Wanajukwaa salaam!
Kilicho nisukuma kuandika uzi huu ni baada ya kushuhudia vijana wengi wakikata tamaa na kujutia maamuzi yao ya kujiendeleza kielimu kwa kukosa haki za kuajiriwa serikalini.
Kama tujuavyo, nafasi za kazi zote za serikali hutangazwa na huombwa kupitia mfumo wa sekretarieti ya ajira.
Kilichonishangaza zaidi ni vile jinsi mfumo walivyouweka hadi nikajiuliza kama kweli tunawatu wenye uwezo wa kufanya maamuzi kwenye hii taasisi au la! ni baada ya kukutana mabinti kadhaa wakimwaga machozi baada ya kukataliwa na mfumo na hata baada ya kufunga safari kwenda ofisi za sekretareti ya ajira kuelezea matatizo yao.
Mfumo uko hivi mfano, mtu aliyesoma degree akaomba kazi kupitia mfumo huo mda fulani nyuma na baadae akaamua kusomea fani nyingine tofauti kwa level ya stashahada basi hawana haki ya kupata kazi serikalini kwa fani ya level ya diploma kupitia mfumo huo wa ajira. Yaani mf. Kasoma degree ya ualimu na baadae akasoma diploma ya uhandisi basi kamwe huwezi pata kazi ya uhandisi serikalini, au ukisoma au ukisoma masters basi huwezi pata kazi kwa degree.
Hata walipofuata ofisini sekretariate walibaki na msimamo kuwa hawawezi kamwe.
Sasa nikajiuliza; hii inafaida gani? Ni nani alitoa na kulitekeleza wazo ya hovyo namna hiyo? Hii ni haki kweli?Hatuwezi songa mbele kwa mawazo ya kimaskini na finyu namna hiyo! Inawakatisha tamaa vijana kusomea fani mbaili mbali.
Sekretarieti ya ajira mlitazame hii kwa upana wake kwa narrow minds namna hii.