JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,688
- 6,484
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC), Salim Abri Asas, amewataka vijana wa chama hicho kumtetea Rais Samia Suluhu Hassan dhidi ya wale wanaomchafua kupitia majukwaa ya siasa na mitandao ya kijamii.
Salim Abri alisema hayo jana chuo Cha Vijana Ihemi Iringa alipokuwa akihitimisha mafunzo ya viongozi 370 wa UVCCM kutoka kata zote za mkoa wa Iringa.
Alisisitiza kuwa kwa kufanya hivyo, vijana hao watamuongezea ari na nguvu Rais Samia kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa ufanisi zaidi.
Alisema kuwa vijana wanapaswa kutumia mitandao ya kijamii kumtetea Rais wao kwa kuandika kuhusu mafanikio yaliyopatikana kupitia serikali ya CCM, kama vile wapinzani wanavyotumia majukwaa hayo kumkosoa na kumchafua Rais.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri Asas akifunga Mafunzo ya uongozi 370 wa UVCCM kata Zote za mkoa wa Iringa Jana katika ukumbi wa chuo Cha Vijana Ihemi.
"Wanatumia asilimia 70 ya hotuba zao kumshambulia kiongozi wetu. Sisi tunataka asilimia 70 ya majibu yetu yawe ya kumtetea Rais wetu. Haiwezekani kiongozi wenu anawafanyia mema, anawatumikia, halafu nyie mnakaa kimya," alisema Mnec Salim.
Aliongeza kuwa lengo kuu la chama cha siasa ni kushika dola.
Alieleza kuwa vijana wanapaswa kutumia mafunzo hayo kwa ufanisi ili kusaidia CCM kuendelea kushika dola na kuwahudumia wananchi kwa njia bora.
"Katika kutawala, mbinu nyingi hutumika. Nchi nyingine hutumia mapinduzi au propaganda kuchafua serikali.
"Sisi Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, na uchaguzi ndio unaamua nani atashika dola. Upinzani utatafuta mapungufu ili ionekane kuwa tumeshindwa, lakini lazima tuzidi kuwa imara," alisema.
Aidha, Mnec Salim aliwataka vijana kuonyesha juhudi zaidi na kuondoa uzembe kwani taifa bado linawahitaji.
Alionya kuwa wasipokuwa makini, wanawake watakuwa mstari wa mbele katika UVCCM.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Agrey Tonga, alimshukuru Mnec Salim kwa kuwasaidia vijana hao, hasa katika ufadhili uliofanikisha mafunzo yao ya siku saba.
Alisema kuwa lengo la mafunzo hayo lilikuwa kuwaongezea vijana maarifa juu ya jinsi ya kuchangia katika maendeleo ya chama, kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa hadi kushika dola.
Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa, Aisha Mapuya, akisoma risala ya umoja huo, alisema mafunzo hayo maalumu yamewapa vijana fursa ya kuelewa serikali inayoongozwa na CCM, nidhamu, maadili, na uzalendo kwa kuzingatia tunu za taifa.
Mapuya pia alieleza kuwa baada ya mafunzo hayo, vijana wamepanga kufanya ziara kuanzia ngazi ya mkoa hadi kata, kuhamasisha wananchi wa rika zote kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.
Pia, alitoa shukrani kwa viongozi wa CCM mkoa wa Iringa, wabunge, na Mnec Salim kwa kufanikisha mafunzo hayo.
Chanzo: Matukio Daima App, Iringa
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri Asas akifunga Mafunzo ya uongozi 370 wa UVCCM kata Zote za mkoa wa Iringa Jana katika ukumbi wa chuo Cha Vijana Ihemi picha na Matukio Daima App