Serikali futeni bima ya afya

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
833
1,476
Asilimia kubwa ya wananchi wana Bima ya Afya lakini hakuna manufaa wanayopata kutokana na Bima ya Afya. Kila hospitali unayoenda ukiisha elezwa na mganga ugonjwa wako na dawa unazotakiwa kutumia basi hapo lazima uingie mfukoni.

Jana nilienda kupata chanjo ya homa ya ini katika hospitali fulani. Nilipofika nikatoa kadi ya Bima ya afya na walichoinieleza kuwa walisha achana na Bima ya Afya kwa sababu zifuatazo:-

(1) Hawalipi kwa wakati. Unaweza kulipwa baada ya mwaka.

(2) Kama madai yako labda 10 millioni basi unaweza kulipwa 2 millioni zingine unaambiwa usubiri.

(3) Kuna madai ya vipimo vingine ambavyo Bima wanakataa kulipa ili hali uliishapima na hivyo inakuwa hasara kwako. Hivyo walikataa kupokea kadi yangu na ikabidi nitoe fedha taslimu Tshs.30,000 ya kipimo na chanjo.

Mimi sioni maana ya kuwa kwenye Bima ya Afya kama kila ukiugua matibabu yote ni fedha unayotoa mfukoni mwako. Serikali futeni Bima ya Afya hakuna nafuu tunayopata sisi wananchi.
 
Bima ya afya inayo changia hela ya kumwona Daktari tu - sasa bima gani hiyo kama si utaniana.
NI kheri uwe huna ujue huna.
 
Back
Top Bottom