Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,625
- 41,095
Mheshimu mjumbe mwema ili upate heshima njema, mtendee wema mjumbe yoyote ili umjue vizuri yule aliyemtuma na msimchukie mjumbe kisa ujumbe wake haukupenda. Mfanye mjumbe kuwa rafiki yako na kamwe usikubali mjumbe kuwa adui yako ikiwa unataka ushinde vita. Hii ni hekima ya kale sana na haijawahi kupoteza maana.
Mjumbe ni mjumbe tu, hana cha kupata au kupoteza moja kwa moja, anachokifanya ni kufikisha ujumbe tu. Kwa Tanzania hii na dunia hii ilivyokaa kwa sasa, Lissu ni mjumbe muhimu mnoo kwa taifa la Tanzania. Kinachompa jeuri na ujasiri ni ujumbe alioubeba na wale waliomtuma. Lissu ana ujumbe!
Chonde chonde, Samia, CCM na Polisi, someni alama za nyakati. Zama zimebadilika mnoo. Nendeni kajifunzeni kwa Nyerere, nini kilimkosa na nini kilimpata alipokuwa akipambana na wajumbe badala ya kupambana na ujumbe. Aliposoma alama za nyakati akaamua haraka sana kung'atuka. Nyerere hakuwa mjinga, aliona mbali sana.
Muulizeni Mzee Mwinyi ni kwa vipi alikubali mabadiliko ya sera za kiuchumi (ubepari) na kisiasa (vyama vingi). Alisoma kwa haraka sana alama za nyakati.
Muulizeni Kikwete, ilikuwaje mapema kabisa 2011 akakubali michakato ya katiba mpya ianze. Alisoma alama za nyakati.
Magufuli alichelewa sana kusoma alama za nyakati, akajikuta anapambana na kivuli tu badala ya kitu halisi, akatumia nguvu kubwa mnoo kupambana na mjumbe badala ya kupambana na ujumbe au kupambana na wale waliomtuma mjumbe.
Mbowe naye alichelewa mnoo kusoma alama za nyakati, huenda chawa waliomzungumka na ahadi ya kupata nusu mkate ilimfanya kipofu, akajikuta yuko nyuma ya muda, kichwa kichwa akaingia kupambana na Lissu, kilichotokea ni kushindwa na kuua Legacy yake yote ya siasa za mageuzi hapa Tanzania aliyoitengeneza kwa zaidi ya miaka 20.
Kushindana na mjumbe inahitaji akili kubwa zaidi kuliko nguvu. Lissu ni akili kubwa sana, ana kipawa na karma yake ya kipekee mnoo katika kufanya harakati zake, ukiona anapambania jambo sasa kwa juhudi kubwa basi wewe jua kwa uhakika alishali 'plot' kitambo zaidi (huenda miaka isiyopungua mitatu nyuma). Na kwa sasa, bila shaka yoyote, watu wenye akili kubwa wameamua na wataamua kuwekeza zaidi kwake ili ujumbe ufike.
Watu wamechoka na chaguzi hewa, sio wapinzani tu, hata wanaCCM, wanausalama, viongozi wa dini, wafanyabiashara, wananchi wa kawaida, wafadhili na wawekezaji hawafurahishwi na hizi chaguzi zetu hewa, zinawaumiza wote. Panya yoyote mwenye ujasiri wa kujitolea kwenda kumfunga paka kengele akiibuka automatically ataungwa mkono tu na panya wote, hata kama ni kwa siri.
Heri nusu shari.....
Mkataa pema.....
Ajidhaniae amesimama.....
Hasira za mkizi......
Lisemwalo lipo........
KIKULACHO KINGUONI MWAKO.