Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mwaka 2017, akihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu namna anavyoutumia mtandao huo, Selena alinukuliwa akisema “Huwa nafuta App ya mtandao huu walau mara moja kila wiki sababu Watu huandika maoni makali kama vile wanataka kukutoa roho”
Mwaka 2019 aliamua kusitisha matumizi ya mtandao wa Instagram ambapo pamoja na sababu zingine alidai ni kuwepo wa unyanyasaji mkubwa, hali iliyomfanya awe kwenye hatari ya kupatwa na sonona.
Baada ya kutokuwepo kwenye mtandao huo kwa zaidi ya miaka 4 huku akimuwaachia udhibiti wa Akaunti hiyo wasaidizi wake, January 13, 2023 alirejea tena kwa kupost picha iliyoambatana na maneno …”Wait, can you tell I’m back on Instagram?”
Selena Gomes ni mwanamuziki mwenye ushawishi mkubwa kwenye Mtandao wa Instagram. Anashikilia nafasi ya 5 ya kuwa mtu mwenye wafauasi wengi zaidi kwenye mtandao huo.
Umewahi kufuta mitandao ya kijamii baada ya kukutana na unyanyasaji wa aina yoyote ile?