Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,800
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, leo Bungeni ijini Dodoma alisimama kutoa taarifa kuhusu kuidhinishwa kwa sera ya elimu na mafunzo ya Elimu 2014 toleo la 2023, amesema sera ya Elimu na mafunzo imefanyiwa mabadiliko kwenye maeneo kadhaa kulinganisha na sera iliyopita na maeneo hayo ni elimu ya lazima kuwa ya miaka 10 badala ya 7, aidha elimu hiyo lazima inajumuisha elimu ya msingi ya miaka 6 na elimu ya sekondari ya chini itatolewa kwa miaka 4, utekelezwaji wa pendekezo hilo utaanza kufanyika mwaka 2027 sambamba na kufuta mtihani wa Darasa la 7.