Saudi Arabia, UAE, Iran, Egypt, Ethiopia na Argentina zakubaliwa kujiunga BRICS

Mzee wa kupambania

JF-Expert Member
Aug 14, 2022
18,846
45,752
20230824_133030.jpg

Sasa BRICS itakuwa na wanachama 11 wenye sifa zifuatazo

● BRICS itakuwa na mataifa 6 kati ya 9 ambayo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta na gesi duniani.

● BRICS itakuwa na mataifa ambayo yana 80% ya oil reserve duniani.

● BRICS itakuwa na mataifa yenye jumla ya GDP $30.76 trillion. Asilimia 36% ya uchumi wa dunia utakuwa mikononi mwa mataifa ya BRICS.

Zaidi ya mataifa 40 tayari yameonyesha nia ya kujiunga na BRICS.

Watafiti wa mambo ya kiuchumi wanasema uwepo wa mataifa makubwa yanayozalisha nishati ya mafuta ndani ya BRICS kutadhoofisha mfumo wa PetroDollar ikizingatiwa baadhi ya mataifa hayo yameanza kutumia sarafu zao katika biashara ya nishati hiyo.
 
1692876358338.png

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza kwamba kundi la mataifa yanayochipuka kiuchumi (Brics) litapokea wanachama wapya sita, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Falme za Kiarabu (UAE) na Iran, mwanzoni mwa mwaka 2024.

Takribani nchi 40 duniani zimeonesha nia ya kuwa wanachama huku 23 zikiwa tayari zimetuma maombi yao. Wanachama wa Brics wamekubaliana kulipanua kundi hilo kwa kuongeza wanachama wapya.

Katika mkutano huo uliofanyika leo Alhamisi Agosti 24, 2023 huko Johannesburg, Afrika Kusini, viongozi zaidi ya 50 kutoka mataifa yasiyo wanachama wa Brics wamehudhuria akiwemo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

“Tumeamua kuzikaribisha Argentina, Misri, Ethiopia, Iran, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwa wanachama kamili wa Brics. Uanachama wao utaanza rasmi Januari Mosi, 2024,” Rais Ramaphosa aliuambia mkutano wa kilele mjini Johannesburg.

Wito wa kupanua Brics inaundwa na nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, ulikuwa umetawala ajenda katika mkutano huo wa siku tatu na kufichua mgawanyiko kuhusu kasi na vigezo vya kupokea wanachama wapya.

Lakini kundi hilo ambalo hufanya uamuzi kwa makubaliano, lilikuwa limekubaliana juu ya “kanuni elekezi, viwango, vigezo na taratibu za mchakato wa kuipanua Brics,” amesema Ramaphosa.

Takriban nchi 23 zilikuwa zimetuma maombi rasmi ya kujiunga na kundi hilo ambalo linawakilisha robo ya uchumi wa dunia na zaidi ya watu bilioni tatu.
 
Hii si habari njema kwa mataifa ya G7

Ikumbukwe kuwaweka pamoja Iran na Saudi Arabia hapo ni juhudi za China za kuyapatanisha mataifa hayo mawili wakati Marekani alitamani mataifa hayo yaendelee kuwa hasimu

Egypt na Ethiopia zimekuwa na msuguano kwenye bwawa la GERD kuyaleta pamoja mataifa hayo ni juhudi nzuri za BRICS

Kikubwa zaidi ni uwepo wa mataifa ya Africa inapendeza sana
 
Watafiti wa mambo ya kiuchumi wanasema uwepo wa mataifa makubwa yanayozalisha nishati ya mafuta ndani ya BRICS kutadhoofisha mfumo wa PetroDollar ikizingatiwa baadhi ya mataifa hayo yameanza kutumia sarafu zao katika biashara ya nishati hiyo
Ikiwa watatumia sarafu zao iwe ni wao wenyewe wanachama wa BRICS au na mataifa mengine yaliyoonyesha nia ya kujiunga na BRICS itaathiri dollar ya Marekani kwa sababu Mmarekani atajikuta amebaki na dollars ambazo hazipo kwenye mzunguko duniani

Na biashara ya mafuta ni mojawapo ya biashara inafanya dollar iwe na demand kubwa duniani
 
Ikiwa watatumia sarafu zao itaathiri dollar ya Marekani kwa sababu Mmarekani atajikuta amebaki na dollars ambazo hazipo kwenye mzunguko duniani

Na biashara ya mafuta ni mojawapo ya biashara inafanya dollar owe na demand kubwa duniani
Mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa China ni Marekani.

Top 5 ya washirika wa kibiashara wa Brazil baada ya China ni Marekani na nchi za Ulaya.
 
Hii inaamaanisha soko kubwa la mafuta la BRICS liko nje kwa mataifa ambayo sio wanachama.

Hii inaweza kuwa faida kubwa sana kwa China yenye uchumi mkubwa na mahitaji makubwa ya mafuta kujipatia mafuta kutoka kwa nchi wanachama kwa bei chee kwa mgongo kwamba ni mwanachama wa BRICS.
 
Mshirika mkubwa zaidi wa biashara wa China ni Marekani.

Top 5 ya washirika wa kibiashara wa Brazil baada ya China ni Marekani na nchi za Ulaya.
Nilimaanisha kwenye biashara ya mafuta kama vile ambavyo sasa hivi Russia na China; Russia na India wanatumia sarafu zao

Bado China na Brazil kuna biashara wanatumia sarafu zao

Saudi Arabia, India wameanza kutumia pia sarafu zao kwenye transactions zao

Je, hauoni hapo dollar ya Marekani imepoteza ushawishi maana kabla ya hapo hayo mataifa yalikuwa yakitumia US dollar?
 
Back
Top Bottom