2016 niliajiriwa na serikali nikapangia kituo cha kazi na kuanza kufanya kazi baada ya mwezi mmoja nilipewa barua ya kusimamishwa nilipomuuliza afisa utumishi wangu kuwa nitarudi lini kazini ? Afisa utumishi aliniambia nitarudi kazini baada ya uhakiki wa watumishi hewa alisema kuwa zoezi hilo ni La mda tu .
Mimi hapa naandika haya kwa masikitiko makubwa sana leo hii nakaribia kumaliza mwaka toka ajira yangu isimamishwe nilipangia kazi kigoma lakini nyumbani ni mwanza nilihamisha mizigo yangu kutoka musoma hadi kigoma nilipo pangiwa kazi nilipanga chumba huko kigoma baada ya kuanza kazi Leo hii mizigo Yangu ipo kwa mwenyekiti wa mtaa mwenye nyumba ndoo ameikabidhi hapo kwa kutoka na mimi kushindwa kulipa kodi ya chumba.
Nilitumia gharama nyingi sana kwenda kwenye usaili,kwenda kazini Leo hii serikali inaniona sina maana yeyote kabisa .
Serikali hii sina hamu nayo tena jamani maana nchi hii imenisaliti kwenye kutokana hali ya ambayo ninayo sasa hivi nchi hii imekuwa ngumu sijui hatima Yangu.
Nimesomeshwa na bibi Yangu kizaa mama baba alishafariki serikali hii imeamua kuniharibia maisha Yangu hivi jamani sasa hivi bibi Yangu alijua amepata angalau sehemu ya kula mpaka sasa sijui hatima Yangu na wenzetu.![]()
Kajitetea hiliUnakimbia wakati hauna break..
What do u expect...
Huyu inabdi aombe radhi uma kwa kutudanganya.