ManoWise
Member
- Jun 21, 2019
- 18
- 19
Leo ningependa kuzungumzia suala la uongozi, siasa, na utumishi wa umma kwa ujumla. Kuna mambo kadha wa kadha ninayaona katika nchi yangu, na mimi kama kijana nimepata mawazo ya kuyawasilisha katika jukwaa hili la mabadiliko maarufu kama "Stories of Change" la mwaka huu wa 2024. Naomba ulisome kwa makini ndugu msomaji.
Kuna viongozi mbalimbali wamelitoa taifa mbali sana mpaka hapa tulipo na wanaendelea kulipeleka mbali. Tunawashukuru sana kwa mchango wao mkubwa.
Hata hivyo, kuna tatizo hasa katika ushirikishwaji wa vijana katika maendeleo ya umma na uongozi. Tumekuwa tukiona viongozi wa nafasi mbalimbali, ikiwemo wabunge, wanakuwa viongozi aidha wa kuchaguliwa au kuteuliwa tangu vijana mpaka wanazeeka.
Jambo hili linasababisha vijana wa kipindi fulani cha muda katika eneo husika au jimbo husika kukosa nafasi ya kuongoza. Hali hii inaweza kupelekea karama zao za uongozi kutotumika ipasavyo, na kutukosesha wananchi ubunifu wao ambao pengine ungeleta maendeleo ya kipekee.
Nasisitiza uwepo wa Imani ya Viongozi wetu kwa vijana na kupokezana vijiti kwa mchanganyiko mzuri wa wananchi wa rika tofauti tofauti na si kuacha mpaka viongozi wazeeke ndipo wawekwe vijana, pengine nawe umekuwa shahidi wa kuona viongozi walewale wa kila siku wakibadilishana wizara, kupanda na kushuka kwa vyeo katika kila awamu ya uongozi na hata wakifanya vibaya au vizuri wanaendelea kutumikia nafasi zao kwa kuhamishwa na kurudishwa na kutolewa na kuwekwa tena kwenye nafasi hizo, yani imekuwa ni kutenguliwa na kuteuliwa kwa majina yale yale ya uongozi na uwepo wa baadhi waliodumu kwa zaidi ya miaka 25.
Na muda mwingine waweza kujiuliza hivi, hakuna watu wengine wanaofiti pia hizi nafasi? Mtu mmoja maarufu aitwaye Malcolm X alisema, "The future belongs to those who prepare for it today." Na sasa ni jukumu letu kuiandaa nchi yetu mapema kwa kizazi hiki na cha baadaye kwa kuweka sawa hili jambo katika mabadiliko ya kiserikali na sera zetu za utumishi wa umma.
Ndugu msomaji, tambua kuwa kumpa nafasi kijana kunamhamasisha kijana. Na hamasa hii inamfanya kijana kutambua mapema malengo na mipango ya jamii yake na kufanya ajitolee zaidi katika uongozi.
Lengo la andiko hili si kutoa maoni ya kupunguza wazee katika nafasi za uongozi na kuweka vijana. Lahasha! Lengo langu ni kutoa maoni juu ya kuongeza idadi ya vijana na jinsi ya kuwaongoza(kuwamentor) na kuwanoa mapema kwa kuwapa nafasi za uongozi.
Kumpa kijana nafasi ya uongozi kuna faida nyingi. Kwanza kabisa, vijana wana mawazo mapya na nguvu mpya ambayo inaweza kusaidia katika kuboresha na kuendeleza nchi.
Ubunifu wao unaweza kuleta njia mpya, nzuri na zenye ufanisi za kutatua changamoto zinazolikabili taifa kwa ujumla.
Kama alivyosema mwandishi maarufu wa kifilipino José Rizal, "The youth are the hope of our future,” akiweka mkazo wa tegemeo letu kwa vijana na Pili, vijana wamezaliwa na kukua katika ulimwengu huu wa sasa wa teknolojia hivyo Uwezo wao wa kutumia teknolojia kwa ajili ya maendeleo ni mkubwa kulinganisha na rika lingine katika nchi yetu ya Tanzania, na wanaweza kusaidia katika kuimarisha mifumo ya kisasa katika serikali na sekta binafsi.
