Salamu za Mwaka Mpya za Rais Samia kwa Watanzania

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,201
5,584
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwautubia Watanzania kwa Salamu za Mwaka Mpya Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar, leo tarehe 31, Disemba.


View: https://www.youtube.com/live/rP1BPXBSSOw?si=3xTPsJK6QcZSgSj-
Ujenzi wa Barabara ya Chalinze
Miradi mingine inayotazamiwa kuanza utekelezaji mwaka 2025 ni ujenzi wa barabara ya haraka kutoka Kibaha hadi Chalinze km 78.9, mradi wa ukaguzi wa lazima wa vyombo vya moto chini ya Shirika la uzalishaji mali la Jeshi la Polisi, mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka, na mradi wa ujenzi wa jengo la biashara na hoteli ya nyota nne katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere

Vifo vya Ajali 2024
Mwaka huu pia nchi yetu ilikumbwa na jinamizi la ajali barabarani, takwimu za Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa kati ya Januari hadi Desemba 2024, nchi yetu ilishuhudia jumla ya ajali 1735, ajali 1198 kati ya hizo zilisababisha vifo vya ndugu zetu 1715 hii ni idadi kubwa sana, ndugu zetu wengine 2719 walijeruhiwa katika ajali za barabarani, asilimia 97 za ajali hizi zimetokana na makosa ya kibinadamu kubwa kabisa ukiwa ni uzembe wa madereva

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mwaka huu pia tulikuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika kwa amani na utulivu, katika uchaguzi ule, kwa mara ya kwanza, wagombea ambao hawakuwa na washindani ilibidi wapate ridhaa ya wananchi kwa kupigiwa kura ya ndiyo au hapana, hii imeondosha rasmi utaratibu wa kupita bila kupingwa, ambayo ni hatua kubwa katika ujenzi wa demokrasia nchini.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwautubia Watanzania kwa Salamu za Mwaka Mpya Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar, leo tarehe 31, Disemba.


View: https://www.youtube.com/live/rP1BPXBSSOw?si=3xTPsJK6QcZSgSj-
Mambo ya kishenzi na aibu
Yaani ana onyesha kuwatuonea huruma kwa ajali wakati serikali ya Ccm ina teka watu, na kuwapoteza.

Watuambie ni watu wangapi wame potezwa na wana potezwa na nani?

Akiwa Rais wa nchi ana takiwa atoke hadharani akemee hili jambo.

Alipi potea Ally Kibao alitoa maagizo kwa IGP ya uchunguzi wa haraka

Huo uchunguzi ume semaje? Tume choka na unafiki wa serikali ya Ccm
 
Mbona wewe una kamdomo na haujatekwa? Au sababu ni behind the keyboard hero? Kama hujui kitu bora ukae kimya. Ungeyajua ya ndani ungezungumza lugha nyingine....
Acheni state apparatus zifanye kazi yake!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwautubia Watanzania kwa Salamu za Mwaka Mpya Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar, leo tarehe 31, Disemba.


View: https://www.youtube.com/live/rP1BPXBSSOw?si=3xTPsJK6QcZSgSj-
Nakubali kabisa.Mwaka 2024 umekuwa mwaka wa mafanikio ya kiuchumi ila wenye Changamoto kubwa kwenye uhai wa watu.

Ajali zilikuwa nyingi sana

Matukio ya mauaji na ya kikatili yalishika Kasi

Vita Kila sehemu ya Dunia.

Tunaomba Mungu hayo yasiwepo mwaka 2025.

View: https://www.instagram.com/reel/DEQOpNtq8Mc/?igsh=ODByeHU0MTlhMjE2
 
Mh Rais nakutakia kheri ya mwaka mpya,
Nakusalimu nikitokea mkoa wa Arusha kwenye MTAA WA kula na kunywa pombeeeeeee!


Asante kwa kumteua Mh Makonda maana ni mbunifu Nina hakika ametuweza watu wa Arusha na anasema wazi.anafanya ulichomtuma

Asante kwa lend cruza festival, Asante kwa wadudu, Asante kwa church shoooo, Asante kwa ili la Jana maana limetusaidia kuambukizana KASWENDE GONO NA MARADHI MENGINE KAMA HIV, maana tulikula nyama tukala bia na baada ya hapo tukakulana hadharani, hope next year atakuja na ngono live firstval
. namwomba kwa ilo hasije sema umemtuma Sasa uliyomtuma ayafanye mkoa wa Arusha tumeisha Anza kutosheka Mh Rais, hakika tunaenjoy.


