BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,817
Serikali imetangaza ongezeko la bei katika baadhi ya bidhaa za vyakula, huku kushuka kwa uzalishaji ikitajwa kuwa sababu.
Miongoni mwa bidhaa za chakula zilizopanda bei katika mwaka ulioishia Septemba mwaka huu ikilinganishwa na mwaka ulioishia Agosti mwaka huu ni mchele, maharage, mahindi.
Hayo yameelezwa leo Septemba 15 na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa bei za bidhaa katika mwaka ulioishia mwezi Agosti mwaka huu.
Dk Kijaji amesema bei ya mchele imeongezeka hadi kufikia kati ya Sh2000 hadi Sh3500 katika Septemba mwaka huu.
"Ikilinganishwa na Agosti mwaka huu bei ya mchele sokoni ilikuwa kati ya Sh1700 na Sh3000,"
Bei ya maharage ilifika kati ya Sh1, 750 hadi Sh3500 ikilinganishwa na Sh1800 hadi Sh2, 600 iliyokuwapo Agosti mwaka huu.
Kuhusu mahindi bei yake imefikia Sh900 hadi Sh1,550 kwa kilo ikilinganishwa na Sh700 hadi 1,500 Agosti mwaka huu.
Kuhusu uzalishaji wa chakula, mahindi yalishuka kwa asilimia 7.1, uzalishaji wa mchele ulishika kwa asilimia 30.9 na maharage uzalishaji ulishuka kwa asilimia 11.1. Kati ya mwaka 2020/2021 ikilinganishwa na Mwaka 2021/2022.
Ongezeko hilo la bei katika baadhi ya bidhaa za chakula na zisizo za chakula zimefanya mfumuko wa bei wa Taifa kuongezeka kwa asilimia 0.1 katika mwezi Septemba ikilinganishwa na mwezi uliotangulia.
Hapa chini ni Bei za Bidhaa kwa Mwezi August 2022