Kuwapa nafasi vijana pia ni njia mojawapo ya kuwaandaa viongozi wa baadaye na kutengeneza kesho iliyo bora zaidi kwa Taifa letu la Tanzania. Ni muhimu kuwapa nafasi vijana sababu itawapa fursa ya mafunzo na uzoefu ambao utawasaidia kuongoza nchi kwa ufanisi zaidi.
Kuna msemo wa kiingereza unasema "Leaders are made, they are not born,” ambao unahamasisha juu ya kukuza na kulea uongozi miongoni mwa vijana wakiwa bado wadogo ili kuwafanya wawe viongozi bora zaidi na zaidi na pia mwanaharakati na mwandishi maarufu wa kimarekani Ralph Nader aliwahi kusema , "The function of leadership is to produce more leaders, not more followers."
Vijana wapewe nafasi ya kuongoza, na sio kuwa wafuasi tu wa vyama na makundi ya kiserikali na kisiasa. Ninaamini vijana wanaweza kutoa suluhisho bora kwa matatizo yanayowakabili wananchi kwa ufanisi na nguvu zaidi.
Hata hivyo, si kila kijana anapaswa kupewa nafasi ya uongozi bila kuzingatia uwezo na uadilifu wake. Ni muhimu kuhakikisha kuwa vijana wenye uwezo na uadilifu ndio wanaopewa nafasi hizo, kama tunavyojua uadilifu na uzalendo ni jambo lenye thamani sana na linapaswa kuthaminiwa katika Nyanja ya uongozi na siasa kwa ujumla.
Hivyo serikali kupitia mamlaka zilizopo wanapaswa kuweka sera na mazingira ya kuwanoa vijana kwa kutengeneza majukwaa na fursa za vijana kujifunza uongozi sahihi.
Mfano kuna Chuo kikubwa cha Uongozi na Siasa kilichozinduliwa mnamo tarehe 23/2/2022 Mkoani Pwani-Kibaha (Mwalimu Nyerere Leadership School) kinaweza kushirikiana na Vyuo vikuu vingine hapa nchini kutumika kunoa vijana mbalimbali kwa kufundisha maadili mema ya Uongozi na kuweka vigezo nafuu vya udahili ili kuruhusu vijana wa ngazi tofauti tofauti ya Uchumi kujumuika, hii itasaidia katika kuwaongoza na kuwapatia ujuzi muhimu wa uongozi.
Picha 1; Pichani ni chuo kijulikanacho kama shule ya uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere kilichopo Kibaha kwa Mfipa mkoani Pwani.
Chanzo cha picha: Mwalimu Nyerere Leadership School
Waswahili wanasema “Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu" hivyo naomba serikali iweke sera ya kuwaunganisha vijana wenye karama za Uongozi bila kujali vyama, dini, ukanda, jinsia, kabila wala rangi zao na kuwajengea misingi mizuri ya uongozi kwa Pamoja na muhimu zaidi kuwapa nafasi za kuongoza na kuwaamini zaidi katika ngazi za juu za uongozi wangali na nguvu na damu changa.
Nafasi za uongozi ni za kupokezana, na kila mmoja ana wakati wake, Ni muhimu kutoa nafasi kwa wengine pia, hususan vijana kwani Uongozi ni dhamana na ni wajibu kuhudumia watu na si vinginevyo. Hii inapaswa kuwa msingi kwa viongozi wa rika zote, vijana na wazee.
Kwa kumalizia, ni muhimu kuhakikisha kuwa tunawapa vijana nafasi ya kushiriki na kuongoza katika nafasi mbali mbali na kwenye maendeleo ya umma na sio kuwa wafuasi tu. Tunapaswa kuwatayarisha vijana wetu kwa kuwaelimisha, kuwanoa ipasavyo, na kuwapa nafasi za kuonyesha uwezo wao.
Kwa kufanya hivyo, tutakuwa na taifa lenye viongozi bora na wenye uwezo wa kulipeleka taifa mbele zaidi katika vizazi vingi vya nchi yetu ya Tanzania.
Naipenda Tanzania yangu,
Mwisho, na Asanteni.