Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,242
- 3,301
Na Jeremy Howell
BBC
Timu ya wanasayansi wa Italia walisema waliweza kwa usahihi kuitambua tarehe ya Sanda ya Turin, na kwamba inaonyesha kuwa ilikuwa ni ya wakati wa Kristo.
Utafiti huu, uliochapishwa hapo awali mnamo 2022, unapinga mtazamo kwamba mabaki ya Sanda hiyo ni "bandia" na inaweza kuwa imetengenezwa katika Zama za Kati.
Utafiti huo, ambao ulichapishwa hivi karibuni, umechapishwa na vyombo vya habari vya nchini Uingereza, Marekani na Ireland.
Wakristo wengi wanaamini kwamba Sanda ya Turin, ambayo pia inajulikana kama "Sanda takatifu," ni nguo ambayo Yesu alikuwa amefungwa na kuzikwa nayo.
Sanda ya Turin ni moja ya mabaki ya kihistoria yaliyochunguzwa zaidi ulimwenguni.
Je, Sanda ya Turin ni nini na historia yake ni ni nini?
Chanzo cha picha,Getty ImagesMaelezo ya picha,Sanda ina damu ya mtu aliyezikwa ndani yake
Sanda ina damu ya mtu aliyezikwa ndani yake, na pia huwa na picha iliyofifia ya mwili wa mtu mwenye ndevu na macho yaliyoingia ndani. Wengi wanaamini kwamba huu ni mwili wa Yesu Kristo, ambao picha yake ilichapishwa kimiujiza kwenye kitambaa.
Sanda hiyo pia ina alama ambazo baadhi ya viongozi wa dini wanasema zinaambatana na majeraha ambayo Kristo aliyapata za mateso aliyoyapata wakati wa kusulubiwa kwake.
Kwa mfano, kuna majeraha mgongoni kutokana na kupigwa viboko na askari wa Kirumi, pamoja na michubuko kwenye mabega kutokana na kubeba msalaba, na majeraha mengine ya kichwani kutokana na kuvaa taji la miiba, kulingana na imani ya Kikristo.
Biblia inasema kwamba Yusufu wa Arimathea aliufunga mwili wa Kristo katika kitani baada ya kifo chake, kabla ya kumuweka kaburini.
Mabaki hayo yaliyoonekana kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1350 wakati mtu aitwaye Geoffroy de Charny alipoiwasilisha kwa kuhani katika mji wa Lirey, mashariki mwa Ufaransa, ambaye alitangaza kuwa ni Sanda ambayo Kristo alizikwa.
Hata hivyo, Pierre d'Arques, Askofu wa Troyes, alihoji ukweli wa jambo hili mwaka 1389 na alichukulia Sanda hiyo kuwa bandia.
Mnamo mwaka wa 1578, Sanda hiyo ilihamishiwa kwenye Kanisa Kuu la San Giovanni Battista huko Turin, Italia, na inaonyeshwa tu kwa umma kwa hafla maalum.
Katika mwaka 1988, wanasayansi kutoka Uswisi, Uingereza na Marekani walifanya vipimo vya utambuzi wa vitu vya kale cha radiocarbon kwenye sehemu ndogo ya sanda hiyo na kuhitimisha kuwa ilitumiwa kati ya 1260 na 1390 AD.
Matokeo ya utafiti wa hivi karibuni ni yapi?
Chanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Sanda ina picha iliyofifia ya mtu mwenye ndevu na macho yaliyoingia ndani, na wengi wanaamini huu ni mwili wa Kristo
Wanasayansi katika Taasisi ya Crystallography nchini Italia, ambao ni sehemu ya Baraza la Taifa la Utafiti, walichunguza nyuzi nane ndogo za hariri ambazo ni sehemu ya nyuzi zilizounda Sanda ya Turin na kuamua tarehe ambayo zilitengenezwa kwa kutumia teknolojia ya X-ray.
Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la kihistoria la Heritage mnamo Aprili 2022, lakini hivi karibuni umepokea umechapishwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari nchini Uingereza, Marekani na Ireland.
Wanasayansi waliweza kupima kiwango ambacho hariri katika kipande cha nguo iliyoharibika kwa muda, na kubaini wakati uliopita tangu kipande cha kitambaa kilitengenezwa.
Timu ya wanasayansi pia ilitumia vigezo vingine, kama vile joto ambalo kitambaa kilihifadhiwa, na kudhani kuwa kipande hicho kilihifadhiwa kwa joto la kati ya digrii 20 na 22.5 Celsius (na unyevu wa kati ya asilimia 55 na 75) kulingana na historia yake.
Wanasayansi hatimaye walihitimisha kwamba Sanda hiyo ilitengenezwa karibu miaka elfu mbili iliyopita, karibu wakati wa Kristo.
Wanasayansi wanathibitisha kuwa njia za kisayansi walizofuata ni sahihi zaidi na za kuaminika kuliko kutumia njia ya kuunganisha radiocarbon, kwani vitambaa kama vile hariri vinaathiriwa na uchafuzi wa mazingira, ambao unaweza kufanya matumizi ya kipindi cha radiocarbon kuwa sahihi.
Sanda ya Turin pia inasemekana kuwa imetengenezwa kwa aina ya kitambaa cha hariri kilichotumiwa katika nyakati za kale na sio aina inayotumiwa katika Zama za Kati.
Mjadala huu kuhusu Sanda ya Kristo unatuelekeza wapi?
Chanzo cha picha,Getty Images
Maelezo ya picha,Mnamo 1578, Sanda ilihamishiwa kwenye Kanisa la Kifalme la Kanisa Kuu la San Giovanni Battista katika jiji la Italia la Turin.
Wasomi wa Italia hawapendekezi kwamba Sanda ya Turin ni kipande cha nguo ambacho Kristo alikuwa amefungwa na kuzikwa nacho, lakini tu kwamba kilitengenezwa wakati huo huo ambao Kristo aliishi.
Matokeo ya utafiti wa wanasayansi hawa yanaweza kuongezwa kwa kiasi kikubwa cha masomo ya awali juu ya amabaki haya.
Tangu miaka ya 1980, zaidi ya utafiti 170 wa kitaaluma yamechapishwa kwenye kuhusu Sanda ya Kristo, wengi wakisema kuwa ni halisi wakati wengine wakisema ni bandia.
Vatican yenyewe pia imebadili mawazo yake mara kadhaa juu ya kama kitambaa kinapaswa kuchukuliwa kama Sanday a Kristo au la.
BBC Swahili