Uchaguzi 2020 Sasa hivi tupo CCM asili na CCM Mpya, hii CCM Mpya ni kikundi kidogo sana cha Bashiru, Polepole na wahamiaji toka upinzani

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,624
870
Chama kimegawanyika vipande vipande kwa sababu ya watu hawa wawili

Hawakuwahi kuwa wana CCM kabisa, wamekuja wameleta aidia za kizamani kabisa wakidhani Watanzania wako stone age.

Hawa wapo chamani kwa maslahi yao tu ya kupata pesa, wala si kufanya chama kisonge mbele hata kidogo

Wale CCM asili Waliokipigania chama hawataki kabisa kuwasikia hawa watu, wamekuja kuvamia chama, na kujiona wao ni bora sana kuliko waliowakuta.

Hawa ndio walikuja na wazo la kununua wapinzani. Unanunuaje mtu mmoja, wakati alipigiwa kura na maelelfu, yaani unachukua mayai, unaacha kuku, kuku ataendelea kutaga, halafu unashangilia umemkomoa kuku

Hawa ndio walimdanganya raisi awekeze mamiradi ya fedha nyingi kuwa ndiyo yatakayompigia kura, leo hatuuziki kabisa kwa wananchi, unamwambia mtu tumejenga fly over wakati yeye anakunywa tope.

Hawa ndiyo walimsapoti raisi wetu, azibe mdomo vyombo vya habari visitangaze habari za upinzani, iwe ni CCM tu, leo sisi tunatafuta raia waje kwenye mikutano tena kwa gharama kubwa, wakati wapinzani wetu, raia wanamtafuta kwa gaharama zao mgombea wao kujua hata yuko wapi

Ndio waliomdanganya ya kwamba upinzani umekufa, wamekaa kinafiki kabisa, leo kwa ground tunapata shida mnoo mpaka lazima tuwalazimisha watumishi woote wa serikali na wanafafunzi kuja kuongeza vichwa kwenye mikutano yetu

Walimdanganya sana mkuu kwamba anakubalika na asijali sana kelele za watu, ona mpaka leo tunafikia hatua ya kupiga magoti kwa raia tuliowaambia watalimia meno...

Yako mengi sana ndugu zangu, lakini kwa kweli tuna hali ngumu, kama chama tukubali tumekosea na hawa watu wawili wamesababisha magawanyiko mkubwa sana chamani. Sasa hivi tupo CCM asili na CCM Mpya, hii CCM Mpya ni kikundi kidogo sana cha Bashiru, Polepole na wahamiaji toka upinzani, ambao hawajawahi kuwa wana CCM, na wamekuja kuchukua nafasi za CCM asili waliokipigania chama

Hawa watu wawili wamesababisha mpaka sasa tume ya uchaguzi na polisi wanaanza kutumika vibaya ili kuokoa jahazi, wakati chama kilipaswa kiwe na nafasi nzuri sana ya kushinda mwaka huu.

RAIS, CHUKUA HATUA. KABLA CHAMA HAKIJAKUFIA RASMI.
 
Ungekuwa umejiunga JF mwaka jana au mwaka huu ningesema wewe ni Bavicha.

List ya wanafiki waliomdanganya Rais na wanaosadia Lissu achukur nchi ni hawa hapa.

1. Mnyeti
2. Makonda
3. Ali hapi
4. Gambo
5. Ole sendeka
6. Pole pole
7. Bashiru
8. Mahera
9. Mtungi
10. Mrema
11. Mbatia
12. Lowasa
13. Rostam
14. Mgombea wa kata( diwani)
15.Mode
16. Kabudi.
17. Kajurumuguli
18. Mambo leo
19.Lau
20. The last but not least... Bashite.

21......the list goes on
 
CCM ya sasa ni chukua chako kupitia tenda za kubomoa chadema kuua upinzani kurejesha mfumo wa chama kimoja, Polepole ameandaa bajeti nyingi za kuidhoofisha chadema kapiga pesa zote kawa tajiri mkubwa kwa mgongo wa chadema, sasa wizi wake unaelekea mwisho hakuna mabaya yasiyo na mwisho
 
Sisiemu itashinda kwa kishindo na tutashangaa na hatutafanya lolote. Hii ndiyo Tanzania iliyojaa watu waoga. Magu songa mbere
 
Ungekuwa umejiynga JF mwaka jana au mwaka huu ningesema wewe ni Bavicha.

List ya wanafiki waliomdanganya Rais na wanaosadia Lissu achukur nchi ni hawa hapa.

1. Mnyeti
2. Makonda
3. Ali hapi
4. Gambo
5. Ole sendeka..
#2 na #20 sijawafahamu hawa bado
 
Mimi nilipoona ule ulinzi wa jiwe miaka mitano ya utawala wake nilijua anataka kufanya mapinduzi kwa mtutu wa bunduki kulinda utawala wake.

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
 
Na akishindwa kujiongezea miaka, huku uraiani ataishiji Kwa Amani ikiwa amejijengea maadui wengi...?

Na Ulinzi atakao kuwa nao ni si kama ule anaopewa na Diwani Kwa sasa...

Nduki
 
Back
Top Bottom