Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,103
- 21,087
Wala sihitaji kuandika thread ndefu juu ya hili, kwa sababu linapaswa kuwa wazi sana kwa mtu yeyote mwenye akili. Kuna tofauti kubwa sana kati ya serikali ya Raisi Magufuli na serikali ya Raisi Samia iliyopo madarakani sasa.
Magufuli akiwa raisi wa Tanzania, alikuwa tayari kufanya lolote lile, na narudia, lolote lile, kwa ajili ya nchi ya Tanzania. Alikuwa tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile alichoona ni maslahi ya Watanzania, ambao yeye alikuwa beneficiary mmoja wao.
Samia, akiwa raisi wa Tanzania, yuko tayari kufanya lolote lile, na narudia lolote lile, kwa ajili ya uongozi na CCM. Yuko tayari kuvunja baadhi ya vipengele vya Katiba ya Tanzania kwa kile anachoona ni kulinda maslahi ya uongozi na CCM, ambao yeye ni beneficiary mmoja wao.
Sasa hiyo ndio tofauti kubwa ya uongozi wa Raisi Magufuli na Raisi Samia.