ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,272
- 4,716
Najiuliza hili swali nashindwa kupata jibu, kati ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa na muda wote toka Tanzania iumbwe na Toka kabla makubaliano ya bandari hayajafanyika ni Mbwana Samata, amecheza vilabu vinginna vikubwa , lakini Nina swali dogo.
Mbwana alivofika ulaya alikuwa akipokea mshahara mkubwa na marupu rupu nje ya mshahara, kwa mshahara wake tu alikuwa akilipwa kwa mwezi takribani milioni 450 za Kitanzania, ukitoka Kodi na matakataka mengine anabaki na kama milioni 350 hapo nje ya marupu rupu.
Tunaomjua karibu Samata tunashindwa kuelewa kuwa zaidi ya nyumba ya Kigamboni hatujaona amefanya chochote cha maana na chakueleweka na ndio anafikia mwisho wake. Tofauti na wenzie kina Adebayor, Mane, ambao wameweka alama lakini wamefanya uwekezaji mkubwa sana.
Kama Samata ameshindwa kumanage funds alizopata na anazopata, basi Watanzania inabidi tujiangalie na tujiterekebishe. Katika hili hatuwezi kumlaumu Wema Sepetu, wala Irene Uwoya kwakuwa Samata alikuwa si mtu wa hizo mambo.
Natoa hoja.