Mh Rais salamu ZAKO za mwaka mpya naomba ikulu MAWASILIANO ikuprintie idadi ya WALIO fatilia hotuba yako na idadi ya WALIO kuwa kwenye Kula bia festival Arusha utaelewa tunako taka utupeleke na sio KUTUIBIA mapambio ya Nini kimefanyika maana unafanya tunaona hakuna haja ya kutwambia na hakuna aliyekuweka ikulu utende mabaya mama
Good morning from Arusha jiji la Makonda.
 
Binafsi natamani kuhamia Arusha kwa jinsi kulivyo noga.
Makonda ni kiongozi bora wa kuigwa.
 
....una falsafa kumbe...
Hawa ndiyo walikuwa wanasema Makonda wakati yupo Dar es Salaam, mikakati alikuwa anampagia Ruge Mtahaba(R.I.P). Na hawachelewi kusema Ruge(RIP) anapendelewa kumshauri kupitia ndoto!!!
 
Mimi na wewe ni nani Mungu kutuweka hai mpaka Sasa...

Nukuu,
""vifo vya ndugu zetu 1715"" sisi ndio tumechaguliwa na bwanaa tupo hai leo tarehe 1/1/2025.
 
RAIS SAMIA: 2024 MWAKA WA KIHISTORIA; MITANO TENA.


Na: Suphian Juma Nkuwi,

Disemba 31, 2024 majira ya saa 3 usiku katika mkesha wa kuelekea mwaka mpya wa 2025, Rais wetu mpendwa, Dkt Samia Suluhu Hassan alitoa hotuba akiuita mwaka 2024 mwaka wa "kihistoria" kupitia vyombo vya habari ambapo aliyataja mafanikio makuu ya Serikali yake kwa nchi, Changamoto kuu na suluhu zake na malengo na vipaumbele vyake kwa watanzania katika mwaka 2025 kama ifuatavyo;

MAFANIKIO;

AMANI NA USALAMA.

Mwaka wa 2025 nchi yetu chini ya Amiri Jeshi Mkuu, Dkt Samia imeendelea kuwa na ulinzi na Usalama imara; mipakani ndani ya nchi na hata katika mali zetu. Bila ulinzi na Usalama hakuna maendeleo wala kukua kwa uchumi.

DEMOKRASIA

Ukiachana na Rais Dkt Samia alivyoruhusu mariadhiano, maandamano, mikutano ya hadhara, uhuru wa Kujieleza, Haki za Binadamu lakini pia katika historia yetu ya vyama vingi, kwa mara ya kwanza hakuna wagombea waliopita kwenye uchaguzi bila kupingwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa bali wagombea wote ambao hawakuwa na washindani walipigiwa kura za ndio na hapana.

Aidha kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 Mhe. Rais Dkt Samia ameruhusu Majadiliano na wadau wa siasa yaliyopelekea marekebesho ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani, Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi na Sheria ya vyama vya Siasa.


UCHUMI

Kwa rejea ya hotuba ya Mhe. Rais Dkt Samia, uchumi wetu unaendelea kukukua kwa kasi ridhishi ambapo takwimu za Januari hadi Juni 2024 uchumi ulikua kwa 5.4 ukilinganisha na 4.8 Januari hadi Juni 2023.

Aisha Deni la taifa limeendelea kuwa himilifu huku Mfumuko wa bei ukiendelea kubaki kwenye lengo la 3% kutokana na Sera nzuri za kifedha.

MAPATO

Kati ya Januari na Octoba Mamlaka ya Serikali inayokusanya mapato (TRA) imekusanya trilioni 21 bilioni 276 sawa na 99.3% ya lengo tengwa kwa mwaka 2024 ikiwa ni ongezeko la 17.5% ulikunganisha na kipindi kama hicho 2023.


