DOKEZO Serikali chukueni hatua kuepusha vifo. Baada ya kuruhusu safari za usiku nimegundua yafuatayo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Hivi karibuni serikali imefanya uamuzi bora kabisa wa kuruhusu magari ya abiria ( mabasi) kutoa huduma masaa 24.

Hili ni jambo bora na la kupongezwa kwani linachochea ukuaji wa uchumi kwa watoa huduma kuweza kutoa huduma kuweza kuongeza muda wa kazi.

Pamoja na uamuzi mzuri kuna kasoro kadha wa kadha ambazo zinaweza kugeuza huduma hii bora kuwa janga kama ifuatavyo:

1. Nimegundua watoa huduma ya usafirishaji sasa magari hayapumziki, mfano mdogo kampuni ya kilimanjaro inafanya safari ya kuja Dar na kurudi Arusha siku hiyo hiyo.

Hiii ni hatari sana kwani kwa utaratibu wa usafirishaji magari hukaguliwa kabla ya safari lakini wao wakirejea Dar na kushusha abiria wanapakia papo hapo kurejea Arusha

2. Madereva hawapumziki kwa kutaka kujipatia pesa zaidi.

Kwa kawaida gari ya masafa marefu inatakiwa kuwa na dereva zaidi ya mmoja kwa ajili ya kupeana zamu.

Hii ni hatari kuna siku italeta msiba mzito.

3. Ubovu wa magari, sina kinyongo wala maslahi na kumtaja Kilimanjaro, ukweli mchungu usiku atatumia magari yamechoka sana na yametembea miaka mingi yenye namba A.

Abiria wamekuwa wakiyalalamikia kwani njiani yanapiga kelele kama vile uko rough road.

Nakiri kuwa ana gari chache mpya, hata haya yaliyochoka injini zake ni Scania lakini yamechoka mnoo.

4. Ubovu wa barabara nyingi nchini ni tatizo kubwa.
Kuna mashimo ambayo ni vigumu kuonekana usiku.

Kwa haya mambo manne yasipoangaliwa na kutatuliwa tutarajie ajali za kutisha.
 
Jumamosi nimekutana na Kilimanjaro express imechochora mitaa ya kirinjiko same acha kabisa ametoka baranarani Zaid ya nusu kilomita kaingia porin Yan angekutana na mti sijui ingekuwaje.
 
Back
Top Bottom