Jerry001
JF-Expert Member
- Apr 29, 2020
- 575
- 1,280
Habari,
Sekretarieti ya ajira mmeaminiwa kutangaza na kuendesha mchakato wa ajira kwa haki na usawa ili watanzania tuombe ajira za umma kupitia taasisi yenu. Mnapokuwa mnaweka vigezo ambavyo havina umuhimu mkubwa na kuzuia watu kufanya usaili ni kama kutuwekea vigingi tu tunaoomba hizo ajira.
Inafahamika kuwa ili kufungua akaunti kwenye mfumo wenu wa ajira portal ni lazima ujisajili kupitia namba ya NIDA, Mchakato wa kupatikana kwa hii namba ya nida wote tunaujua. Na ndio kitambulisho halali cha mtanzania.
Sasa inapokuja suala la ku-shortlist watu kwa ajili ya usaili, kuna vitu muhimu kama vyeti vya academics na transcript pamoja na barua ya kuomba ajira. Ila hili la mtu kutokuitwa kwenye usaili kwa sababu hajaweka cheti cha kuzaliwa ni kigingi kisicho na sababu wakati taarifa zake zipo kwenye NIDA. Mbaya zaidi ati mtu anakuwa not-shortlisted kwa sababu cheti cha kuzaliwa hakijagongwa muhuri wa mwanasheria. Huu ni ukatili tu usio na sababu yenye mashiko.
Fanyeni kazi yenu kwa weledi. Acheni kujigeuza taasisi ya kuhakiki taarifa ambazo hazina mashiko kwenye kuomba ajira. Afterall hivyo vyeti vya kuzaliwa ambavyo mnazuia watu kuwa short-listed mnaviomba tena original copies wakati wa kufanya usaili. Cheti cha kuzaliwa kina taarifa gani ya msingi kwenye uombaji wa ajira wakati taarifa zote zipo kwenye NIDA? Taasisi za mifuko ya kijamii kama PSSSF na NSSF zilishatoka huko, zinatumia taarifa za NIDA kutimiza majukumu yake. Badilikeni.
Sasa hivi ni zama za teknonlojia, mifumo inasomana. Ukiweka index number ya form four au form six inabidi mfumo wenu uvute vyeti kutoka NECTA. Hili la kutokumwita mtu kwa sababu ya cheti cha kuzaliwa hakijagongwa muhuri ni kigingi kisicho na sababu yenye mashiko. Cha kushangaza attachment ya cheti cha kuzaliwa mmeweka kwenye kipengele cha other attachments jinsi ambavyo hamjakipa kipaumbele.
NB: Waombaji wa ajira tufuate maelekezo ili kuepukana na hizi changamoto.
Nalog out