Kuendana na ushindani wa kiuchumi katika dunia ya Sayansi na Teknolojia, Serikali imeanzisha UCHUMI WA KIDIJITALI ambapo wizara ya TEHAMA imeanzishwa pakiwepo mkakati madhubuti wa kila mtanzania kuwa na jamii namba itakayotolewa na NIDA.



UWEKEZAJI

Kati ya Januari na Novemba 2024 Miradi mipya iliyosajiliwa nchini ni 865 yenye thamani ya Dola za Kimarekani bilioni 7.7 ambazo zinatarajiwa kuzalisha ajira 205000.

VIWANDA

Mhe. Rais Dkt Samia amesema kwa mwaka 2024 Serikali yetu imetoa vibali kuanzishwa kwa viwanda vipya vikubwa 15 vyenye thamani ya dola za Marekani milioni 235 ambazo zitazalisha ajira 600 na kuuza bidhaa nje ya nchi zitakazobeba thamani ya dola za Marekani 94 milioni kwa mwaka.


DIPLOMASIA

Mwaka 2024 nchini yetu baada ya kufunguliwa kimataifa na Rais Dkt Samia ilipata ngekewa ya kushiriki mkutano wa G20 ambao kati ya maazimio muhimu yatakayoinufaisha nchi yetu ni pamoja na kupata sapoti mbalimbali za kuanzishwa mkakati makhususi wa matumizi ya nishati safi na kukuza kilimo chetu kimataifa.


Katika kupanuka kidiplomasia nchi yetu chini ya Rais Dkt Samia, ilipata ushindi wa Mtanzania Daktari Ndungulile katika kiti cha Mkurugenzi wa Shirika la Afya duniani, WHO kanda ya Afrika. Mungu amrehemu.

Aidha katika Ziara nchi 16 alizofanya Rais wetu Dkt Samia nje ya nchi, kwa hakika zimeimarisha Diplomasia na uchumi wetu kwa kiwango cha kujivunia, mfano;


ZIARA YA KOREA

Ziara hii imesababisha nchi yetu kupata dola za Marekani bilioni 2 milioni 500 ambazo pamoja na matumizi mengine zitajenga Kituo cha kisasa cha reli, Kituo cha anga na urubani, Kituo cha kusambaza umeme Nyakanazi, Kituo cha uchenjuaji madini na Vito, Kuboresha hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Ujenzi wa bandari Bagamoyo, Wete na Kituo cha filamu na burudani cha kisasa.

ZIARA YA CHINA

Ziara hii kwa mara ya kwanza imefungua Soko la mazao ya soya, mihogo mikavu, mabondo ya samaki, mazao ya baharini, mashudu, asali, alzeti na pilipili , pamoja na makubaliano ya Uboreshaji wa reli ya TAZARA.

Katika sekta ya Diplomasia pia, chini ya Rais Dkt Samia kwa mwaka 2024 nchi yetu ilipata fursa ya kusimamia chaguzi katika nchi za Msumbiji, Botswana, Mauritius na Namibia

HUDUMA ZA JAMII

Huduma zote za kijamii ikiwemo za afya , Usambazi Umeme, uboreshaji elimu zimeendelea kuimarishwa, bila kusahau mkakati wa upatikaji maji safi na salama ambapo mradi wa "kumtua mama ndoo kichwani" imefikisha miradi ya maji 1300 nchini itakayosaidia kutimiza lengo la maji safi na salama 95% mijini na 85% vijijini.

KILIMO


Rais Dkt Samia ameendelea kuhimiza Uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara na kusimamia masoko ambapo bei nzuri ya mazao ya kilimo zilizowanufaisha wakulima zimepanda kama ifuatavyo;

UFUTA

Mwaka 2024 Kilo moja iliuzwa 4850 wakati kwa mwaka 2023 kilo moja iliuzwa 3600.

KAHAWA

Aina ya Arabika kilo moja iliuzwa 8500 wakati kwa mwaka 2023 iliuzwa 6500; Kahawa aina ya Rubusta 2024 iliuzwa kilo 5000 badala ya 3500 kwa mwaka 2023.


MBAAZI

Kilo kwa mwaka 2024 iliuzwa 2236 badala ya 2000 kwa mwaka 2023.


