Sanaa ya Muziki katika Ukombozi wa Afrika

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
258
423
Suala ukombozi wa bara la Afrika kutoka kwenye mikono ya wakoloni na ukoloni mambo leo baaada ya ukoloni halisi halikuwa kazi rahisi lilihitaji mchango wa jasho na damu kutoka kwa kila kundikatika jamii ili kuweza kufika mapinduzi ya kweli.

Wasomi walitumia karamu zao kuandika vitabu ili kuwaelezea wazungu machungu ambayo jamii zao ziliyapata kutokana na kutawaliwa kimabavu,
waaalimu waliwafundisha wanafunzi wao elimu ya kujitambua ili waweze
kuanzisha mapambano kuupinga ukoloni.

Waandishi wa vitabu vya hawakusita kuandika maandishi ambayo yangeweza kusambaa na kuueleza ulimwengu kuwa jamii ya Kiafrika ilikua imechoka na maisha ya kukandamizwa na kutumikishwa na ukoloni.

Vitabu vya waandishi nguli kama Peter Abraham wa Afrika ya kusini vilitumika katika
kuhubiri machungu ya watu wa Afrika ya kusini huko migodini na mashambani, kwenye
kitabu kama “The Mine Boy” Abraham alieleza namna ambavyo ugumu wa maisha wa
watu wa Afrika unavyo wafadhaisha na kuhitaji mabadiliko.

Je sanaa ya muziki ilisaidia vipi katika masuala ya ukombozi wa bara la Afrika?

Wajue baadhi ya wanamuziki walio tumia sanaa ya muziki katika kuchochea ukombozi wa bara la Afrika.

Philip Dube maarufu kama “Lucky Dube”. huyu alikuwa ni mwanamuziki wa
muziki wa rege nchini Afrika ya kusini ambaye alizaliwa tarehe 3 Agost 1964 na baadae kuwa msanii mkubwa wa muziki wa rege baada ya kuvutiwa na wasanii wa muziki kama Peter Tosh.

Dube aliamini kuwaa muziki wenye masuala ya kijamii na kisiasa ulio husishwa na rege ya kutoka Jamaica ungefaa kwa hadhira ya Afrika kusini ambayo ubaguzi wa rangi ulikuwa umekithiri.

Enzi za uhai wake Dube alirekodi kanda 22 ambazo zilisaidia sana katika kukuza kujitambua kwa waafrika katika kudai haki
zao, nyimbo kama House of Exile na Freedom Fighter zilikuwa chachu kubwa ya ukombozi nchini Afrika Kusini.

Miriam Makeba “Mama Afrika” alikua ni mwanamke jasiri mpigania uhuru, haki na mwanamuziki nchini Afrika kusini ambaye alitumia miaka 30 ya uhai wake uhamishoni nchini Italia baada ya kukumbwa na msukosuko mkubwa kutoka serikali ya kibaguzi ya kikaburu nchini Afrika Kusini.

Makeba alizaliwa machi 4, 1932 wakati wa uhai wake alipata kurekodi vibao mbalimbali ikiwemo kibao “Pata pata” na “Klick Song” ambapo alitambulika ulimwenguni kote kuwa mwana mapinduzi hata Rais mstaafu wa nchi hiyo Nelson Mandela baada ya kifo cha Makeba alisema Makeba aliimba muziki ambao ulihamasisha nguvu na matumaini miongoni mwetu.

Mwana sanaa mwingine ni Fela Kuti ambaye alizaliwa Oktoba 15, 1938 huko Abeokuta Nchini Nigeria alikua mtoto wa mwanaharakati mtetezi wa wanawake Funmimilayo Ronsome Kuti.

Kupitia sanaa ya muziki Kuti alihubiri masuala ya ukombozi na haki sawa, mwaka 1977 Kuti alitoa kibao chake kilichoitwa “why blackman suffer” kikiwa na tafsiri ya “kwanini mtu mweusi ana- teseka” kikiwa na maudhui ya kumpa uelewa mwafrika katika kupambana na changamoto za kijamii.

Miaka miwili baadae alianzisha chama cha siasa (Movement of People) miaka mitano baadae alihukumiwa miezi kumi na mitano jera kwa kosa la utakatishaji fedha na alipoachiwa alijiingoza rasmi kwenye siasa na maandamano ya utetezi wa haki za kiraia mpaka alipofikwa na umauti 1997.

Kwenye Nyanja ya ushairi huwezi kuzungumzia ukombozi wa Afrika pasipo kumtaja mwandishi mashuhuri “Shaban Robert” ambaye alizaliwa mwaka 1909 mkoano Tanga nchini tanzania na kufariki 1962.

Kazi za Robert zilitumika sana katika kukuza uelewa wa jamii ya watu vitabu vyake vya ushairi kama Pambo ta Lugha (1948),Marudi Mema (1952), Uhuru (1967),Ashiki Kitabu Hiki (1968), Mashairi ya Shaaban Rohert (1968), Mwafrika Aimba (1969) na Sanaa ya Ushairi(1972) vilikuza uelewa wa watu wa Afrika na viliendeleza na kuitangaza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru.

Ni wazi kuwa kazi za sanaa zilitumika ipasavyo na wasanii katika kusaidia ukombozi wa bara la Afrika kabla ya uhuru na baada ya uhuru kwakua wanasanaa wakiwemo wanamuziki walikua na nguvu kubwa ya kuikutanisha hadhira yake na kuielimisha kuhusu ukombozi.

Hata baada ya uhuru sanaa na wanasanaa wamebaki mstari wa mbele katika kuleta mageuzi ya kweli katika jamii ya watu wa Afrika ikiwemo kukemea uongozi mbovu, ufisadi na rushwa ambavyo ni vikwazo vya maendeleo.

Peter Mwaihola.
 
ROBERT NESTA MARLEY (Bob Marley) alizaliwa 06/02/1945 nchini Jamaica na alifariki 11/05/1981 nchini marekani ingawa hujamtaja labda kwasababu sio mwafrika, lakini kwangu mimi huyu ndiye jabari la muziki wa reggae duniani pamoja na nyimbo nyingi za ukombozi na kupinga mbinu za ukandamizaji, unyonyaji na uonevu zinazofanywa na mabeberu.
Vibao vyake baadhi ni;
1.Babylon system
2.Africa Unite
3.War
4.Zimbabwe
5.Get up Stand up
6.Bad Card
7.No more trouble
8.Slave Driver
9.Forever loving Jah
10.Natural mystic
11.Time will Tell
Orodha ni ndefu ila tuishie kusema jamaa alitumia vizuri kipaji chake kuipigania dunia.
 
ROBERT NESTA MARLEY (Bob Marley) alizaliwa 06/02/1945 nchini Jamaica na alifariki 11/05/1981 nchini marekani ingawa hujamtaja labda kwasababu sio mwafrika, lakini kwangu mimi huyu ndiye jabari la muziki wa reggae duniani pamoja na nyimbo nyingi za ukombozi na kupinga mbinu za ukandamizaji, unyonyaji na uonevu zinazofanywa na mabeberu.
Vibao vyake baadhi ni;
1.Babylon system
2.Africa Unite
3.War
4.Zimbabwe
5.Get up Stand up
6.Bad Card
7.No more trouble
8.Slave Driver
9.Forever loving Jah
10.Natural mystic
11.Time will Tell
Orodha ni ndefu ila tuishie kusema jamaa alitumia vizuri kipaji chake kuipigania dunia.
Hakika
 
Back
Top Bottom