- Thread starter
- #21
Tume ya pili imeainisha deni wanalopaswa kulipa ACACIA. Lakini bado hatujakubaliana na ACACIA kama watalipa.Hivi deni ambalo wanadaiwa na wamekubali kulipa ni deni gani?ni fedha ambazo zimebainika kuwa ziliibiwa kutokana na mikataba mibovu ambayo ilipitishwa na watuhumiwa wetu?au katika pesa hizohizo chache walizotakiwa kulipa Kuna sehemu hawajalipa?.
Deni lenyewe linatokana na udanganyifu waliotufanyia. Deni hili linajumuisha:
1.
4% ya kiasi walichotudanganya kimo ndani ya makinikia kuanzia 1998. Hapa wanaweza kupata punguzo wakidai kuwa haya ni makadirio tu na hakuna uthibitisho kuwa huo mchanga wa zamani ulikuwa na kiasi sawa na ule ulioko bandarini sasa hivi.
2.
Kodi ya mapato ya madini ambayo walidatudanganya wamepata, kama ilivyo kifungu cha 1.
3.
Makontena waliyosema wamesafirisha tangu 1998 ni kidogo kuliko ukweli kufuatilia takwimu za wenye meli waliosafirisha haya makontena. Hapa wanapaswa kulipa mrabaha, kodi ya TRA, na faini ya wizi tokea 1998.
Kifungu cha 1 na cha 2 tunaweza kujadiliana nao na wakapata unafuu.
Lakini hiki cha 3, eeeeh ndugu yangu - huu ni wizi na hawawezi kuchoropoka hapa.
Sijui kama nimekujibu swali lako.