Sakata la watumishi hewa: RC Makonda awaapisha wakuu wa Idara wote jijini Dar

ndugu kama ulishafanya kazi huko ukagundua kuna wafanyakazi hewa kwanini hukuwai hata kutoa hiyo Oja,hata kama sio ngazi za juu basi hata jamii forum...??? Hii ni ishara ya kinafiki.
Mbona unakuwa kiazi namna hii, ww una uhakika gani kwamba sikutoa hoja?
 
Mbona unakuwa kiazi namna hii, ww una uhakika gani kwamba sikutoa hoja?
sikuiona ungetoa details,ili tujue ni tatzo mlilolgundua muda mrefu.Alafu kama nyinyi wataalamu wa kusolve hayo maswala mlikaa bila kutulia mkazo kwenye kuyasolve hasa mnataka watu wenye taaluma za siasa wayasolve kama nyny mnavojua.....alafu hakuna kiazi katika kutoa hoja za kuelimishana ndo maana me nmekuuliza swali bila kukutukana.
 
Hapa kazi tu, hakuna sheria ya kumlinda mfanyakazi ukizingua tunakuapisha.
 
narudia tena kukuuuliza unaelewa uandikacho?ushenzi na udhalilishwaji huko wapi,hilo ni suala la ubunifu wa utatuzi wa uyeyushaji wa watumishi hewa,wee unaibgiza na uccm ndani usifikiri sana kwa kutumia masaburi ya nyumbu
 
Safi sana. Mfano mzuri sana huu kwamba unamtaadharisha mtu ya kile kitakachotokea endapo hatotimiza wajibu wake. Hapo hata kosa likitokea mtumishi huyo awajibishwe sawa sawa.

Big up RC Makonda
 


Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda amewasainisha mkataba wakuu wote wa idara kusimamia na kuhakikisha hakuna mtumishi hewa atakayebainika kwenye idara zao.

Katika utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilotoa Machi 15 mwaka huu kwa wakuu wa mikoa kufuatilia na kubaini watumishi hewa, Mkoa wa Dar es Salaam umebainika kuwa na watumishi hewa 209 walioisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni mbili.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Makonda alisema hayupo tayari kuendelea kuona watumishi hewa wanaendelea kuwapo.

Alisema ni jukumu la kila mkuu wa idara kuhakikisha anasimamia eneo lake. Makonda alisema mkataba utaanza kazi rasmi baada ya siku saba.

Alisema baada ya hapo, atakayebainika kuwa na mtumishi hewa, atawajibika katika kulipa gharama zote za hasara alizoingiza kwa malipo yatakayofanyika.

“Nataka ndani ya siku saba hizi mpitie upya, mhakiki watumishi wenu baada ya hapo sitataka kusikia sababu yoyote lazima tufanye kazi kila mmoja kwa nafasi yake na msisubiri kila kitu msimamiwe,” alisema Makonda.

Pia aliwataka wakuu hao kuhakikisha kila mwisho wa wiki wanampelekea taarifa ya kila idara jinsi watakavyofanya kazi.
 
makonda mbunifu sana huyu kijana mungu amlinde atasaidia sana mkoa huu wa dar na kwenye utumishi wa umma kwa ujumla.
 
Makonda Ni Mpuuzi, atakuja Kumletea aibu Kubwa Rais, I wish I was one of them! Kuna Kamnyama Fulani Kanaitwa Squirrel, huwa mimi nakaita Suicide Squirrel kwani saa zote Kana rukaruka, Katarukia mbele ya gari liendalo kasi, Katarukia Kwenye nyaya za umeme, mbele ya treni nk. Saa zote Ni kukurupuka tu. Watu wa aina ya Makonda hawabadiliki wana ADD ni Drama Queens. Ananiudhi sana Na Maigizo yake. Nani amempa Mamlaka ya Kuwaapisha-apisha watu?

Shida anaachiwa bila challenge Kwa Kuwa Rais anamsifu sifu, Makonda is a CCM stooge anayeaminiwa kufanya Kazi za siasa chafu ambazo Vijana Wenye akili kama Akina Mwigulu Nchemba walishazitema.

There is No Polite way to rebuke and challenge this guy, Mnakumbuka wakati fulani Askofu fulani alikuwa na Kesi na akiwa Bado Mahututi Makonda akampelekea Barua ICU anataka naye aende kwake akamhoji, Yaani Polisi waliomhoji yeye anaona walikuwa Wanasesere yeye ndio yeye!

Sheria Tayari ipo Mwizi, Fisadi, Mzembe, Mbadhilifu anatakiwa aachishe kazi na Ashtakiwe kama Rais anavyofanya.
Sio Kuapishwa au Kusomewa Albadiri au Kukemewa mapepo, au Kumwagiwa Maji ya Baraka. (SHERIA TAYARI ZIPO - MKAONDA ACHA MAIGIZO ACHA KUTAFUTA UTUKUFU) Maana sasa Tabia zako Ni Beyond Kutaka SIFA
 
Jamani this is too much,aisee kulipa tena,wallah tukatae unyanyasaji kisa cha kunifanya kuapa,wallah mimi ningeandika notsi ya masaa 24

Na najua Wote hapa hatutetei, Wizi, Wafanyakazi hewa, Safari za Kipuuzi nk. Ila Kuna Wanafanya Vita Hivi Kwa Umaarufu wa Siasa na Kutaka sifa Kwa Rais Bila Kujali Wananchi. Hebu Fikiria Tanzania Iwe na Rais Kama Makonda, Wakati Mwingine Tuanatakiwa Tufikirie, The likes of Makonda are Power hungry people, They will do all they can to get a Political or Corporate Position, and as soon as they get it; everything they do in their newly acquire position is to facilitate their thirsty to secure yet a higher position. In doing so they will destroy, humiliate, abuse, use and crush anybody for such purpose. They are never satisfied with power. Am sure the Likes of him have dreams of being in the top position of the country Government one day, that's why they act the way they do, We must resist them Now. Even when it come to Hon Magufuli,(Whom I still respect and Like) one will be stupid to think that the Idea of running for the office came in his mind in may 2015!
 

mkuu mbona povu hivyo wewe ni KEBWE nin
 
Hii strategy ni nzuri balaaa.....Wanaonufaika na mishahara ni hawa wakuu wa IDARA hasa Ma Afisa ELIMU..na Hii mbinu ingeenda hadi kwa wakuu wa Mashule maana hawa ndo wanajua wafanyakazi wao...Hili la wafanyakaz hewa nalichukia sana maana waTanzania wengi hawana Ajira imagine hao watumishi hewa 10250 si ni ajira hizo za watanzania ambao wangekua wanasaidia wazazi wao na jamaa zao...Hili la MAKONDA linapaswa kuigwa na Wakuu wote wa MIKOA lakini nishauri WAKUU WA MASHULE nao wale viapo sawa na vya wakuu wa idara maana Afisa elimu pekee hawez beba mzigo pekeake....BIG UP PAUL MAKONDA for this approach am sure many ghost workers will b caught....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…