KAKAO

2024 Kilo moja iliuzwa 35000 badala ya 29500 kwa mwaka 2023.


KOROSHO

Kwa kilo moja mwaka 2024 iliuzwa 4195 badala ya 2190 katika mwaka 2023.


MIRADI YA KIMKAKATI

BWAWA LA UMEME la mwl Nyerere limeanza kuzalisha umeme megawati 3169 ikilizanganishwa na mahitaji ya megawati 1888.


RELI YA KISASA, SGR

Sasa reli ya SGR linatoa huduma ya usafirishaji kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma ambapo Shirika la reli lilikuwa linasafirisha abiria laki 3 hadi 4 kwa mwaka ila ndani ya miezi 5 ya SGR abiria waliosafirishwa wamefika milioni moja na laki 2 kwa mwaka.



NDEGE

Hadi mwaka 2024 tumefikisha ndege 16, pameongezeka safari 25 ndani na nje ya nchi ikiwemo ndege ya abiria Afrika kusini na ndege ya mizigo kwenda China.


Aidha Abiria waliosafirishwa na usafiri wa ndege zetu kwa mwaka 2024 ni milioni moja na laki moja, na kwa upande wa mizigo iliyosafirishwa ni tani elfu 10.

Mhe. Rais Dkt Samia pia ameboresha viwanja vya ndege vya Arusha, Kahama, Mpanda na Songwe na kuahidi mwaka 2025 kukamilisha viwanja vya ndege vya Iringa, Mtwara, Kigoma, Msalato, Musoma, Shinyanga na Sumbawanga.


CHANGAMOTO

Mwaka 2024 nchi yetu ilikumbwa na Kimbunga Hidaya na maporomoko ya ardhi mkoani Manyara.

Mheshimiwa Rais Dkt Samia amejenga nyumba za kisasa 109 kwa waathirika wa maporomoko ya ardhi Wilayani Hanang na kutoa Bilioni 136 kukarabati Miundombinu iliyoathirika.

UPUNGUFU WA FEDHA ZA KIGENI

Hususani dola, Mhe. Rais Dkt Samia alichukua hatua ya dharura kuunda kamati ya kushughulikia kadhia hii na sasa upatikanaji wa dola umeimarika.


MIPANGO 2025


Kukamilishwa Bwawa la umeme la Mwl. Nyerere.

Kukamilishwa ujenzi wa Daraja la kigongo-Busisi Februari 2025 ambalo hadi sasa limefikia 94%.


Miradi ya kupunguza misongamano katika majiji ya Dar esSalaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma kupewa Kipaumbele na kumalizwa kwa barabara ya mzunguko Dodoma iliyofikia 80% na ya Uyole hadi Songwe Airport iliyofikia 20%


KUANZISHWA SERA NA SHERIA ZA HAKI JINAI ambapo hadi sasa mpango wa Samia Legal Aid umesaidia kutoa huduma za kisheria kwa wananchi 495552.


Watanzania naomba tuendelee kumwamini Rais wetu, na tumchague kwa kishindo mwaka huu 2025 aendelee kutuongoza vema na kutuletea mageuzi makubwa ya kisekta yasiyomithimika hadi 2030.


KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI, NA KAZI IENDELEE!!

Suphian Juma Nkuwi,
Kada- CCM
Januari 01, 2025
Singida,
Simu: 0717027973
 

Attachments

  • 20250101_181105.jpg
    632.4 KB · Views: 1
Wewe ndiyo yule kijana aliyetuhumiwa kuwagombanisha Zito na Maalim kipindi kile, halafu akahamia si si emu! Na baadaye kuanza kuonekana kwenye sherehe za Yuu Dabliu Tii, huku ukishiriki nao kucheza taarab!! Au nimekufananisha!!!
 
Wewe ndiyo yule kijana aliyewagombanisha Zito na Maalim, halafu baadaye ukahamia si si emu! Na baadaye kuanza kuonekana kwenye sherehe za Yuu Dabliu Tii, huku ukishiriki nao kucheza taarab!! Au nimekufananisha!!!
Ni yeye
 

Attachments

  • JamiiForums1049284733.jpeg
    75.4 KB · Views: 1
  • downloadfile-8.jpg
    32.8 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…